Njaa haina huruma

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
10,344
14,120
Usimuone mtu TUMBO limemvimba kama mpira unaokaribia kupasuka kwa kujazwa sana Upepo.
Ukatamani kupata Tumbo kubwa kama hilo,
77e3f5a2747a40cee451e61decbac1e5.jpg

Usiombe kuwa na NJAA iliyokomaa kwani NJAA iliyokithiri ndiyo inayozaa TUMBO kubwa kama pipa (KITAMBI)
usione vingozi wanatunyanyasa, wana tupeleka peleka kama mizigo chanzo chote cha hayo ni NJAA.

matokeo mabaya ya NJAA yanaweza yasionekane pApo hapo, lakini punde tuu NJAA itakapo zihirisha madhara yake ni Hatari, vilio na simanzi.
c339c93da69e6626d90bfc742a399b6c.jpg

MLAANI sana yule anaekuombea NJAA,
Mpende na kumthamini sana yeyote anayekujali na kukufanya USHIBE, japo muda mwingine SHIBE ikizidi inaweza kukufanya ukashindwa kuwajibika ipasavyo.

NJAA ndio inayosababisha wadogo zetu wafeli vibaya mitihani yao,

RUSHWA, UKAHABA na UJAMBAZI chanzo si kingine ni NJAA.

VIONGOZI wenye uchu wa madaraka wanatamani KUSHIBA, WASHIBE wao tu huku wakisahau nyuma yao tupo watu lukuki tunaotegemea Busara na Hekima zao. Wanatunyanyasa na kutuzarau lakini tusiache kuwaombea maana NJAA imewajaa kwenye matumbo yao. Labda ipo siku watashiba, watarizika kisha watatukumbuka na sisi tutesekao, kucha kutwa tusijue wapi pa kupata mkate na maji ya kupooza NJAA zetu.

WANASIASA wenye akili ndogo kama kichwa cha SISIMIZI, Wasio na Huruma, wanaiba mali zetu.
Wanatumia njaa zetu kama ngazi ya kujinufaishia. Kwenye kampeni Wanakuja kwa nyuso za Ukarimu wakijua wazi Matumbo yetu yanauma, Yananguruma kwa NJAA, wanaturushia MICHELE na SUKARI kama warushiwavyo kuku na mfugaji.


f23ee35841e846c6ec2e33db02772c3a.jpg


Nina njaa ya miaka nenda miaka rudi huyu ameniomba KURA
Namchagua nikitegemea nitasahau NJAA inayonitesa.
ila hali inanigeukia ata kile chakula cha akiba nilichojitahidi kukitafuta BWANA HUYU amekichoma na kukiteketeza chote, NALIA kwa uchungu machozi hayatoki, Tumbo lina NJAA sijui wapi pa kulipata tone la maji ya matunda.

Nakuombea SHIBE Rafiki yangu unaesoma Ujumbe huu, Nawaombea Shibe iliyokithiri wote wanaotumia madaraka yao vibaya huku wakijisahaurisha kuwa sisi wananchi ndio mabosi wa WIZARA zote. Maana kwa Kodi zetu ndiyo inayowafanya WABUNGE kuwa BUNGENI, KODI zetu ndizo zinazo wazungusha MAWAZIRI HUKU NA HUKO, hata hizo harakati za WIZARA kuamia DODOMA zinafanikishwa na Kodi zetu wananchi.

RAis wetu mpendwa kwa Kodi na KURA zetu ndizo zilizomfikisha pale alipo na dizo zinazo mpa nguvu ya kufanya yote anayo yafanya.
Naamini ipo siku sisi wenye Njaa na Viongozi walioshiba, tutashiba pamoja. Majambazi, Makahaba na wala Rushwa wote wataacha hayo kutokana na shibe.
Ni MiMi ninaye teswa na njaa
IDDY MHANDO
 
Wanasiasa wetu wote wana njaa. Wanapiga sana kelele, wanagonga meza, wanashinda kwenye nyumba za ibada, wanavamia taasisi binafsi na kutisha kuchapa watu viboko na mwisho wanatuomba tuwaombee. Njaa njaa njaa njaaaaaaaa.
 
Wanasiasa wetu wote wana njaa. Wanapiga sana kelele, wanagonga meza, wanashinda kwenye nyumba za ibada, wanavamia taasisi binafsi na kutisha kuchapa watu viboko na mwisho wanatuomba tuwaombee. Njaa njaa njaa njaaaaaaaa.
Wacha kabisa
 
Back
Top Bottom