Ni muda tu umepita tangu nitoke nyumbani ambako ndiko nimekuja na maswali njiani
Nilikwenda nyumba ni kupeleka ka mzigo flan hivi ambako kabla ya kwenda huko nilikuwa nimekwenda kumpa pole jamaa yangu mmoja hivi ambae alikuwa amepata msiba wa mdogo wake,nilipotoka kwake nikaona sio mbaya nikapitia nyumbani na nikaweka haka kamzigo
Wakati natoka na kufunga mlango alifika mpangaj mwenzangu pale nyumbani ambae ni jamaa yangu pia na kama mnavyojua nyumba zetu za kiswazi,ukitoka tu nje ya chumba chako unakutana na chumba cha jirani yako,tulisalimiana na kuanza kuulizana za maisha na wakati tuko kwenye salam alipita binti ambae nae ni mpangaji kama sisi akitoka kuoga bafuni kwani bafu lipo pembeni ya nyumba kama kawaida ya nyumba za uswahilini huku amejifunga kijikanga kimoja tu huku khanga hiyo ikishindana nguvu na maji ambayo yalikuwa yanailazimisha ikamatane na mwili
Baada ya kumuona kila mmoja wetu alijikuta akikaa kimya kwanza na kuanza kumtupia macho binti yule na kila mmoja kati yetu akiwaza lake na alipoondooka kwenye upeo wa macho yetu tukawa kama tumekurupuliwa na nilianza kumuambia yule mpangaji mwenzangu kuwa 'aisee Mungu nae bana anaumba wakati mwingine",jamaa yangu alicheka kidogo na kuniambia kuwa "we acha tu'
Nilitafakari kidogo na nilimuuliza kama na yeye anadhani kuwa yule dada anafanya kusudi au laa akaniambia kuwa inawezekana ni kusudi lakini nilimuambia kuwa wakati huyu dada anaingia bafuni hatukuwepo huenda alikuwa anajua kuwa hatupo kama ilivyo kawaida yetu,jamaa alikubaliana na mimi na maongezi yaliendelea na kuanzia pale mada ilibadilika na kuwa ya yule dada
Nilimuambia vile ambavyo yule dada alikuwa ameumbika na kiukweli nilimuangalia kwa uchu lakini nilibakia kuangalia tu kwani yule daa pale kaja kwa muda na anaondoka keshokutwa,nilipozidisha masifa yule jamaa yangu aliniambia kuwa kinachonifanya nimsifie sana yule dada sio kingine ni "njaa' tu na wala yule dada sio kwamba kaumbika kama nilivyokuwa namuelezea
Baada ya hili jamaa yangu aliniabia kuwa yeye ana mpango wa kuoa muda wowote kwani "njaa" imemchosha na hapo ndipo nilipopigwa na butwaa na kumuuliza sababu ya kuoa kwa kusukumwa na "njaa"
Alinijibu kuwa kwa anavyojua yeye karibu kila anaeoa au kuolewa hufanya hivyo kwasababu ya "njaa" na sio kingine,baada ya kusema hayo niliona muda unakwenda na bsdo sijaingiza chochote siku ya leo hivyo kutishia kupata mlo wa usiku na ilibidi nimuage ili niwahi kibaruani,niaji nilikuja huku nikitafakari sana kama kweli kuoa kunasababishwa na "njaa" au kuna sababu nyingine
Kwakweli sikujua kama maneno ya yule jamaa kama yana ukweli wowote ule na kichwani mwangu kwa kadiri nilivyokuwa natafakari sikuona kama kweli kuna siku "njaa" itakuja kunifanya nioe japokuwa "njaa" nayo ni "noma" na ina mavurugu ambayo ni khatari ..lol
Hebu nisaidieni hapa ni kweli kuwa watu wanaweza kuoa au kuolewa kwasababu tu ya kupelekeshwa na "njaa" au kuoa/kuolewa kunatakiwa kuwe na sababu nyingine?
Ngoja niseme tu kweli kuwa suala la "njaa" binafsi haliniingii akilini kunisababisha nioe
Haebu niambie wewe unaoneje hili ........