mazojms
JF-Expert Member
- Sep 22, 2017
- 1,625
- 2,546
- Habari za wakati huu mabibi na mabwana wa humu jamii forum. Tuachane na salamu maana lengo la kuandika uzi si kusalimu watu.
- Nimesikia habari za kubadili mtaala wa elimu na nimesikia maoni mbalimbali. Personally nafikiri mtaala uliopo hauna shida.
Hakuna mtaala utakaoanzishwa au utakaokuja kuanzishwa dunia hii ambao utamfundisha mtu namna ya kujiajiri ( In 3 simple steps[emoji3][emoji3]). Hakuna mtaala ambao utamfundisha daktari anatomy pamoja na namna ya kujiajili. Kujiajili ni matokeo ya elimu iliyotolewa kikamilifu.
- Yani leo tumesahau matatizo ya elimu yetu na tumeamua kujificha kwenye kichaka cha mtaala?
Mtaala hata uwe vipi hauwezi kusaidia chochote kama utekelezaji wake si kamilifu.
Je, mtaala uliopo unatekelezwa kikamilifu? Utasemaje mtaala unamapungufu wakati utekelezaji wake si kamilifu? Mtaala una mapungufu au utekelezaji wake ndio wenye mapungufu? Na je mabadiliko ya mtaala yatazingatia madhaifu tunayoyaona katika utekelezaji?
Sisemi kwamba mtaala hauhitaji mabadiliko, lakini je tunazo takwimu za kutosheleza zinazoonyesha bila shaka kwamba mtaala ndio unashida na unahitaji mabadiliko na sio udhaifu katika utekelezaji wake?
Wengine tumesoma shule ambazo hata maktaba zake zilikua hazina vitabu na labs zisizo na vifaa vya kutosha. nakumbuka mazingira mabovu ya shule yalinifanya nisome nikijali kufaulu zaidi kuliko kufanyia kazi kile nilicho elewa. Alafu leo nasikia eti mtaala ndio unashida lets be serious guys.
● Ni shule ngapi zisizo na walimu wa kutosha?
● Je Mazingira ya shule zetu yanaruhusu elimu kutolewa kwa ukamilifu?
●Je walimu wamekua motivated vya kutosha kutoa elimu kikamilifu?
● Je miundombinu ya shule zetu inaruhusu kutoa elimu kwa ukamilifu?
● Ni shule ngapi zinatoa elimu zikizingatia mabadiliko ya technolojia? Na je vijana wanaandaliwa kukabiliana na mabadiliko hayo? Je kijana anaweza kujiajiri kwenye technolojia kama haijui technolojia yenyewe?
● N.k
Kuna msemo unasema " you are what you eat" kwa maana ya kwamba kile mwanafunzi anachopokea ndicho mwanafunzi anachokua (Mwalimu pia ni mwanafunzi wa zamani). Utekelezaji mbovu wa sera za elimu ndio tatizo lililotufikisha hapa.
Ni hayo tu.