Nivumilie au?

𝕄𝕜𝕦𝕦 𝕙𝕦𝕪𝕠 𝕡𝕚𝕘𝕒 𝕔𝕙𝕚𝕟 .....𝕜𝕚𝕜𝕦𝕝𝕒𝕔𝕙𝕠 𝕜𝕚 𝕟𝕘𝕦𝕠𝕟 𝕞𝕨𝕒𝕜𝕠 .....𝕞𝕨𝕒𝕟𝕒𝕦𝕞𝕖 𝕞𝕡𝕒𝕞𝕓𝕒𝕟𝕒𝕛 𝕀ℕ𝔸 𝔹𝕚𝕕 𝕒𝕞𝕡𝕒𝕥𝕖 𝕞𝕨𝕒𝕟𝕒𝕞𝕜𝕖 𝕞𝕡𝕒𝕞𝕓𝕒𝕟𝕒𝕛𝕚
 
Mkuu naombaa mpambanuo wa matumizi ya 2500 ya chakula kwa siku,mnakulaa nini
 
Ukifunga utafanya biashara gani mkuu?na kwa mtaji upi?hizo ni hatua tu,tofauti ya wanaofanikiwa na wasiofanikiwa inaanzaga hapo hapo kukata tamaa kirahisi.
 
Pambana kwa nafasi yako mkuu we mpe option ya kuondoka kama ana ona hayawezi hayo maisha
 
Pambana mwanaume mwenzangu,usikatushwe tamaa na changamoto.Komaa mpaka baada ya miezi mitatu utaona matunda
 
Biashara ina wiki kadhaa tu unataka uache? Kaa miezi kadhaa uone matokeo.
Mkeo mmeoana au mmebebana tu?
Tafuta maisha!
 
Acheni kuonea wanawake yani mtu afurahie ela ambayo hata mahitaji muhimu tu haikidhi yani mnataka apretend.. Swali kwani wewe siku ulioingiza hyo 12500 ulijsikiaje ilikuwa sawa na ulipoingiza 2500?

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
Mpuuzi kweli wewe.Yaani hapo unaona anamuonea mwanamke? Yaani mtu amepambana badala ya kurudi mikono mitupu amerudi na kidogo bado unaona unaonewa? Kwanini wewe usiende kujitafutia hicho kiasi unachotaka? Kwani Umempendea mapenzi ya kweli au ni tamaa ya pesa na unapretend hali ya kuwa upo kimaslahi?
 
Kama haamini mauzo na faida muweke siku moja kwenye hiyo biashara aone mauzo yake.
Hapana! Asimuweke hapo auze atamuibia na jamaa atafilisika kwa mtaji mpaka kukata tamaa! Huyo demu inaonekana anatamaa!
 
mkuu usidharau.. hiyo 2500 huku mbeya..ni kubwa saanaa.. ukiwa na mchele na unga ndani ..
 
Mwanamke hatakiwi kujua kama umepata au umekosa mkuu...
 
Hongera kwa kutokata tamaa.

USHAURI

Umiza kichwa kufuata wateja walipo

Usimwambie mwanamke kipato chako cha siku,hao ni kama watoto. Iko siku atakuumiza kichwa ujione hutafuti au mzembe kumbe ni riziki na siku,


Badala yake,timiza majitaj hata kwa kukopa ila usimwambie Leo,hunahela au unayo..wewe n baba wa familia(couple family)


MTANGULIZENI MUNGU.MTAFIKA MBALI
 
Pole sana kwa changamoto unayopitia, kama vipi mkabidhi hiyo biashara ya Samaki wewe uangalie njia nyingine ya kupambana ukiwa kama Mwanaume haba na haba hujaza kibaba.
NB : na akija kuleta Uzi kua mwanamke alimpa mtaji wake wa samaki kaula na dume jengine Nadhani kitachoandikwa hapa huu Uzi ataujutia maisha yake kwa mawazo yako ulompa
 
Usimshauri hichi kitu kumbuka hapo alipo tayar anahudumia vichwa viwili inamaana akija mtoto tayr kichwa cha 3 hicho je ataweza kuvitunza kwa elfu 2500
Akili ndo itapanuka vizuri

Atatafuta namna ya kuongeza kipato
 
Aise dogo umri wako bado sana mwache aondoke pambana upate japo biashara yenye faida walau 10 per day.

Maana hapo ukijichanganya ukapata mtoto/ujauzito utatamani ardhi ipasuke. Kulea mtoto ni kazi sana utazeeka chaap. Ushauri wangu mwache aondoke ujipange kwanza ukae vizuri kimaisha 2500 haiwezi kutumza familia zaidi utawatesa tu member wa familia yako.
 
Hebu mkae chini na wife mpange namna ya kukuza hiyo biashara yenu, nae aingie mzigoni msaidiane. Atafute mama ntilie au hata wanawawake wenzie majumbani apite kuwauzia samaki. Sio akae tu akisubiria kufurahia faida. Mwanzo mgumu ila kama mna nia mtatoboa tu.

Halafu baadae mambo yawe safi umletee nyodo
 
Naunga mkono hata kwa jinsi ilivyo hiyo kazi inamfaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…