Niuze mme wangu kwa mzungu?

Niuze mme wangu kwa mzungu?

fatu2010

Senior Member
Joined
Mar 4, 2014
Posts
173
Reaction score
143
Habari zenyu wana MMU, nikiwa ndio natoka kujirusha mambo ya TGF, sorry kama ntakosea some sp na grammar unajua tena ukishapata maji ya rangi ya mende kizungu kinapanda tuuu!

Anyway story iko hivii, nikiwa zangu club mara napata msg thru whassup;

"Shost hapa sijalala, nina mawazo sana, kesho tuonane unisaidie kitu yani shemeji yako simuelewi kabisa"

Nikauliza "humuelewi vip na yuko anatafuta maisha ulaya, kwani amesharudi shule?"

Akajibu, "tuonane kesho nahisi kuchanganyikiwa kabisa, anasema anatakiwa kurudi bongo mambo yamekuwa magumu ila kama nikiweza tukubaliane amuoe mzungu kwa kuzuga (ili awe raia) huku mi nivumilie tuu afu aje amuache mzungu wakati akiwa tayari ni raia ndio anichukue mimi"

Nikahisi kama castle zangu zimekuwa deluted kichwani, nikasema ngoja huyu anahitaji succinct advice kutoka humuu!

Ninapolala nawaachia wakuu, hii ishu akubali ili mmewe aoe mzungu kwa mda ama agome mmewe arudi baada ya shule? Nijuavyo toka jamaa aende sio haba shost kabadili hata saloon, high heels shoes, yani catalogue na design sio haba. I'm pretty sure kwenda kwa huyu shem kumewasogeza kidogo kimaendeleo (just imagine akiwa dent tu). Na sasa anamaliza so huenda wakafanya over and above the limit.

Sasa je afanyeje, jamaa aoe kwa kuzuga ama arudi tu na masters yake afundishe?

Ushauri please, abh nikiamka nichuje nianze vip kumpanga huyu mrembo
 
We vipi wewe ulle sisitujadili! by the way upo na nani hapo ....ni wa kudumu au umeokota SANSIRO! ukinijibu hay nitakupa professional ushauri na bia zitzisha kichwani
 
Atumie akili huyo huyo rafiki yako( kama sio inakuhusu wewe mwenyewe) akumbuke huyo jamaa anaweza kuwa hana mapenzi na huyo mama wa kizungu atakayefunga nae ndoa, lakini wakiishi kwa muda fulani akajikuta anampenda na hapo ndio mwanzo wa kutelekezwa huyo rafiki yako,

na nani kampa guarantee kuwa akigraduate ndio maisha yatakuwa mazuri zaidi, kila siku si unaskia story za wabeba box ulaya, watu wana masters na phd lakini wanafanya kazi za hovyo, mwambie amshauri mumewe akimaliza arudi bongo, kwenye maisha katika kutafuta tunatake calculated risks, lakini sio za hivo!
Angekuwa yeye ndio yupo huko ughaibuni mumewe angekubali aolewe na zee la kizungu????

Nawaza tu kwa sauti!
 
Amruhusu tu afu na yeye mlete kwangu.
 
Mmhh... Hii haina tofauti na eti nikisafiri mke wangu anifungashie nguo za safari na kisha aniwekee packet tatu za condom eti nijilinde huko niendako. Huko nikipata kimwana akanipa penzi adimu si nitamtelekeza mke wangu. Tope tope kweli hii mada!
 
Atumie akili huyo huyo rafiki yako( kama sio inakuhusu wewe mwenyewe) akumbuke huyo jamaa anaweza kuwa hana mapenzi na huyo mama wa kizungu atakayefunga nae ndoa, lakini wakiishi kwa muda fulani akajikuta anampenda na hapo ndio mwanzo wa kutelekezwa huyo rafiki yako,

na nani kampa guarantee kuwa akigraduate ndio maisha yatakuwa mazuri zaidi, kila siku si unaskia story za wabeba box ulaya, watu wana masters na phd lakini wanafanya kazi za hovyo, mwambie amshauri mumewe akimaliza arudi bongo, kwenye maisha katika kutafuta tunatake calculated risks, lakini sio za hivo!
Angekuwa yeye ndio yupo huko ughaibuni mumewe angekubali aolewe na zee la kizungu????

Nawaza tu kwa sauti!

Mkuu haya maisha haya bana, nawaza ndio angekuwa mke wangu anataka hivyo aaagh! Yani atumike mda wote huo huku najua? Never ever heri tuishi kwa shida tu! Hatari sana ccm wametufikisha hapa
 
Hahahahahah aiseee hatare sana, haya mambo bana! Umasikini ni mbaya mweeee

Nakuunga mkono Umaskini mbaya ndugu yangu......na shida hazina adabu

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mkuu haya maisha haya bana, nawaza ndio angekuwa mke wangu anataka hivyo aaagh! Yani atumike mda wote huo huku najua? Never ever heri tuishi kwa shida tu! Hatari sana ccm wametufikisha hapa

Kaka J tunainyooshea kidole CCM hata kwa maamuzi ya kipum..bav ya kijana mmoja anayefanya masters Ulaya? Ummm...sitashangaa nikisikia CCM inalaumiwa kwa hizi mvua zinazotiririka sasa..
 
Kaka J tunainyooshea kidole CCM hata kwa maamuzi ya kipum..bav ya kijana mmoja anayefanya masters Ulaya? Ummm...sitashangaa nikisikia CCM inalaumiwa kwa hizi mvua zinazotiririka sasa..

Mkuu hujasikia mtu anasema bora awe mbwa ulaya kuliko kuwa mtu Tz? Ccm hawawezi kwepa hii dhambi, nchi imekuwa ngumu mpk watu wanaandika ishu kama hizi-ni shida sana. Maliasili zipo, ardhi ipo uongozi tu ndio shida boss

Ishu za mvua na ccm zinaingilianaje sasa na wewe?
 
Hiyo masters yake haijamsaidia,ameshindwa hata kujua thamani ya mkewe?...umaskini wa akili ni mbaya kuliko wa kipato....
 
Aaah, kwani si kaenda kusoma? Sasa huo uraia anaoutaka wa nini? Mwambie tanzania tunahitaji wasomi kuliko ulaya, amalize masters arudi hapa. Pia mwambie penzi halionjwi wala kujaribiwa, aishi tu kama mgeni amalize hivyo videgree vyake arudie ndoa yake hapa!
 
Nna mashaka na upendo wa jamaa kwa mkewe, huenda ana mwanamke wa kizungu huko anamzuzua sasa anataka ahalalishe tu.
 
Back
Top Bottom