Niutoe wapi ujasiri wa kupima hiv!!

Niutoe wapi ujasiri wa kupima hiv!!

Tasia I

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2010
Posts
1,223
Reaction score
193
Salute wakuu.
Ukweli ni kua mimi sio fuska, ila nimewah kua na mahusiano kadhaa kabla ya haya niliyo nayo sasa hivi.
na kama ilivyo hata kula tunda mara 1tu inatosha kuambukizwa HIV.
kwa sasa nina relation amabayo ni serious na naona kwa umri huu nilionao hii inaweza kua ya kudumu
ikimpendeza Mungu iwe ndoa kabisa!
kabla ya kufika huko natamani sana nikapime HIV ili nijijue ila wandugu ninapata mno hofu??
kila nikiwaza naona kama ni stress naenda kuatafuta ni bora nikae hivi nilivyo mpaka itakapolazimu kupia.
wadau hebu nipeni courage ya kwenda kupima HIV tafadhali!
 
mtafute Mentor mtapeana ujasiri na matumaini ya kwenda VCT mkijiamini,huo ugonjwa uchukulie kama magonjwa mengine akilini mwako ndipo na miguu itapata nguvu ya kwenda kupima lakini kama ubongo wako umejiwekea uwoga hata ukisindikizwa unaweza kufa kwa presha kabla hata hujapokea majibu,hata hivyo utapewa ushauri kabla ya kuchukuliwa vipimo.
 
Last edited by a moderator:
Kwani wewe kinachokuogopesha ni nini mpaka uogope kupima? Ondoa woga pima ujue afya yako coz ata ukwepeje kupima kama unania ya kuolewa nilazima mpime tu tena wote wawili.
 
mtafute Mentor mtapeana ujasiri na matumaini ya kwenda VCT mkijiamini,huo ugonjwa uchukulie kama magonjwa mengine akilini mwako ndipo na miguu itapata nguvu ya kwenda kupima lakini kama ubongo wako umejiwekea uwoga hata ukisindikizwa unaweza kufa kwa presha kabla hata hujapokea majibu,hata hivyo utapewa ushauri kabla ya kuchukuliwa vipimo.
ASNAM asante. Mentor njoo huku mkuu unisaidie naski we ni mjuzi.
 
Last edited by a moderator:
Tumia ujasiri ule ule ulioutumia ku do bila kupima
mkuu ku-do hakuhitaji ujasiri,
na sidhani kama zote ulizopiga?pigwa ulipima kwanza. kama we ulishapima ukajikuta ukopoa usidhani ni
ujanja ni neematu. na utulie........!
 
Kwanza jua kuwa kuugua si kufa, siku hizi watu wanaukimwi wanaweza kuzaa bila kumwambukiza mtoto, ukiwa nao na ukaukubali waweza ishi miaka mingi.

Pia watu wengi wasi wasi nikuogopa kunyanyapaliwa, sasa wewe kama tatizo ni hilo, nenda hospitala ya mbali ukapime wasikokujua. Maana watabibu wetu wengine wanakosa ethics akikujua tu basi mji mzima utajua.

Ni vyema ukiijua afya yako na ukaweza vilevile kujua afya ya mwenzio.

Ni ngumu sana, kuamua kupima. Tatizo pale unapokuwa umepima na ukaambiwa uko positivu watu wengi wanakosa matumaini na kuanza kuwaza hadi wanakufa kwa stress.

Life after HIV test kama ni positive ni ngumu kidogo inahitaji ujasiri wa hali ya juu. So ujiandae sana waone washauri nasaa wanamengi ya kukutia moyo!
 
Vyovyote vile it wont be the end of the world; suppose unao, kipi kinatisha; kuumwa au kufa?
Ni wenye Ukimwi tu ndio wanaoumwa? Nenda Oceon Road au hata hospitali yoyote.
Au kama ni kufa, wenye ukimwi wangapi unaowajua bado wako hai, na waso ukimwi wangapi wamekufa?
Au ni unyanyapaa ndio unaouogopa?

Nenda na mawazo kuwa tayari umeathirika, ili kama ni kweli shock iwe ndogo; ikiwa si kweli then uruke ruke kwa furaha na kuamua kubadilisha staili yako ya maisha.
 
Mawazo mazuri haya na yanatia moyo
 
Usijali si lazima kupima kama hauko tayari!
 
mimi mwenyewe nimepima kwa mara ya pili tena leo hapa niko fresh,
nina furaha na kumshukuru mungu maana njia zangu nazijua mwenyewe..
Kapime tuh usiogope..
 
Kupima yataka moyo ndugu,kuna thread moja nimeianzisha hapa MMU jana,itafute usome experience za watu!!
 
.........kama we ulishapima ukajikuta ukopoa usidhani ni
ujanja ni neematu. na utulie........!

amen tasnia I. Mungu akupe courage ya kwenda kupima
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom