Niungeni mkono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niungeni mkono

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by PHILLIP MOGENDI, Aug 25, 2010.

 1. P

  PHILLIP MOGENDI New Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NIMEFANIKIWA KUWA MGOMBEA WA KITI CHA UBUNGE WA JIMBO LA KINONDONI, DAR-ES-SALAAM KUPITIA TIKETI YA CHADEMA.

  NILIZALIWA WILAYANI KINONDONI, NIKASOMA CHUO KIKUU CHA DAR-ES-SALAAM, NIMEJENGA WILAYANI KINONDONI NA NAISHI WILAYANI KINONDONI PIA.

  BAADA YA DIGRII YANGU YA KWANZA YA SAYANSI YENYE MKAZO WA MAHESABU NA TAKWIMU NILIAJIRIWA NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAMA KATIBU MSAIDIZI WA BUNGE. NILIFANYA KAZI PIA KAMA KATIBU KAMATI ZA BUNGE NA KUSIMAMIA KAMATI YA MAHESABU YA SERIKALI- PAC NA KAMATI YA MASHIRIKA YA UMMA- POC. NILIKUWA MSAURI WA WABUNGE KWENYE KAMATI HIZI WAFANYE KAZI KUZINGATIA KANUNI ZA BUNGE.

  NILIFANIKIWA KWENDA KUSOMA MAREKANI DIGRII YA PILI INAYOITWA KWA KIZUNGU MASTERS OF MANAGEMENT INFORMATION SYSTEMS - MMIS. NILIRUDI OFISI YA BUNGE BAADA YA MASOMO. NILRUDI TENA MAREKANI KUSOMA STASHAHADA YA KIMATAIFA YA USIMAMIAJI MIRADI NA KUFAURU MITIHANI NA KUWA SIFA YA MTAALAMU MENEJA MSIMAMIAJI MIRADI. NIKAFANYA KAZI KWENYE MAKAMPUNI MAWILI YA MAREKANI LILE LA HEWLETT PACKARD- HP KULE HOUSTON, TX NA BAADAE KWENYE KAMPUNI LIITWALO GUIDESTONE FINANCIAL RESOURCES LILILOKO JIJI LA DALLAS, TX KAMA MENEJA MSIMAMIAJI MIRADI.

  BAADA YA HAPO NILIAMUA KUJIAJIRI NA KUUNDA KAMPUNI IITWAYO CORPORATE DELIVERY SERVICE, LLC HUKO WICHITA, KANSAS NA MWAKA ULIOPITA NILIRUDI TANZANIA NA KUUNDA KAMPUNI IITWAYO PHINYA GROUP OF COMPANIES (T) LIMITED.

  NI MANI YANGU KUWA KWA UZOEFU WANGU BUNGENI, ELIMU YANGU NA UWEPO WANGU MAREKANI KWENYE DEMOKRASIA PEVU KUNANIFANYA NIWE NA ARI YA KUJA KUOMBA RIDHAA YA WANACHI WA KINONDONI KUWATETEA NA KUWATATULIA SHIDA ZAO KWA KUSIMAMIA MAENDELEO YA MANISPAA YA KINONDONI KWANI MUNGE ALIYEPEWA NAFASI HIYO AMESHINDWA KUSIMAMIA MIRADI NA MAENDELEO KWA UJUMLA YA KINONDONI AIDHA KWA SABABU YA UWEZO WAKE KIELIMU AU KWA KUTOKUWAJALI WANANCHI WALIOMPA FURSA HIYO.

  ELIMU YA USIMAMIAJI MIRADI WA KIMATAIFA NILIYONAYO NI HAZINA NITAKAYOITUMIA KWA MANUFAA YA WANA-KINONDONI ILI KUDHIBITI MATUMIZI YA MAPATO YA WALIPA KODI. KUNA KERO NYINGI SANA ZINAZOTUSIBU KINONDONI AMBAZO KWA UMAKINI NILIONAO NIKIPEWA RIDHAA YA WNAKINONDONI NITAZISHUPALIA NA KUZITATUA KWA MANUFAA YA WAPIGA KURA WANGU.

  NAOMBA MAONI YENU JUU YA NIA YANGU HIYO. PIA NAOMBA USHIRIKIANO WAKO WA HALI NA MALI ILI NIWEZE KUFANIKIWA KUFANYA KAMPENI MAKINI NA ITAKAYOLETA USHINDI. NI BORA TUMPATE MBUNGE MWENYE ELIMU NA UZOEFU WA KUTOSHA WA SHUGHULI ZA KIBUNGE BADALA YA KUENDELEA KUMRUDISHA MTU YULE ALIYEKWENDA KUJIFUNZA BUNGENI NA HIVI LEO ANARUDI KUWAOMBA KURA WANAKINONDONI NA BILA AIBU ANADAI KUWA KIPINDI CHA MIAKA MITA ALIKUA AKIJIFUNZA NA SASA APEWE ILI AKAFANYE KAZI!

  NAOMBA MSAADA WAKO WA KIFEDHA NA WAWEZA KUTUMA FEDHA KUPITIA CRDB PLC ACCOUNT NUMBER 01J2021601301 JINA NI PHILLIP NYANCHINI MOGENDI.

  PIA WAWEZA KUWASILIANA NAMI MOJA KWA MOJA KUPTIA EMAIL phinya68@yahoo.com, www.phillipmogendi.com na simu: 0719 24 9858, 0767 24 9859, 0786 24 9859.
   
Loading...