CCM mmejipangaje kulipa matrilioni mliyowaibia watanzania?
Kwanini CCM mlishindwa kumwandaa rais awamu ya tano mpaka mkaamua kutuletea mtu anayejiita kichaa?
Kwanini nyie CCM mliuza gesi kwa mtutu wa bunduki kisha mnakuja kutuambia eti tuliibiwa?
Kwanini CCM mnafikiri kinyumenyume? Mfano takwimu zikionyesha uchumi umeporomoka CCM mnasema umekua;
mkiambiwa katiba haifai masikio yenu yanasikia inafaa;
mnasema rushwa ni adui wa haki, lakini CCM mnakumbatia wala rushwa;
mnaandika ilani ya kurekebisha katiba baadae mnaigeuka;
mnaambiwa sheria ya vikokotoo mbovu, nyie mnapitisha kwa dansi na kusasambua bungeni;
yaani kila jambo zuri mnaloshauriwa nyie CCM mnaligeuza kinyumenyume. Kwanini?
Ni upi uhusika wa CCM katika mambo ya utekaji?
(Hasa hasa ile sinema maarufu ya utekaji wa Mo ilisababisha polisi watuletee picha za rangi na kuziita za CCTV a.k.a sisiTV a.k.a nyieTV).
Ni kweli kuwa Ibilisi ndiye baba yenu mlezi wanaCCM siku hizi?