Niulize chochote kuhusu mizimu

YANI MISUKULE KWAKO NI WATU WALIO FUFUKA AU UNAMAANISHA NINI

KAMA UNAZUNGUMZIA MISUKULE INAYOPOTEZWA KIMAZINGIRA MNADHANI MNAZIKA MTU KUMBE NI MGOMBA WA NDIZI BASI NGOJA NIKUACHE KIDOGO MKUU
Kama unaamini hivyo basi hakuna tatizo

Ahsante
 
Tungelikuwa tunapewa options ya jinsi kuwa katika form, ningechagua kuwa MALAIKA.
 
Mizimu ina jinsia?
 
Hilo ni agano
 
Mizimu ya kichawi isikie tu kwa watu ni hatari sana yaana ni full package inavuruga kila kitu kuanzia nyota, kazi, ndoa mwili mpaka biashara na maradhi juu

Kujinasua nenda kanisani au watafute wazee wako wa ukoo
mimi sio Mkristo mimi ni Muislam na wazee wote wamesha fariki Ninao mzimu wa kichawi unaniliazimisha niwe mchawi lakini sitaki unaniharibia kila kitu na mpaka maradhi unanitia nitakuja huko Gamboshi nipambane nao mzimu wa kichawi.Nipate kuutoa usinifuate tena .
 
Wewe ni mkongwe hapa jukwaani unafahamika kwenye ekimu ya kiroho uoande wa tiba asili sidhani kama hilo tatizo hujui pa kulimaliza
 
Kwanza tambua kuwa MUNGU ana huruma sana na viumbe wake kuliko hasira/ghadhabu zake.

Ukiuliza kwanini Ibilis hakuangamwizwa hapo hapo alipokosea ni sawa na kusema kwanini Mungu amekuacha wewe uendelee kuishi ilihali ni mtenda dhambi.

Ibilis yeye hukumu yake ilishapita kitambo anajua kuwa yeye ni wa motoni hivyo anachofanya ni kulipa kisasi kwa Adam kwa kuhakikisha anaingia motoni na uzao wa Adam.

Mungu kashatuonya wanadamu kuwa tusimfanye ibilis kuwa ni rafiki yetu bali tumfanye kuwa ni adui. Yaani sisi na Ibilis ni maadui.

Hivyo ukipotea ni matokeo ya nafsi yako kumfanya ibilis kuwa ni rafiki yako badala ya kumfanya kuwa ni adui. Ni sawa uambiwe mbele yako kuna shimo kubwa ila bado ukakaza fuvu na kwenda kuingia kwenye shimo hilo.

Ibilis baada ya kuhukumiwa moto, alitumia nafasi hiyo kumuomba Mungu kwasababu anajua Mungu ni mwenye rehema sana, hivyo hakuomba toba bali aliomba maisha marefu.Mungu alimkubalia dua lake.
Ni hii ni kuonesha kuwa hata sisi wenye dhambi tukimuomba Mungu kwa dhati basi anapokea maombi yetu na kutujibu pia.

Mungu ni mjuzi wa yote anayajua yajayo na yaliyopita na ya sasa. Kutupa wanadamu mtihani sio kwamba alikuwa hajui tutakayoyatenda humu duniani. Ila alituacha tuishi ili siku ya mwisho tusije kuleta lawama kuwa hatukupewa muda wa kuyatenda mema. Ni kuwa mwisho wa siku kutakuwa hakuna excuse...! Nafasi wote tumepewa na tumechagua yale tuliyoyaridhia wenyewe.

Mungu hapendi maovu ndio maana akaleta mitume na manabii ili kubainisha haki . Alipomuumba mwanadamu alimpa akili na kumbainishia mazuri na mabaya kisha akampa na hiyari ya kuchagua mema au mabaya. Hivyo ukiyafanya mabaya ni matokeo ya chaguzi za nafsi yako mwenyewe
 
Hujui unachokiongea...Mizimu ni sawa na majini!
 
Mizimu Ina nguvu gani Kwa maisha ya watu walio hai?
 
Unaweza kutaja kozi angalau tano unazosoma kwenye hiyo degree yako ya uchawi?

Unaajiliwa na taasisi gani baada ya kuhitimu?
Chuo kinasajili wanafunzi wa ngapi kwa mwaka?
Ni kozi zipi zinazopendwa na wanafunzi wengi?
Kabla ya chuo kikuu je, kuna shule za msingi na sekondari ulizosoma za kichawi?

Chuo kipi maarufu hapa Africa mashariki?
Mna mahusiano na Satanist au freemason
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…