Wewe kama mwenyeji wa lushoto una machungu gani na wilaya yako haswa suala zima la kuvuna na kukata miti.Zamani lushoto ilikuwa inaaminika sana kwa kuwa na miti mizuri na hali ya hewa nzuri lakini siku hizi ndivyo sivyo.
Mfano; Shelukindo alikata miti na kusafisha eneo la wananchi ili ajenge hekalu lake na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.
Wenyeji wa Wilaya hii ni Wasambaa 'wagosi wa ndima' ni wilaya ambayo ipo katika milima ya usambaa, hali ya hewa ni baridi kipindi kikubwa cha mwaka, na kunalimwa sana mazao mbalimbali kama mahindi, makabichi, matunda aina mbalimbali, viazi nk