Nitumieje mbolea inayotokana na kinyesi cha popo?

DENAMWE

JF-Expert Member
Dec 29, 2019
807
805
Naomba ushauri/maelekezo ya namna ya kutumia mbolea inayotokana na kinyesi cha popo kwa ajili ya kilimo cha mboga mboga kama nyanya, mshumaa, pili pili aina zote, bilinganya nk.
 
Tutumia kama unavyotumia nyingine
Matumizi ya mbolea hayafanani.
Matumizi ya samadi si sawa na mbolea za viwandani.
Nimeambiwa mbolea ya popo ni kali kuliko za wanyama wengine.
Inaelezwa kuwa ina naitrojeni nyingi.
Hata hivyo, hata mbolea za viwandani zinatofautiana kati ya moja na nyingine.
SA si sawa na Urea.
NPK/TSP si sawa na CAN nk
 
Mnataka kuibua magonjwa Mtambuka..... hao popo wamesababisha magonjwa mengi sehemu mbalimbali. kula wewe na familia yako hizo mboga na mkae ndani kwenu tu msituletee magonjwa mbalimbali
 
Matumizi ya mbolea hayafanani.
Matumizi ya samadi si sawa na mbolea za viwandani.
Nimeambiwa mbolea ya popo ni kali kuliko za wanyama wengine.
Inaelezwa kuwa ina naitrojeni nyingi.
Hata hivyo, hata mbolea za viwandani zinatofautiana kati ya moja na nyingine.
SA si sawa na Urea.
NPK/TSP si sawa na CAN nk
MTAFUTE AFISA KILIMO MZOEFU
 
Pima PH ya udongo wako kwanza kabla ujatumia mbolea ya aina yoyote, unaweza kuharibu ardhi nzuri kwa kuweka mbolea bila kujua. Kuna maabara nyingi zimefunguliwa siku sio nyingi zinapima Soil Ph na wanatoa ushauri wa kitaalam, ni aina gani ya mbolea uweke au usiweke na kiasi.
 
Back
Top Bottom