Nitumie Moyo au ubongo?

Nitumie Moyo au ubongo?

pipi mti

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
764
Reaction score
515
Wakuu habari,

Nilikua na kademu Fulani ivi na tulipendana zaidi ya sana.Na mapenzi haya huenda yalihimarishwa na changamoto na misukosuko ambayo tumewahi kupitia kipindi cha nyuma.

Kwao ni mkoani Mbeya, na nilikutananae miaka ya nyuma kidogo nikiwa nasomanae chuo kimoja pale mbeya.Ni muda wa miaka mitatu hadi sasa tangu tuachane baada ya kugraduate, na tumekua tukichat sana kwa njia ya simu huku tukiendelea kupanga namna ya kukutana tena japo Mara kadhaa tulikua tukipanga na inashindikana kwa sababu tofauti tofauti.Hivyo amekua akilalamika Mara kwa Mara kwamba amenimiss mno na kila siku ipitayo bila kuniona anaona kama mwaka .

Baada ya kupata nafasi na pesa ambayo ingetosha kwa nauli,ghalama za hotel kwa muda nitakaokaa,gifts ndogo ndogo pamoja na pesa kidogo ya kumuachia nikaona sasa ni muda mzuri wa kumvutia waya.

Katika mazungunzo nikamwambia"Nimepata muda na pesa ya kuja huko na kwa hesabu za haraka haraka nahisi nitakua nimespend kama 1.5 M kukamilisha yote niliyopanga kukamilisha nikiwa huko.Nimeona nikuulize kama nije sasa ivi au nikutumie icho kiasi cha pesa utumie kwa mahitaji yako alafu nije mwakani mwishoni ambapo ndio naweza kupata nafasi nyingine?.

Jibu lake akanijibu eti.
Baby unajua msimu wa sikukuu sio mzuri sana kwa safari , alafu ukizingatia Mimi ni wako tu na nitakutunzia kilicho chako ,Sipendi uteseke kuja kote huku kwa ajili yangu ni bora iyo mwakani mimi ndio nije huko. hivyo nirushie iyo ela tu mpenzi wangu."

Sasa hapa wakuu nishaurini nitumie moyo au akili?maana nikitumia moyo kusema kweli nakapenda bado ila nikitumia ubongo naona kabisa hakafai na wala hakajanimiss wala nini na inawezekana kameshakua kama wale shwaini wa mjini wanaotanguliza pesa mbele.
 
Mkuu ungetumia akili kutokumwambia kiasi ulicho nacho....
Fisi ukimuonesha bucha la nyama lazima ang'ang'anie apate angalau mfupa kwa njia yoyote aidha kwa kukuzunguka wewe au hata kukuuma tu ili apate nafasi ya kutafuna mzoga!!!

Alafu miaka mitatu kama uliwahi mugonga utadhani hadi leo atabaki hivi hivi asipate ile radha? Na wewe umeweza? Usikute ashaolewa na kama kuchat a kuongea na simu basi anaongelea chooni au mumewe a nafanya kazi za kuingia shift za usiku!!
 
Wee na wew falaaa hata Ungekuwa wew ungechagua nini...????? Etii uendee au umtumiee pesaaa..kwani umeambiwaa huko aliko hakuna dyudyuuu... Pesa ndo mpango dyudyu ukute hata saa hiziii ameikaliaa hukoo...
 
Kama unampenda sana sana sana sana sana sana mtumie tu, wala usisikie maneno ya watu. Wakati unaanza naye mahusiano mpaka unamvua chupi yote uliyafanya kwa akili yako. Mtumie tu, pesa inatafutwa na inapatikana ila upendo wa kweli ni ngumu sana kuupata the journey is hard...mtumie usimpoteze huyo mwali.
 
Wanasemaga fuata Moyo na si Akili..

Ningekushauri ufuate vyote viwili, kwa sababu ndio washauri wanaokusaidia kuishi maisha yako, ingawa haitakuwa rahisi.

Kumbuka usifanye haraka kwenye maamuzi yako.
 
Back
Top Bottom