Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Nikiwa kama mwanachama hai wa chama kinachojiandaa kushika madaraka nchini, na nikiwa mmoja ya Watanzania wanaolitazama taifa hili kama lulu ya ulimwengu, nikiwa na akili timamu, nitawasilisha hoja zangu tatu kwa chama changu Chadema ziwe agenda muhimu katika uchaguzi 2O2O.
Agenda hizo ni:
1. Mabadiliko ya mfumo wa ulinzi na usalama.
2. Uraia Pacha
3. Jamii za Wahindi na Waarabu wa Tanzania zitambuliwe rasmi na zishiriki shughuli zozote za utumishi wa nchi katika maeneo yote nyeti ya nchi.
Hoja ya kwanza nimeitafiti na kujiridhisha kwamba maendeleo ya taifa kwa vina vyote katika mlinganyo wa ulimwengu, mfumo wa vyombo hivi kwa sasa ni kikwazo kikubwa sana kufikia malengo.
Hoja ya 2. Nimejiridhisha kuwa taifa linakosa fursa na nyingi na hasa utaalamu na mitaji ya watanzania wenye uraia wa nchi nyingine kwasababu ambazo zimepitwa na wakati kwaulimwengu wa leo, Izingatiwe kuwa sababu kuu ya kuweka zuio la Watanzania walioghaibuni waliopata uraia wa nchi nyingine huko zilikuwa ni usalama hasa baada ya uhuru na kwenye harakati za ukombozi kusini mwa jangwa la sahara na katika kipindi cha Uhujumu Uchumi chini ya akina Sokoine. Sababu hizo na nyingi leo hazina mashiko....
Hoja ya tatu ni kuwa jamii hizi za wahindi na waarabu ambao ni watanzania halisi na tena kimsingi hazina uraia wa nchi zingi bali Tanzania tu, ndizo zinazochangia pato la taifa kwa ujumla kupitia mitaji yao ya uwekezaji nchini, ni jamii zilizo na wataalamu wa fani mbalimbali kama madaktari, wahandisi, na wachumi ambao leo wangeingia kwenye mifumo ya kiutumishi wa nchi kwa nyanja zote wataleta mafaa kwa taifa kuliko kukumbatia kasumba ambazo nadharia yake ni ubaguzi tu kwa raia nchini.
Ziko sababu nyingi sana za kutetea hoja zangu hizi, nitawasilisha hoja na utetezi wake naamini chama changu kitanielewa na kuzipokea hoja hizi kuwa sehemu ya agenda uchaguzi ujayo, na hazuwi agenda tu za maneno ili kujipatia ufuasi tu kama wale wenzetu 2OO5 walikuja na agenda ya OIC walipewa madaraka wakawatelekeza waliowaahidi.
Kisha 2O1O wakaja na utapeli mwingine wa Mahakama ya Kadhi, hawakutekeleza hadi 2O15, wakaja na utapeli mwingine kwamba watagawa milioni hamsini kila kijiji na watagawa laptop kila mwanafunzi wa Tanzania, matokeo yake kila mwanafunzi nchini anabeba dumu la maji na mfagio wa chelewa...
Chadema kama chama imara nchini usanii kwetu mwiko, tunaahidi unaloweza kutekeleza...!
Ili uelewe zaidi faida na hasara ya hoja hizi, soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
MREJESHO;
Nimesoma maoni/hoja za watu wengi juu ya hoja zangu tatu ninazokusudia kwasilisha kwa Chama changu cha Chadema, Hoja zangu hizo ni:

Nimeona kwamba hoja ya kwanza inakubalika bila kikwazo kwa wengi wenu mliochangia, lakini hoja ya 2 na 3 nimeona kuna michango tofauti, kumbwa zaidi hoja ya Tatu wengi hamna hoja za msingi za kuikataa zaidi ya chuki na mitazamo ya kibaguzi tu. Bado naamini hoja yangu inanguvu kuliko zenu.
Nichambue kidogo hoja ya 2 ya Uraia wa Nchi Mbili,....
Kimsingi, Hakuna sababu yoyote ya kiusalama inaweza kuwa justification ya jambo hili la Uraia wa nchi mbili, Watanzania waelewe, msingi wa jambo hili ulitumika kwakuwa baada ya Uhuru nchi yetu ilikuwa sio mwanachama wa ulinzi na usalama wa kimataifa yaani Interpol, ambayo ni polisi ya kimataifa, leo ni wanachama, hivyo hoja ya usalama kwamba wahujumu uchumi watakimbilia nchi nyingine wakishaiba ni DHAIFU na inadhihirisha ujinga na ubaguzi tulio nao kama taifa. Unaweza kujiuliza sababu za kujiunga Inter
pol ni nini ikiwa tunashindwa mambo madogo kama haya ya kudhibiti watu wetu tunaodhani watakimbilia nchi nyingine wakifanya makosa huku.
Ukweli unasimama kuwa makosa mengi yanayowakimbiza watanzania wanaoitwa wahalifu nchini ni makosa yanayotokana na sheria za kisiasa zinazopingwa na jumuiya za kimataifa kama vile sheria ya uhuru wa Habari, Sheria ya Mitandao, sheria ya vyombo vya habari na sheria ya uchochezi ambazo nyingi yazo ni sheria za kikoloni ambazo ulimwengu unazipinga...hivyo mtu aliyetenda kosa la uchochezi kwa sheria ya Tanzania, kosa hilo kwa sheria ya Marekani sio kosa na hatakamatwa na Interpol ikiwa Serikali ya Tanzania itamhitaji ili kufunguliwa kesi...
Na Yericko Nyerere

Last edited: