Nitawashangaa sana kama CHADEMA watajitokeza kusimamisha wagombea uchaguzi mdogo ujao

CCM haitumii nguvu kubwa. Kwenye kampeni za uchaguzi Mdogo umeona Rais ama Waziri Mkuu ama Makamu wa Rais wameenda kwenye kampeni? Turudi kwenu CHADEMA, ni nani ambaye hajashiriki kupiga kampeni? Maana kwa mara ya kwanza nilimuona Lowasa akivaa gwanda kumnadi Salum Mwalimu lakini holaaaa! Sisi tulipeleka akina Kibajaji, Msukuma nk ambao ndio size ya akina Mbowe
Amiri jeshi mkuu aliwakilishwa na Jeshi la polisi! Na kazi kubwa waliyoifanya kwa niaba ya mwenyekiti wenu ni pamoja kumuua Akwilini! Au unadhani wale polisi walikuwa wanamimina risasi kwa bahati mbaya? Mungu amlipe sawa sawa na matendo yake!
 
CCM haitumii nguvu kubwa. Kwenye kampeni za uchaguzi Mdogo umeona Rais ama Waziri Mkuu ama Makamu wa Rais wameenda kwenye kampeni? Turudi kwenu CHADEMA, ni nani ambaye hajashiriki kupiga kampeni? Maana kwa mara ya kwanza nilimuona Lowasa akivaa gwanda kumnadi Salum Mwalimu lakini holaaaa! Sisi tulipeleka akina Kibajaji, Msukuma nk ambao ndio size ya akina Mbowe
Mkuu Mawaziri na Naibu spika wamepiga Kampeni..Au umesahau?
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Kwanza kabisa nitumie fursa hii kuwashukuru Watanzania wa majimbo ya Siha na Kinondoni waliotuwakilisha vema kuukataa upinzani. Kwa yaliyotokea huko Kino na Siha ni dhahiri sasa kuwa upinzani umeishiwa pumzi, umekataliwa, umedharauliwa na unaelekea kufa kifo cha fedheha kubwa.

Kwa sisi wenye busara, tuliwashangaa sana CHADEMA walipojitokeza kugombea majimbo ya Siha na Kinondoni baada ya hapo awali kususia uchaguzi uliofanyika huko Songea, Singida na Longido. Tuliwashangaa kwa sababu tulijua fika kuwa hawatashinda. Pia sababu zilizowafanya wasishiriki majimbo hayo zingali zipo.

Vuguvugu la wabunge na madiwani kujiondoa CHADEMA lingali linashika kasi kwa sasa. Hivi ninavyoandika wabunge 10 wa CHADEMA na madiwani zaidi ya 50 wameshawasilisha maombi ya kutaka kujiondoa kwenye chama chao na kujiunga na CCM. Hili ni pigo kubwa sana kwa upinzani. Tukumbuke kuwa wabunge hawa hakuna anayewalazimisha kuhama. Bali kwa utashi wao na kutambua kuwa walipo sasa hawatimizi majukumu yao ipasavyo. Hawana raha kuwa ndani ya CHADEMA. Wameamua kujiondoa na kujiunga na Team Wazalendo. Swali langu, je baada ya wabunge hawa kutua CCM, CHADEMA watajitokeza tena kushiriki uchaguzi wa marudio? Jumatatu njema.

Nawasilisha
Lazima wasimamishe wagombea ili waineshe dunia jinsi ambavyo haki haitendeki,
 
Sijui wabunge wa upinzani hawajajua ni nini kinafuata, au ni kuweka maslahi ya kifedha mbele?

Nakumbuka kabla ya chaguzi hizi ndogo nilisema humu, upinzani wanaweza kushinda uchaguzi lakini hawatoshinda..

Wabunge wa upinzani hata sielewi wanaendelea kubaki kuwa wabunge ili nini, kwanza hukuna wanachokitaka wakafanyiwa, wanabaguliwa waziwazi.

Njia pekee ya kuonesha dunia kwamba hawaridhishwi na hali hii ya kunyanyaswa ni wote kwa ujumla wao kujiudhulu nafasi zao za ubunge na kuwaachia CCM waendelee kufanya yanayowapendeza.
Naunga mkono hoja .Wabunge wa vyama vya upinzani onyesheni umoja wenu na kutoa maamuzi mazito.Dunia itawaelewa.Jiudhuluni wote ili dunia ione hali halisi iliyopo.
Sisi wananchi sio wajinga, tutawaelewa!

Sikutegemea kama atakuja kutokea mtu atakayewaona wapinzani kama maadui wa taifa, hili ni jaribu kwa amani ya nchi yetu na kwa uweza wa Mungu tutalishinda na tutasimama tukiwa kitu kimoja!
 
Back
Top Bottom