Nitatue matatizo gani ili niwe billionaire?

Edsger wybe Dijkstra

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2019
Posts
244
Reaction score
491
Habari za muda huu wadau,

Katika pita pita zangu Instagram na social network sites zingine nimegundua Bongo humu humu kuna watu wana pesa chafu wanakula le maishaz! Sasa na mm nimechoka kuishi maisha ya kubangaiza na kufanya biashara ambazo hazina potential ya kutengeneza utajiri.

Wadau naombeni ushauri na experience zenu nitatue matatatzo gani in terms of kuanzisha biashara, matatizo ambayo yatani-catapult nipate utajiri.

Na mimi nataka nile maisha aseee.
 
Njia za kupata utajiri hasa huku kwetu bhana nyingi ni ujanja ujanja,sijui huko kwa wenzetu ughaibuni,yani huku lazima ucheze rough ndio utoboe,na hizo huwa ni siri zao huwa hawazisemi,sasa kama umeamua kujilipua we jilipue at your own risk...
Mkuu hamna utajiri ambao ni purely clean ,lazima chenga chenga ziwemo .lakini naamini bado kuna fursa zipo za kupiga pesa kwa njia ambazo ni halali kwa kiasi kikubwa .
 
Utajiri watu wanaupata kwa namna mbalimbali, wapo wanaorithi kutoka kwa wazazi/ familia zao, wapo wanaoupata kwa kuzichanga na kuzamia nchi anayohisi inaunafuu wa fursa, wapo wanaoupata kwa kujifunza kupitia kwenye mitandao kama JF, Youtube, Insta nk, wapo wanao bet, kuanzisha biashara nk. ni wewe tu wakuchek unafiti wapi kwa akili na uwezo ulio nao.
 
Unataka kuwa Billionea na hujui ufanye nini?

Upo tayari kujifunza kutoka kwa mtu ambaye hana net worth hata ya 500 USD?

So, you said Yes

Well, thanks for your vote of confidence, Sasa tuendelee...

... Ni muhimu kuwa na ujuzi wa aina Mbili

#1 Marketing
#2 Product Development

Unaweza kujifunza moja, ila ukitaka kuwa unstoppable basi ni vema ukajifunza hizo skills zote

Haya, twende kwenye Jibu la swali lako

Je, unapaswa kutatua matatizo gani ili kuwa Billionea tena Kipindi cha JPM?

Ni ngumu kukupa Jibu la moja kwa moja, ila naweza kukupa vigezo vya kuzingatia wakati unachagua tatizo la kulitatua

Tatizo hilo ni lazima liwe na sifa hizi

#1 Tatizo ambalo linakumba watu wengi na wapo tayari kufanya chochote kile kutatua kero hiyo

#2 Tatizo hilo liwe linawakumba watu ambao wanauwezo wa kumudu gharama za Kuondoa tatizo lenyewe

Tip,

Watoto wanapanda games, ila hawana hela za kununua hizo games

#3 Tatizo hilo liwe ni WANT na sio NEED

Tip,

Watu wengi (wewe ni mmoja wao) wako na NEED ya kusoma na kujifunza Elimu ya Biashara, ila tupo na WANT ya kusoma Habari za michezo na burudani

Ushawahi kujiuliza kwanini Mwanasports inauza copy nyingi kila siku kuliko vitabu vya Ujasiliamali na biashara?

#4 Tatizo hilo liwe linaweza jutatuliwa kwa muda mfupi, yaani matokeo ya Suluhisho lako yasizidi siku 30 kuanza kuonekana

Tip,

Jiulize ni kwanini Madawa yanauhitaji mkubwa kuliko supplements na foods ambazo ni preventives za magonjwa

#5...

#6...

Zipo sifa nyingi, nahisi hizo juu ni za muhimu zaidi

Unaweza ukajiuliza sana ni bidhaa gani ambazo zitaendana na sifa hizo hapo juu

Well,

Mfano, Tatizo la chunusi & Vitambi kwa Kina Dada.
 
Ahsante mkuu, nimepata point muhimu sana kwenye post yako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom