Uchaguzi 2020 Nitasimamia maendeleo ya kiuchumi nchini "Prof. Lipumba" Lindi

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
Lipumba.jpg

NITASIMAMIA MAENDELEO YA KIUCHUMI NCHINI "PROF.LIPUMBA"

Lindi

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itajenga uchumi wa kisasa wenye ushindani wa kitaifa na kimataifa na utakaohimili misukosuko ya utandawazi, unaokuwa kwa kasi bila kuharibu mazingira, na ambao utakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Kukua kwa uchumi kunahitaji uongozi imara na utawala makini, mikakati na mipango mizuri ya maendeleo na utekelezaji mzuri wa
mikakati na mpango hiyo. Kujenga mazingira mazuri ya kuwekeza, kufanya biashara na ushirikiano wa kimataifa bila kuathiri uhuru wa nchi yetu.

Kuweka misingi ya utawala bora na utekelezaji wa sera utakaohakikisha kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia 8 – 10 kila mwaka kwa miaka kumi ijayo na kufanikisha kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu mwaka 2030.
 
CUF imekufa rasmi kifo cha mende!Kusini ilikuwa ngome ya CUF lakini leo Lipumba anapata watu wachache namna ile utafikiri ni mkutano wa mgombea udiwani?😁😁,dhambi ya usaliti imewalipa!Mlidhani CCM ni rafiki zenu,wakawatumia kuhujumu UKAWA na hatimaye kumuhujumu Maalim Seif!

Baada ya uchaguzi mtabaki kama tambala bovu!What a shame,hustle zote za Lipumba miaka nenda rudi zimeishia shimo la taka!What a waste!
 
Back
Top Bottom