Nitasimama na SIMBA yangu daima

Nitasimama na SIMBA yangu daima

Wakati naanza kushabikia mpira kulikuwa na timu tatu kubwa
, Simba, yanga na Pan. Pan nayozungumzia ni ile ya kina Pondamali, Tenga, Mtagwa, Adolph Rishard, Peter Tino ambayo nusu ya wachezaji wake walikuwa Taifa stars. Ila nilichagua Simba na siwezi kuondoka. It
 
FB_IMG_1709531836499.jpg
 
Kumshindanisha CHAMA na PACIME ni kumjengea presha PACOME bila sababu. Chama ni kama KAMBARAGE aliyeishi Ikulu miaka 23 halafu unamshindanisha na Rais aliyeko madarakani kwa miaka 2. Kushindanishwa na CHAMA inabidi uwe na muendelezo wa mambo mazuri walau misimu 3, sio miezi 6.
 
Nilijitambua kuwa mimi ni SIMBA mwaka 1982, almost miaka 41 hivi iliyopita.. Ni shabiki kindakindaki wa SIMBA sports club. Mimi si shabiki maandazi.

SIMBA ni timu kubwa sana Tanzania, Afrika na duniani kote.. Simba imekuwa role model kwa timu nyingi kwa mengi mazuri iliyoyafanya. Ina mafanikio mengi kitaifa na kimataifa. Inaheshimika na kutambulika sana kuliko hata mpinzani wetu.. Ni mojawapo ya timu maarufu popote uendapo.

Kwa sifa zote hizo
Kwa mafanikio yote hayo
Kwa ukongwe wote huo
Kwa umaarufu wote huo.. Nitaanzaje kuichukia timu yangu hii kwa changamoto ndogo ndogo za kupita?

Kwenye maisha kuna kupata na kuna kukosa
Kuna nyakati za mafanikio na kuna nyakati za maanguko
Kuna nyakati za furaha na kuna nyakati za huzuni pia

SIMBA tunapitia kipindi kigumu lakini si kama maadui zetu wanavyoaminisha watu mitandaoni.. Ni changamoto za muda hazitakuwepo milele.. Ni nyakati za nzige.. Tunazitafakari...hatukati tamaa tunapambana tutazishinda na kuwa imara zaidi.. Washindi zaidi wakubwa zaidi na zaidi

Soka lina matokeo matatu
Kushinda
Kushindwa
Kutoa suluhu
Kwasasa sisi ni washindwa wa muda. Tunaachia nafasi za furaha kwa wengine wanaokua. Ni muhimu kufanya hivi pia.. Huwezi kuwa mshindi daima. Maisha yana pande mbili nasi kwasasa tuko upande wa pili.

Acha kwasasa adui afurahi lakini hili nalo litapita kama mengine yote yalivyopita.

Viva SIMBA.... Viva Forever.View attachment 2525426
i am proud of you
 
Kikosi Cha Simba kimeanza Safari ya kuifuata RS Berkane nchini Morocco Kwenye mchezo wa fainali ya kwanza CAFCC🔥🔥🔥
1747177837483.jpg
 
 
"KWA-MKAPA HATOKI MTU - Hii slogan iliyoanzishwa na Simba SC ndiyo hasa inawaumiza kichwa CAF, RS BERKANE na VIBARAKA wao. Wanahofia kombe litabakia Tanzania, kama hali hii ya kiwanja ipo hivi leo, WHY mechi isichezwe ikachezwe Zanzibar?

CAF waliwapa mashabiki wa Simba SC tunzo ya mashabiki bora Afrika wakiwa hata hawajacheza Nusu Fainali, lakini ile turn out yao kila game na namna wanavyohanikiza ushindi ilikuwa balaa, leo timu ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa. CAF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya CAF inatafuta ahueni ikacheze Zenji kwenye mashabiki 15,000 wanaogopa mashabiki 60,000/ watashusha gharika.

Nafahamu jitihada kubwa zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na Serikali, TFF na Simba SC juu ya kutumia uwanja wa Mkapa., nafahamu namna msimamizi/mkaguzi wa Viwanja wa CAF wa mwanza (Moustafa) ambaye alikuwa Mmorocco alivyokuwa anataka mechi ikachezwe Zanzbar akiogopa Kwa-Mkapa, nafahamu aliyeletwa pia anatoka Morocco 🇲🇦.

Hapa kuna vita ya Morocco 🇲🇦 Vs Tanzania 🇹🇿, kama una kichwa maji pekee ndio huwezi kujua hii kitu. Ila Morocco mpaka sasa wanasaidiwa na CAF kitu ambacho ni hatari sana."

BİN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)
1747346823100.jpg
 
Timu yetu imetua Mji ambao mechi itachezwa tayari kwa Mazoezi ya mwisho hapo kesho kabla ya mechi Jumamosi
FB_IMG_1747362276666.jpg
 
Back
Top Bottom