nilizaa na binti mmoja miaka kumi iliyopita, hatukuoana na wala hatukuwahi kuishi pamoja, hali ya maisha ilinilazimu kumuomba huyu binti mtoto nimlee na alinikubalia, niliishi na mtoto hadi nilipokuja kuoa miaka kama minne baadae,na nina wadogo zake kwa wife, bahati nzuri huyu binti naye alipata wa kumuoa na wana watoto. Sijui ni utoto ama ujinga ...ni kwamba sikuwahi kuwatafuta au kuwaona wazazi au ndugu za huyu binti niliyezaa naye isipokuwa dada yake mmoja tu.
kadri umri unavyosonga naanza kuyaona makosa niliyoyatenda na napata wakati mgumu wa jinsi ya kufanya...
- mtoto wangu kwa sasa ni mkubwa na ana uwezo wa kutambua kila kitu na ni mdadisi mno, shida niliyo nayo ni kuwa hajui na sidhani kama anafahamu kuwa mama yake (mke wangu) sio biological mother wake!
- hawajui babu/bibi, wajomba na ndugu zake wengine wa upande wa mamake mzazi
- SHIDA kubwa hata mama yake mzazi huwa anamwita aunt na hajaonana naye takriban miaka mitano sasa, na hili la kumwita aunt mamake kuna siku aliniuliza ..hivi baba mbona hatuendagi tena kwa yule aunt aliyenipa zawadi ya vigari nikiwa mdogo?! iliniuma mno...
- nitaanza vipi na nitaanzia wapi kumwelewesha mwanangu kuhushu hili???naogopa kwani naona kama nitamvurugia mahusiano yake na wadogo zake pamoja na mama yake (wife)
- huyu binti tayari ana mume wake na ambaye anatambulika kwao, nitafanyaje endapo itabidi kufahamika kwa mzazi mwenzangu huyu?!kuna leo na kesho..na pia sipendi na sitafurahia kusikia kuwa mwenzangu huyu ana mikwaruzano na familia yake (esp.mumewe) kwa sababu yangu ama mtoto, japokuwa mumewe anafahamu na tunafahamiana na kuheshimiana! Binti huyu hatujawahi kugombana hata siku moja
- hali halisi imepelekea kutokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na mwenzangu ....note:mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzangu yalikoma kitambo na huwa namuheshimu mno na sidhani kama itatokea kurudia mahusiano yale...so please futa wazo hilo kama unalo
ninajua nilifanya makosa na nayajutia! ila pia nadhani nina nafasi ya kurekebisha pia, ila kivipi ....ndio mtihani