Nitashukuru mawazo yako!

Kilambi

Member
Apr 3, 2009
94
18
nilizaa na binti mmoja miaka kumi iliyopita, hatukuoana na wala hatukuwahi kuishi pamoja, hali ya maisha ilinilazimu kumuomba huyu binti mtoto nimlee na alinikubalia, niliishi na mtoto hadi nilipokuja kuoa miaka kama minne baadae,na nina wadogo zake kwa wife, bahati nzuri huyu binti naye alipata wa kumuoa na wana watoto. Sijui ni utoto ama ujinga ...ni kwamba sikuwahi kuwatafuta au kuwaona wazazi au ndugu za huyu binti niliyezaa naye isipokuwa dada yake mmoja tu.
kadri umri unavyosonga naanza kuyaona makosa niliyoyatenda na napata wakati mgumu wa jinsi ya kufanya...
  • mtoto wangu kwa sasa ni mkubwa na ana uwezo wa kutambua kila kitu na ni mdadisi mno, shida niliyo nayo ni kuwa hajui na sidhani kama anafahamu kuwa mama yake (mke wangu) sio biological mother wake!
  • hawajui babu/bibi, wajomba na ndugu zake wengine wa upande wa mamake mzazi
  • SHIDA kubwa hata mama yake mzazi huwa anamwita aunt na hajaonana naye takriban miaka mitano sasa, na hili la kumwita aunt mamake kuna siku aliniuliza ..hivi baba mbona hatuendagi tena kwa yule aunt aliyenipa zawadi ya vigari nikiwa mdogo?! iliniuma mno...
  • nitaanza vipi na nitaanzia wapi kumwelewesha mwanangu kuhushu hili???naogopa kwani naona kama nitamvurugia mahusiano yake na wadogo zake pamoja na mama yake (wife)
  • huyu binti tayari ana mume wake na ambaye anatambulika kwao, nitafanyaje endapo itabidi kufahamika kwa mzazi mwenzangu huyu?!kuna leo na kesho..na pia sipendi na sitafurahia kusikia kuwa mwenzangu huyu ana mikwaruzano na familia yake (esp.mumewe) kwa sababu yangu ama mtoto, japokuwa mumewe anafahamu na tunafahamiana na kuheshimiana! Binti huyu hatujawahi kugombana hata siku moja
  • hali halisi imepelekea kutokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na mwenzangu ....note:mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzangu yalikoma kitambo na huwa namuheshimu mno na sidhani kama itatokea kurudia mahusiano yale...so please futa wazo hilo kama unalo
ninajua nilifanya makosa na nayajutia! ila pia nadhani nina nafasi ya kurekebisha pia, ila kivipi ....ndio mtihani
 
Mimi binafsi sioni tatizo lolote hapo!..Nitajibu kwa kila hoja:...1:Mtoto ni wa kumweleza tu, wala hana tatizo, kwani hata akijua kuna shida gani?...je unahisi ataanza kiburi au wasiwasi nini, na uhusiano na hao wadogo zake utaharibika vp?..Usiwe mwoga, likabili jambo hili Mkuu uondoe uzia!..Vinginevyo, dhambi ya kutomwambia itakukula zaidi huko mbeleni.shtuka!...2;.Kwenye ishu ya wajomba/baba wadogo, hata kama itamaanisha kutoa kitu(any token) itabidi ufanye hivyo ili kuweka sawa upepo...Mtoto akishakuwa mkubwa huwa hakunaga malumbano mengi
 
Hilo jambo dogo mweleze mkeo na mkalishe mtoto mkiwa pamoja na mkeo umwambie, na kama mume wa unayemuita mzazi mwenzako mnafahamiana na kuheshimiana basi jambo la mtoto wa mkewe ni dhahiri analielewa, cha msingi baada ya kumueleza mtoto unamwita mama yake aende naye kwao na kumfahamisha bibi , babu n.k kisha siku nyingine unaenda nae wewe mwenyewe na kujitambulisha kwao. kama ni wa elewa na hakuna migogoro basi ushamaliza
 
nilizaa na binti mmoja miaka kumi iliyopita, hatukuoana na wala hatukuwahi kuishi pamoja, hali ya maisha ilinilazimu kumuomba huyu binti mtoto nimlee na alinikubalia, niliishi na mtoto hadi nilipokuja kuoa miaka kama minne baadae,na nina wadogo zake kwa wife, bahati nzuri huyu binti naye alipata wa kumuoa na wana watoto. Sijui ni utoto ama ujinga ...ni kwamba sikuwahi kuwatafuta au kuwaona wazazi au ndugu za huyu binti niliyezaa naye isipokuwa dada yake mmoja tu.

kadri umri unavyosonga naanza kuyaona makosa niliyoyatenda na napata wakati mgumu wa jinsi ya kufanya...
  • mtoto wangu kwa sasa ni mkubwa na ana uwezo wa kutambua kila kitu na ni mdadisi mno, shida niliyo nayo ni kuwa hajui na sidhani kama anafahamu kuwa mama yake (mke wangu) sio biological mother wake!
  • hawajui babu/bibi, wajomba na ndugu zake wengine wa upande wa mamake mzazi
  • SHIDA kubwa hata mama yake mzazi huwa anamwita aunt na hajaonana naye takriban miaka mitano sasa, na hili la kumwita aunt mamake kuna siku aliniuliza ..hivi baba mbona hatuendagi tena kwa yule aunt aliyenipa zawadi ya vigari nikiwa mdogo?! iliniuma mno...
  • nitaanza vipi na nitaanzia wapi kumwelewesha mwanangu kuhushu hili???naogopa kwani naona kama nitamvurugia mahusiano yake na wadogo zake pamoja na mama yake (wife)
  • huyu binti tayari ana mume wake na ambaye anatambulika kwao, nitafanyaje endapo itabidi kufahamika kwa mzazi mwenzangu huyu?!kuna leo na kesho..na pia sipendi na sitafurahia kusikia kuwa mwenzangu huyu ana mikwaruzano na familia yake (esp.mumewe) kwa sababu yangu ama mtoto, japokuwa mumewe anafahamu na tunafahamiana na kuheshimiana! Binti huyu hatujawahi kugombana hata siku moja
  • hali halisi imepelekea kutokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na mwenzangu ....note:mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzangu yalikoma kitambo na huwa namuheshimu mno na sidhani kama itatokea kurudia mahusiano yale...so please futa wazo hilo kama unalo
ninajua nilifanya makosa na nayajutia! ila pia nadhani nina nafasi ya kurekebisha pia, ila kivipi ....ndio mtihani
EEH!mzee....
una dini?kama ndiyo ninakushauri uende kwa viongozi wako wa roho wakupe courage ikibidi uwatumie hata kuyatatua matatizo haya kifamilia
 
lakini pia umenishtua kidogo,inaonekana una hisia za mapenzi na mzazi mwenzio!...hapa sijui nikushauri nin
 
Mimi binafsi sioni tatizo lolote hapo!..Nitajibu kwa kila hoja:...1:Mtoto ni wa kumweleza tu, wala hana tatizo, kwani hata akijua kuna shida gani?...je unahisi ataanza kiburi au wasiwasi nini, na uhusiano na hao wadogo zake utaharibika vp?..Usiwe mwoga, likabili jambo hili Mkuu uondoe uzia!..Vinginevyo, dhambi ya kutomwambia itakukula zaidi huko mbeleni.shtuka!...2;.Kwenye ishu ya wajomba/baba wadogo, hata kama itamaanisha kutoa kitu(any token) itabidi ufanye hivyo ili kuweka sawa upepo...Mtoto akishakuwa mkubwa huwa hakunaga malumbano mengi

thanks mkuu PJ, wasiwasi wangu naona kama inaweza kumnyima mtoto uhuru na raha moyoni mwake, anaweza pia kujenga masononeko kitu ambacho sitaki kimtokee
hili la pili kwa kweli ikitokea kikahitajika chochote niko radhi kwa mikono miwili kutoa , ila sasa nianzeje!?? ..
 
Pole mtu wangu, najua unaumia. Hii ni situation nzito sana, but remember always the truth shall set you free. Its about time umtafute mzazi mwenzio mkiwa na partners wenu hadharani (kwa vile wote wanalitambu) muwekane wazi jinsi ya kuongea na mtot, mtoto amtambue mama yake na ndugu zake. i hope that helps.
 
lakini pia umenishtua kidogo,inaonekana una hisia za mapenzi na mzazi mwenzio!...hapa sijui nikushauri nin
hesima mbele mkuu!! amini kuwa sina na sidhani kama nitakuwa nazo juu yake, sina ugomvi nae na namheshimu mno yeye pamoja na mumewe!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom