Nitashangaa na kusikitika kama hatutampongeza Dkt. Mwigulu Nchemba na kubadilika kwa ukweli mchungu huu

Si kweli kila Mtanzania akiamua Kuacha 'Anasa' au Matumizi ya 'Kipuuzi' na yasiyo ya lazima kuwa na Bima ( hasa ya Afya ) inawezekana. Tujitathmini na tubadilike tafadhali.

Unajua maana ya kila Mtanzania? Nimehamia Mbezi beach, juzi napita karibu na Bahari nakuta familia inaishi kwenye open space yenye gerage ya parking isiyo na milango, wanapika kwa kuni!

Sasa ni starehe gani hawa wanaacha wawe na Bima!? Wasomi wa hii nchi wana mapepo sijui! Nime kaa na huyo Mama na kuongea naye na watoto wake nikaumia sana sana!

Kuna watu (wengi sana) wana shida za kutupa kwenye hii nchi, ukivuka upande wa pili anapokaa huyu Mama there are huge, beautiful, massive Houses na magari ya Kifahari!
 
Du, mbona hoja yako ina kauli kavu na kali ujuaji mwingi mbele giza!

Ati Bima ni Extra cost! Faida ya Bima yoyote huwezi kuiona hadi unapofikwa na shida. Mfano ulio wazi ni pensheni (kwa waajiriwa) ambayo kimsingi ni "bima ya maisha baada ya kustaafu". Je, maisha ya wastaafu yangekuwaje kama haikuwa lazima (kisheria) kulipia pesheni kila mwezi kwa makato ya mshahara?

Ushauri wangu itungwe sheria kila leseni ya biashara iambatane na bima kama ilivyo kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri.

Watu mkishakuwa na vijisent Bwana, mnasahau umaskini wa koo na ndugu zenu!
 
"Watanzania waache kuwekeza sana katika Bajeti za Kunywa Pombe kila mara huku wakishindwa hata tu kukata Bima kitu ambacho nadhani kwa Mtu makini ni muhimu zaidi katika Maisha yake "

Chanzo: Cloudstv 360

Mtani wangu kutoka Mkoani Singida Dk. Mwigulu Nchemba unajua fika kuwa GENTAMYCINE sikukubali kutokana na Uyanga wako, ila nisiwe Mnafiki kwa hiki ulichokisema upo sahihi 100% na nakuunga mkono pia.

Binafsi nitajitahidi sasa nami hizi Bajeti zangu za kununua 'Migoma' ya Kwenu Singida pale Kimboka, Beach Kidimbwi na Maandazi Road Msasani nizielekeze katika Kukata Bima yangu kwani ni Aibu na Upopoma (Upumbavu) kama si Ungumbaru (Ujinga) mkubwa kufanya 'Anasa' huku ukiwa huna Bima yoyote.

Kidogo Mtani wangu Waziri Dk. Mwigulu Nchemba naanza sasa Kuiheshimu hiyo 'Doctorate' yako japo huko nyuma kuna Kauli zako fulani fulani zilikuwa zinanilazimisha nianze Kukupuuza kama si Kukudharau pia.

Unajua kumkejeli mtu kwa kumsifia, yani huu ujinga ndo unataka uutumie ku halali sha Dr yake?

What about those people ambao hawana basic needs Kama shelter and food! Waache nini walipe Bima?

You know when a Politician is telling lies? When he/she opens his/mouth! Nothing straight comes from their mouth!
 
Back
Top Bottom