Nitapataje mabelo ya viatu vya mtumba kwa bei nafuu?

blakafro

Senior Member
May 1, 2014
152
104
Habari wakuu, nimekuwa nikiipenda biashara ya viatu vya mtumba kwa muda mrefu sasa umefika wakati wa kuianza rasmi biashara hii ingawa nimekwama kwa kutokujua baadhi ya mambo nimejaribu kufafuatilia ni kama kuna usiri fulani umekuwepo ukiwauliza wazoefu wa hii biashara kuhusu sehemu wanayochukua mzigo,

Nimekuja hapa kuomba msaada kwa yoyote anaejua sehemu wanapochukulia mzigo hapa nikimaanisha yale mabelo ya viatu kwa uchunguzi niliofanya wanaouza haya mabelo ni wahindi na wanapatikana kariakoo ila ndo sikufanikiwa kujua ofisi zao zipo kariakoo sehemu gani ndio sababu nimekuja kuomba msaada hapa wakuu anaejua naomba anijuze.
 
naamini watakuja jf sio wachoyo usikate tamaa mkuu mpaka ufike hatua ya kulitumia wazo ujue umelisotea kweli ulipo bado pambana
 
Ukifika kariakoo panda Balaji au boda boda watakupeleka kwenye hiyo mitaa.
 
Mimi pia nahtaj vya ofisini(moka) grade A
ila naogopa usije toa laki nne na nusu ukutane na maraba kama ya kangi.
Ukiyapata hayo maraba si unakuwa na permanent customer ambaye ni Kangi aka Ninja!!
JF ni kiboko aisee,kama una ile picha ya Ninja wawekee wadau waone raba za mheshimiwa Ninja!!
 
Back
Top Bottom