Nitapata wapi tabibu au mbobevu wa mifupa hapa Mwanza?

nyamva

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
240
150
Wadau kama kichwa kilivyofafanua, nahitaji daktari mbobevu wa mifupa, kwa kifupi nina mwanangu alianguka kama mwaka hivi akaumia mguu, baadaye mguu ulivimba sana, baada ya kusinyaa kwa kutumia tiba za jadi mguu ulipona, Ila baada ya kupona mguu huo umekuwa mfupi yaani mwanangu anatembea kwa kuchechemea.

Hali hii imekuwa ikiniumiza sana hasa ikizingatiwa alizaliwa akiwa normal. Mwanangu Ana miaka 9 tu. Kifupi nahitaji uchunguzi ikiwezekana tiba ipatikane kwa gharama yoyote iwe kwa bima ama cash.
 
Anzia Hindu mandal kule jiran na BMC coz specialists wote ndo sehem pekee huwa wanapiga tempo kwa wingi toka BMC so inakuwa rahisi kukuunga na BMC vinginevyo utasoteshwa mkuu hii naongea by so many experiences
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom