Naumia sana nikimwangalia.
Kinacho nifanya niumie, wakati namtongoza alikuwa hataki kabisa, lkn nikamlazimisha mpaka akakubali. Tangu hapo amekuwa ni msumbufu sana, yani kwa siku anaweza kufika ninapo kaa hata mara nne.
Hali hii imekuwa ikinipa wakati mgumu sana, ananifanya nimchukie kwani wakti mwingine huwa nahitaji kuwa pekee yangu ili kufanya mambo yangu mengine, lkn bila kutgemea utakuta ameshafika.
Nilijaribu kumweleza kwamba awe anajipa mda kidogo wa kuja kwangu lkn habadiliki. Yuko tayari hata aanzishe safari kutoka nyumbani kwao ya kwenda kununua pipi dukani ili mradi apite kwangu, na hapa ninapo kaa wala sio njia ya dukani kwao lkn hulazimika azunguke lengo apite kwangu.
Huyu binti ni kwamba hanipi hata ule mda wa kummiss, hakuna!
Nataka kumwacha lkn kwa jinsi ninavyo muona ataumia sana, ukizingatia tuko majirani.
Sasa leo kafanya kitu ambacho inanilazimu kumwacha hata kama ataumia..ilikuwa mida ya saa tatu na nusu hivi usiku, wakti nmelala, nikasikia mtu anagonga kwa sauti ya chini sana kwenye dirisha la chumba ninacho lala, sikuitikia akarudia tena kwa mara ya pili. Nikasema ngoja ninyate nichunggulie nani huyu? Kabla sijachungulia akaniita, mm sikuitika na wala yeye hakurudia tena, baada ya kama dk 8 hivi, nikampigia simu uko wapi akanijibu yuko nyumbani amelala, lkn baaadae akashtuka, akaniambia niko kwako, nikamwita asogee dirishani nikamsema sana. Kilicho nikera usiku wote huu hata nyumbani watasema yuko wapi? Ukizingatia yeye ni mtoto wa kike?
Nataka kumwacha lkn nashindwa ntampa sababu gani ambayo atanielewa bila kuumia?
Asante..