Nitakuwa wa Mwisho Kuamini CHADEMA wanahamia Mikocheni

Nitakuwa wa Mwisho Kuamini CHADEMA wanahamia Mikocheni

Mi nawaza tu.

Basi itokee iwe kweli, au kwa sababu yoyote ile patokee tatizo na CHADEMA washindwe kuingia kwenye jengo hilo..., mbona itakuwa ni kizaazaa?

Siyo kwa furaha ya hawa machizi wataniwenu; lakini nahofia tu wananchi watalichuliaje swala kama hili?

Ni jambo dogo, lakini uaminika wa chama utaharibika sana, na hawa hawa machizi ndio watakuwa mstari wa mbele kuwananga kwa wananchi!

Usiombee pawepo na dosari kama hiyo wakati huu.
Lakini ndugu yangu hivi kuhamia Mikocheni ni tamko la Chama? Au hilo jengo lililoonyeshwa na gazeti ni taarifa ya chama au ni tetesi za hilo gazeti?
Sioni kama kuna la kuhofia maana sijaona popote Mnyika kama mtendaji mkuu au Mbowe kama mwenyekiti au msemaji mkuu Mrema kutoa kauli ya kuhamia Mikocheni.
Usikute gazeti limetumiwa kututoa kwenye kadhia ya Bandari yetu.
 
Yani Cute Wife unakubali kuwa na jitu pumbavu namna hii?.

Mwanaume hapaswi kuwa Mbeya namna hii.subiri watu wahamie au washindwe ndio ulete habari.

Sasa ulivojiaminisha hivi wakihamia je? Tutakuja kukuchumbia.
 
Lile jengo kwa sasa ni la Chadema namfahamu hadi estate agent aliyefanikisha dili ile!
Mimi nilikuwa "nikiwaza" tu kwa sauti/maandishi.
Maana ninayolenga ni kwamba wakati huu uaminifu wa CHADEMA kwa wananchi ni kila kitu.
Historia inaonyesha hiki chama kimepata shida sana kuaminiwa na wananchi, ndiyo maana CCM imeweza kutamba miaka yote hii (pamoja na kwamba wanahujumiwa na kukandamizwa na vyombo vya dola).

Lakini jambo kubwa katika yote hayo, ni KUAMINIWA na wananchi, ndio swala muhimu kuliko yote.
 
Lakini ndugu yangu hivi kuhamia Mikocheni ni tamko la Chama? Au hilo jengo lililoonyeshwa na gazeti ni taarifa ya chama au ni tetesi za hilo gazeti?
Sioni kama kuna la kuhofia maana sijaona popote Mnyika kama mtendaji mkuu au Mbowe kama mwenyekiti au msemaji mkuu Mrema kutoa kauli ya kuhamia Mikocheni.
Usikute gazeti limetumiwa kututoa kwenye kadhia ya Bandari yetu.
Ninakubaliana nawe.

Kwa msingi huo wa uliyoyaeleza chama kinaweza kueleza tu kwamba habari hiyo ilikuwa si rasmi toka ndani ya chama.
Watu wenye uelewa watalikubali hilo.
Lakini wapotoshaji bado watakuwa na 'field day' ya kuwananga CHADEMA.
 
Back
Top Bottom