Nitakachofanya hataamini.

Promethazine

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2017
Posts
262
Reaction score
260
Wakuu heshima kwenu.

Miaka ya juzijuzi nilizaa na binti Fulani akiwa bado yupo chuo, muda wa kujifungua ulipofika baada ya mwezi mmoja nilimchukua mtoto kwa kuwa alikua na mitihani (UE), mtoto akiwa na mwezi mmoja, yes mwezi mmoja! Kwa ushirikiano wa sister angu ambaye alijitolea kulea mtoto yule akiwa anafanya biashara zake.

Basi nimekuwa natoa fedha za matumizi bill ya maziwa na mahitaji mengine( akina mama wanayafahamu vizuri zaidi.

Sasa binti juzi nilimuambia kuwa nampa jina mtoto litakalokuwa official atatumia mpaka shule maana jina analotumia mpaka sasa alipewa na babu yake upande wa mama, alichonijibu ni kuwa kakaribia kumaliza chuo aje amchukue mwanae, kuwa kama nataka kumpa jina nitafute mtoto mwingine, yaani hapo hasira yangu iliwaka juu yake ina maana huyu binti ananichukuliaje? Maneno anayonitamkia ni ya dharau sana, kwamba mimi akili zangu ni mbili!!

Wakina mama wanajua kazi ya kulea ilivyo ngumu, Mimi pia nimeingia gharama za kulea mpaka sasa mtoto ana mwaka na nusu.

Sikubali kuchekwa ujinga nitakachomfanyia huyu binti hatoamini maana nilikwishasikia anashirikiana na mama yake watamtorosha mtoto binti atakapomaliza chuo and once he is gone is forever!!! (kwenye hili Nina ushahidi, alishanitamkia kuwa siku nikiruhusu mtoto akaenda kwa mama yake alipoolewa sitampata tena),

Nitakachofanya hataamini nitamhamisha mtoto aende mbali sana, najua atakosa malezi ya mama kuliko kuwa na mama mpuuzi wa hivyo.

Watu wanaachiwa watoto bila msaada wowote wewe unaleta dharau!!!
Sikubali kuchekwa ujinga.
 
Muache amchukue, akikua dogo atakutafuta mwenye mkuu.Huwezi kuwa mjinga mkuu, wewe sio wa kwanza kufanya hivyo ili mladi haendi kumdhulu.
 
Yaani mimi mwanaume akisema achukue mtoto akamlee hata sipati shida. namwachia kwani shida iko wapi.
ila angalia isije kuwa mtoto si wako.. jaribu kupima DNA
DNA mkuu sina imani nayo pia, nilishajitosa mwaka na nusu sasa kulea, kila mtu anajua ni mtoto wangu nikimkataa leo itakuwa ni jambo la ajabu kidogo.
 
Pole sana...

Kwa jinsi ulivyoeleza kama ni kweli usiwaache wachukue mtoto... Huwa naamini sisi wanawake tukiwa na watoto basi mama zetu huwa wanachukua jukumu la kulea mtoto kama kuna dharura kama hizi.

Huyu mama yake alikuwa wapi kushauri mtoto akae nae yeye matumizi upeleke huko Leo ashirikiane na mwanae kutaka kutorosha mtoto! Usikubali.
 
Mama yake na baba yake walishaachana mama kaolewa kwingine na baba yake kaoa kwingine, yeye kakulia kwa shangazi ambaye pia hajaolewa.
 
Fuata sheria mtoto apate haki zake muhimu, weka tofauti zenu pembeni.
 
Mama yake na baba yake walishaachana mama kaolewa kwingine na baba yake kaoa kwingine, yeye kakulia kwa shangazi ambaye pia hajaolewa.
Bado sio sababu ya mama yake kushindwa kumlea mtoto kama kweli walikuwa wanajua wanamuhitaji

Siku zote mtoto ni wa mama
 
Muache amchukue, akikua dogo atakutafuta mwenye mkuu.Huwezi kuwa mjinga mkuu, wewe sio wa kwanza kufanya hivyo ili mladi haendi kumdhulu.
Mama na baba wa binti walishaachana yeye kakulia kwa shangazi ambaye pia hajaolewa.

Mara ya mwisho trial ya kutorosha mtoto kuelekea mama alipoolewa ilishindikana mtoto alikuwa na miezi mitatu.
 
Mama na baba wa binti walishaachana yeye kakulia kwa shangazi ambaye pia hajaolewa.

Mara ya mwisho trial ya kutorosha mtoto kuelekea mama alipoolewa ilishindikana mtoto alikuwa na miezi mitatu.
Umegundua kwanini wanamtaka mkuu?
 
Consider DNA test isije kuwa mtoto anapelekwa kwa Baba yake akapewe jina linalomhusu
 
Bado sio sababu ya mama yake kushindwa kumlea mtoto kama kweli walikuwa wanajua wanamuhitaji

Siku zote mtoto ni wa mama
Mama wa mtoto ni jeuri sana alishanitamkia kuwa nikimruhusu tu aende mama yake alipoolewa sitomuona tena
 
Tufanye umetoa sadaka kumlea na Mungu atakubariki. Usishindane na mwanamke maana wanawake wengine wanazijua ajili zao. Mwache amchukue kwa Moyo wako wote na uendelee na maisha yako maana yawezekana mtoto sio wako ( anaweza akwambia one day ukimng'ang'ania sana). Epusha kesi na usumbufu mpe mtoto mradi tu uhakikishe anamlea vizuri. ILA matumizi usitume maana kaamua mwenyewe. Usikubali watumie kigezo cha mtoto. Pole sana.
 
DNA mkuu sina imani nayo pia, nilishajitosa mwaka na nusu sasa kulea, kila mtu anajua ni mtoto wangu nikimkataa leo itakuwa ni jambo la ajabu kidogo.
Pole afadhali kumwacha mapema na hivyo ulivyovigharamia vikawa kama sadaka kuliko kuumbuliwa Mahakamani baada ya DNA kusema si wako! Chungulia sheria ya mtoto ya mwaka 2009!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…