Nitajuaje mchele wa plastic kabla sijaununua???

Nitajuaje mchele wa plastic kabla sijaununua???

girlie

Senior Member
Joined
Jul 14, 2017
Posts
170
Reaction score
180
Habarini,jamani nilinunua kiroba cha mchele sehemu nayoiamini kabisa ila cha kushangaza nao ni plastic vile vile.
Nkidunda yani unadundika,msaada kwa anaejua jinsi ya kuangalia mchele wa plastic kabla sijaununua(ukiwa ndani ya kiroba)..Maana ni tabu kweli kweli.
 
Hakuna mchele wa plastic wewe acha umbwiga!!!
 
mnaosema hakuna mbona sa wali wa sku hizi unakosa harufu??
 
mnaosema hakuna mbona sa wali wa sku hizi unakosa harufu??
Wali wa buku mia mbili unakuwa hauna harufu (kwanza sio kusema hauna harufu sema haunukii).

Kuna marashi yanapuliziwa kwenye wali kama haunukii yanaitwa (Ricepafu).
 
mnaosema hakuna mbona sa wali wa sku hizi unakosa harufu??

Kwasababu wanatumia mbegu za kigeni... zamani mbeya walikuwa wanalima mchele wa kienyeji ndio ulikuwa unaharu sana. Wakulima wanaenda na nyakati. Pia matumizi ya madawa mashambani yanaharibu uhalisia wa mazao.
 
reasonable
 
mnaosema hakuna mbona sa wali wa sku hizi unakosa harufu??
Kukosa harufu inategemea na mambo mengi, storage, aina ya mbegu,umekaa muda gani kabla ya kuuzwa.parkage.preservation n.k
 
Hizi taarifa za mchele feki mbona zimeshakanushwa...

Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
utakuwa una viambata vya tennis.. jaribu kuwasiliana na Serena Williams.... just kidding jibu la msingi hakuna mchele wa Plastic .
 
1, Chukua punje kadhaa za mchele na uziweke kwenye glasi ya maji, mchele wa plastiki utaelea na mchele halisi utazama chini.

2, Tupa punje kadhaa za mchele kwenye moto- ukiona pua yako inanusa plastiki, basi jibu tayari unalo.

3, Tupa punje kadhaa za mchele kwenye mafuta ya moto yanayopogoma (200 c), mchele wa plastki utayeyuka na kubaki chini ya sufuria.

4, Wali wa mchele wa plastiki hauchachi na wala hautaota kuvu (fungus) usipohifadhiwa kwenye jokofu kwa siku kadhaa.

5, Mchele wa plastiki wakati unapikwa unatengeneza "layer" nzito hapo juu.

6, Mchele wa plastiki, hauna ukoko!

Enjoy eating your much deserved real deal WALI!
 
Back
Top Bottom