Nitajuaje kama nimeota au nimeoteshwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitajuaje kama nimeota au nimeoteshwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tatanyengo, Apr 10, 2011.

 1. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la watu kutoa tiba kwa kuwa wameoteshwa. Napenda kufahamu kama nikiota ndoto nitajuaje kama nimeota au nimeoteshwa? Nikiota labda nimemwoa binti wa jirani yangu nikamweleza je atakubali au kuoteshwa kunatokea kuhusiana na tiba tu?
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  huu ni utata....inahitajika wataalamu wa ndoto hapa......mambo yamekuwa mengi sana siku hizi
   
 3. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  1. Nijuavyo mimi, kila ndoto inahusu vitu halisi katika maisha ya mtu - yaani, vitu ambavyo huyo mtu anavipenda, havipendi, amevipata, ameshindwa kuvipata, anavitamani avipate, anavichukia, anaviogopa, hana uwezo navyo n.k...

  2. Ndoto zinahitaji kuzitufuatilia kwa karibu sana ili kujua ujumbe wake.

  3. Baadhi ya ndoto zina 'pattern' fulani - mfano, wanyama (simba, kiboko nk), shimo refu sana, kuzama majini, kuvuka barabara kwa shida sana na kisha kuvuka gari la speed sana kupita, kukabwa shingoni au kuwa katika hali ya hatari na kupiga kelele, kuwaambia rafiki, ndugu wakusubiri wakati unakojoa nk.

  4. Ni kweli unaweza kupata ujumbe kuhusu maisha yako kwa kufuatilia ndoto unazoziota. Kwa hiyo, unaweza kugundua kitu fulani katika maisha kwa kufuatilia ndoto - maana zina ujumbe unaohusu maisha ya kila siku ya mtu.
   
 4. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Tafuta thread ''Ujue ukweli wa Ndoto'' nliweka humu ili jamii wajue. Maana wengi inawapa shida na mashaka kujua. Wanafikiri ni hovyo hovyo tu! Ndoto zimewekewa kanuni kama ilmu zingine. Ukipata humo utaelewa zaidi na waweza kuchangia au kuuliza zaidi.
   
Loading...