Nitaiweka wapi sura yangu

Inawezekana unapenda kutunga stories lkn kabla hujaweka hitimisho ni lazima upangilie vitu viendane. ..kama nyumba mliokuwa mnaishi..ni ghorofa?! Hatujaelewa basi ungeweka maeneo yanayojulikana zaid kuwa na majengo hayo..standard ya maisha je? Ni nzuri, kama ni nzuri kwann mtembee buguruni hlf baba atoke gesti bubu kama pesa IPO!" ? Kasingizia amesafiri . sawa reality ipo wapi kwann hajaenda mbali na hapo..gomz na bugurun si mbali ...na pia kama hamuogopi mama ako anampiga kwann aogope ww kumsema. ...na makosa mengi wakati mwingine rekebisha. Asante
 
Hahahahahaha, Hii Chai au Capacchino? by the way hongera dogo, we una kipaji, ila Setting na mandhari uliyotumia haisadifu kabisa....

Ghorofa Gomz, Bughuruni Guest, atleast mtu anayemiliki Orofa anaweza enda Lodge.....

Chuo labda kama ulikuwa Kampala University, na mtu akizimia anapelekwa hospital sio nyumbani! kwa hiyo baada ya masaa mawili tulitegemea uwe hospitali na sio nyumbani...

Pia umeshindwa kuconsider issue ya foleni, any way utungaji wako mzuri unahitaji kuchange vitu vidogo sana
Cc shigongo
 
Last edited by a moderator:
Nikiwa nipo katika Matembezi ya hapa ma pale na Mama angu Mdogo maeneo ya Buguruni, Ghafla tunamuona Baba akiwa anatoka ktk nyumba moja iliyokuwa na kibao kilichoandikwa Guest House iliyopo maeneo ya Buguruni Malapa akiwa na mwanamke mwengine ambaye si Mama Angu. Sura ya huyo mwanamke ilikuwa ngeni kabisa machoni kwangu.

Nilishtuka..maana Baba alituaga nyumbani akisema anakwenda kikazi Mwanza na atarudi baada ya Wiki moja.

Nina uhakika Baba alituona ila nadhani hofu aliyokuwa nayo kwa wakati ule ilimfanya atupite kimya kama hajatuona.

Ukweli sio yeye tu hata sisi hatukutemea kukutana nae pale.

Nikiwa bado nastahajabu ya Musa . Ghafla Mama mdogo akaniuliza..Umeona upumbavu anaofanya baba ako? Nilibaki kimya, sio kwamba sikuwa na maneno ya kusema,la hasha nilikuwa bado nipo kwenye bumbuazi.

Kitendo hicho kilifanya matembezi yetu ya Jioni yaishie hapo. Kila mtu alikuwa amevurugwa. Tukaenda kituoni pale Buguruni Malapa, Mama mdogo akapanda daladala ya kwenda kwake Msasani na Mimi nikaenda kupanda za kuelekea nyumbani Gongo la Mboto.

Nilifika nyumbani na kumkuta mama sebureni akimnyonyesha mdogo wetu wa mwisho. Nilishindwa kumuangalia usoni. Nilimsalimia na baada ya salamu nikapandisha ngazi kwenda chumbani kwangu.

Moyo wangu ulibeba mzigo mzito sana. Nilijiuliza maswali mengi, nilijiuliza nimwambie mama au nisimwambie?

Nilijua fika mama ataumia sana. Nilijua watagombana sana na baba. Moyoni nikasema sitaki kujua mama ataumia kwa kiasi gani lakini ni lazima nimwambie, siwezi kumsaliti mama angu.

Nikatoka chumbani na kuanza kuelekea sebureni,nikiwa kwenye ngazi mara simu yangu ya mkononi inaingia ujumbe wa maneno kutoka kwa baba 'Ole wako umwambie mama ako ulichokiona'.

Nilifadhaika. Nilishikwa na hofu ambayo sijawai kuwa nayo katika maisha yangu. Nikasimama pale kwenye ngazi kwa muda kisha nikaamua kurudi chumbani.

Baba yangu namjua vizuri ni mkorofi sana. Akiamuaga kumpiga mama anampigaga kama anapiga mpira.

Nilipowaza hilo nikajikuta naanza kukosa nguvu ya kumwambia mama. Ukweli usiku ule sikupata usingizi hata kidogo.
Hatimae mama sikumwambia nilichokiona.

Baada ya wiki moja

Baba alirudi nyumbani na zawadi mbalimbali kama kawaida ya mtu aliyetoka safari . Maisha yakaendelea.

Wiki moja baadae nikiwa chuoni nilipokea simu kutoka kwa mama ' mwanangu wewe wa kunifanyia hivi mama ako' nikauliza 'nimefanya nn mama' akaendelea 'Kwa taarifa yako mama ako mdogo kanipigia simu kaniambalia kila kitu, wewe kwa ujinga wako unasupport maovu ya baba ako, si ndiyo, unamfichia maovu yake, nilikuweka tumboni miezi tisa mwanangu leo unanisaliti' alipofika hapo akakata simu.

Nilishindwa kujizuia nilianza kulia,nililia sana tena kwa kwikwi na sauti. Kweli nilijiona mjinga sana kwa kushindwa kumwambia mama ukweli,nilijiona msaliti kwake. Nililia kwa uchungu sikuweza tena kuendelea na masomo siku ile.

Baada ya dakika kama 10 nikiwa bado nalia baba nae anapiga simu. Nikafuta machozi, nikameza mate kidogo ili niweze kuongea kwa sauti ya kawaida. Nikapokea simu.

'Wewe mtoto mjinga sana umeamua kumwambia mama ako ujinga wakati nilikwambia usimwambie, mpumbavu sana wewe, kuanzia leo usinijue nisikujue na utajisomesha mwenyewe mshezi wa tabia wewe' kwa sauti ya chini nikamwambia baba 'sio mm niliyemwambia ni ma mdogo' lakini simu ilikuwa imeshakatwa.

Pale nilipokuwa nilidondoka chini,na kuzimia.
......................................................
Nilikuja kuzinduka baada ya masaa mawili nikajikuta nipo nyumbani nikiwa nimezungukwa na watu wengi sana. Nilisikia watu wanalia lakini sikuelewa nini kilikuwa kimetokea.

Et naambiwa Mama amefariki kwa Presha.
*************End**************

Tunaomba sehem ya pili tafadhali
 
Hivi gongo la mboto kuna nyumba ya ghorofa? Manake mie mgeni daslama.
Halafu unazimia chuoni na after two hrs unazindukia nyumbani? Lazma una bodyguards na kahelicopter

teh teh...alisahau bhana,acha arudi pale buguruni malapa apande la kwenda masaki.....
 
Asanteni wote kwa Pole na ushauri mliotoa..nimejifunza vitu vingi sana kupitia comment zenu..Asanten
 
Nikiwa nipo katika Matembezi ya hapa ma pale na Mama angu Mdogo maeneo ya Buguruni, Ghafla tunamuona Baba akiwa anatoka ktk nyumba moja iliyokuwa na kibao kilichoandikwa Guest House iliyopo maeneo ya Buguruni Malapa akiwa na mwanamke mwengine ambaye si Mama Angu. Sura ya huyo mwanamke ilikuwa ngeni kabisa machoni kwangu.

Nilishtuka..maana Baba alituaga nyumbani akisema anakwenda kikazi Mwanza na atarudi baada ya Wiki moja.

Nina uhakika Baba alituona ila nadhani hofu aliyokuwa nayo kwa wakati ule ilimfanya atupite kimya kama hajatuona.

Ukweli sio yeye tu hata sisi hatukutemea kukutana nae pale.

Nikiwa bado nastahajabu ya Musa . Ghafla Mama mdogo akaniuliza..Umeona upumbavu anaofanya baba ako? Nilibaki kimya, sio kwamba sikuwa na maneno ya kusema,la hasha nilikuwa bado nipo kwenye bumbuazi.

Kitendo hicho kilifanya matembezi yetu ya Jioni yaishie hapo. Kila mtu alikuwa amevurugwa. Tukaenda kituoni pale Buguruni Malapa, Mama mdogo akapanda daladala ya kwenda kwake Msasani na Mimi nikaenda kupanda za kuelekea nyumbani Gongo la Mboto.

Nilifika nyumbani na kumkuta mama sebureni akimnyonyesha mdogo wetu wa mwisho. Nilishindwa kumuangalia usoni. Nilimsalimia na baada ya salamu nikapandisha ngazi kwenda chumbani kwangu.

Moyo wangu ulibeba mzigo mzito sana. Nilijiuliza maswali mengi, nilijiuliza nimwambie mama au nisimwambie?

Nilijua fika mama ataumia sana. Nilijua watagombana sana na baba. Moyoni nikasema sitaki kujua mama ataumia kwa kiasi gani lakini ni lazima nimwambie, siwezi kumsaliti mama angu.

Nikatoka chumbani na kuanza kuelekea sebureni,nikiwa kwenye ngazi mara simu yangu ya mkononi inaingia ujumbe wa maneno kutoka kwa baba 'Ole wako umwambie mama ako ulichokiona'.

Nilifadhaika. Nilishikwa na hofu ambayo sijawai kuwa nayo katika maisha yangu. Nikasimama pale kwenye ngazi kwa muda kisha nikaamua kurudi chumbani.

Baba yangu namjua vizuri ni mkorofi sana. Akiamuaga kumpiga mama anampigaga kama anapiga mpira.

Nilipowaza hilo nikajikuta naanza kukosa nguvu ya kumwambia mama. Ukweli usiku ule sikupata usingizi hata kidogo.
Hatimae mama sikumwambia nilichokiona.

Baada ya wiki moja

Baba alirudi nyumbani na zawadi mbalimbali kama kawaida ya mtu aliyetoka safari . Maisha yakaendelea.

Wiki moja baadae nikiwa chuoni nilipokea simu kutoka kwa mama ' mwanangu wewe wa kunifanyia hivi mama ako' nikauliza 'nimefanya nn mama' akaendelea 'Kwa taarifa yako mama ako mdogo kanipigia simu kaniambalia kila kitu, wewe kwa ujinga wako unasupport maovu ya baba ako, si ndiyo, unamfichia maovu yake, nilikuweka tumboni miezi tisa mwanangu leo unanisaliti' alipofika hapo akakata simu.

Nilishindwa kujizuia nilianza kulia,nililia sana tena kwa kwikwi na sauti. Kweli nilijiona mjinga sana kwa kushindwa kumwambia mama ukweli,nilijiona msaliti kwake. Nililia kwa uchungu sikuweza tena kuendelea na masomo siku ile.

Baada ya dakika kama 10 nikiwa bado nalia baba nae anapiga simu. Nikafuta machozi, nikameza mate kidogo ili niweze kuongea kwa sauti ya kawaida. Nikapokea simu.

'Wewe mtoto mjinga sana umeamua kumwambia mama ako ujinga wakati nilikwambia usimwambie, mpumbavu sana wewe, kuanzia leo usinijue nisikujue na utajisomesha mwenyewe mshezi wa tabia wewe' kwa sauti ya chini nikamwambia baba 'sio mm niliyemwambia ni ma mdogo' lakini simu ilikuwa imeshakatwa.

Pale nilipokuwa nilidondoka chini,na kuzimia.
......................................................
Nilikuja kuzinduka baada ya masaa mawili nikajikuta nipo nyumbani nikiwa nimezungukwa na watu wengi sana. Nilisikia watu wanalia lakini sikuelewa nini kilikuwa kimetokea.

Et naambiwa Mama amefariki kwa Presha.
*************End**************

hii muvi ilichezwa na nani vile? kama sio ray basi kanumba au mtunisi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom