Nitaiweka wapi sura yangu

Nikiwa nipo katika
Matembezi ya hapa ma pale na Mama angu Mdogo maeneo ya Buguruni,
Ghafla tunamuona Baba akiwa anatoka ktk nyumba moja iliyokuwa na
kibao kilichoandikwa Guest House iliyopo maeneo ya Buguruni Malapa
akiwa na mwanamke mwengine ambaye si Mama Angu. Sura ya huyo mwanamke
ilikuwa ngeni kabisa machoni kwangu.

Nilishtuka..maana Baba alituaga nyumbani akisema anakwenda kikazi Mwanza
na atarudi baada ya Wiki moja.

Nina uhakika Baba alituona ila nadhani hofu aliyokuwa nayo kwa wakati
ule ilimfanya atupite kimya kama hajatuona.

Ukweli sio yeye tu hata sisi hatukutemea kukutana nae pale.

Nikiwa bado nastahajabu ya Musa . Ghafla Mama mdogo akaniuliza..Umeona
upumbavu anaofanya baba ako? Nilibaki kimya, sio kwamba sikuwa na maneno
ya kusema,la hasha nilikuwa bado nipo kwenye bumbuazi.

Kitendo hicho kilifanya matembezi yetu ya Jioni yaishie hapo. Kila mtu
alikuwa amevurugwa. Tukaenda kituoni pale Buguruni Malapa, Mama mdogo
akapanda daladala ya kwenda kwake Msasani na Mimi nikaenda kupanda za
kuelekea nyumbani Gongo la Mboto.

Nilifika nyumbani na kumkuta mama sebureni akimnyonyesha mdogo wetu wa
mwisho. Nilishindwa kumuangalia usoni. Nilimsalimia na baada ya salamu
nikapandisha ngazi kwenda chumbani kwangu.

Moyo wangu ulibeba mzigo mzito sana. Nilijiuliza maswali mengi,
nilijiuliza nimwambie mama au nisimwambie?

Nilijua fika mama ataumia sana. Nilijua watagombana sana na baba. Moyoni
nikasema sitaki kujua mama ataumia kwa kiasi gani lakini ni lazima
nimwambie, siwezi kumsaliti mama angu.

Nikatoka chumbani na kuanza kuelekea sebureni,nikiwa kwenye ngazi mara
simu yangu ya mkononi inaingia ujumbe wa maneno kutoka kwa baba 'Ole
wako umwambie mama ako ulichokiona'.

Nilifadhaika. Nilishikwa na hofu ambayo sijawai kuwa nayo katika maisha
yangu. Nikasimama pale kwenye ngazi kwa muda kisha nikaamua kurudi
chumbani.

Baba yangu namjua vizuri ni mkorofi sana. Akiamuaga kumpiga mama
anampigaga kama anapiga mpira.

Nilipowaza hilo nikajikuta naanza kukosa nguvu ya kumwambia mama. Ukweli
usiku ule sikupata usingizi hata kidogo.
Hatimae mama sikumwambia nilichokiona.

Baada ya wiki moja

Baba alirudi nyumbani na zawadi mbalimbali kama kawaida ya mtu aliyetoka
safari . Maisha yakaendelea......

Wiki moja baadae nikiwa chuoni nilipokea simu kutoka kwa mama ' mwanangu
wewe wa kunifanyia hivi mama ako' nikauliza 'nimefanya nn mama'
akaendelea 'Kwa taarifa yako mama ako mdogo kanipigia simu kaniambalia
kila kitu, wewe kwa ujinga wako unasupport maovu ya baba ako, si ndiyo,
unamfichia maovu yake, nilikuweka tumboni miezi tisa mwanangu leo
unanisaliti' alipofika hapo akakata simu.

Nilishindwa kujizuia nilianza kulia,nililia sana tena kwa kwikwi na
sauti. Kweli nilijiona mjinga sana kwa kushindwa kumwambia mama
ukweli,nilijiona msaliti kwake. Nililia kwa uchungu sikuweza tena
kuendelea na masomo siku ile.

Baada ya dakika kama 10 nikiwa bado nalia baba nae anapiga simu.
Nikafuta machozi, nikameza mate kidogo ili niweze kuongea kwa sauti ya
kawaida. Nikapokea simu...

'Wewe mtoto mjinga sana umeamua kumwambia mama ako ujinga wakati
nilikwambia usimwambie, mpumbavu sana wewe, kuanzia leo usinijue
nisikujue na utajisomesha mwenyewe mshezi wa tabia wewe' kwa sauti ya
chini nikamwambia baba 'sio mm niliyemwambia ni ma mdogo' lakini simu
ilikuwa imeshakatwa.

Pale nilipokuwa nilidondoka chini,na kuzimia.
......................................................
Nilikuja kuzinduka baada ya masaa mawili nikajikuta nipo nyumbani
nikiwa nimezungukwa na watu wengi sana. Nilisikia watu wanalia lakini
sikuelewa nini kilikuwa kimetokea.

Et naambiwa Mama amefariki kwa Presha.
*************End**************

mama yako mdogo kielehele sana unajua matoke ya kitu icho lakin hakujiongeza kama mtu mzima? si kila jambo utasema.pole
 
Chai hii, tena chai kavu isiyo na vitafunwa

Hadithi hii haina tofauti na zile hadithi za miaka ile "MAMA MDOGO NAYE ANATAKA" la gazeti la sani nk
 
Mbona rahisi hivyo hiyo sura iweke mfukoni mwako, simple like that
 
Hivi gongo la mboto kuna nyumba ya ghorofa? Manake mie mgeni daslama.
Halafu unazimia chuoni na after two hrs unazindukia nyumbani? Lazma una bodyguards na kahelicopter

Huwenda kuingia na kutoka chumbani kuna vile vingazi, sio lazima iwe ghorofa. Huwenda anasoma Kampala internationaleee University
 
Nyumba yenu kumbe ya ghorofa!!sasa mbona mzee anaenda gueat bubu buguruni?????????

What a good question!

+Kwa kweli kama ingekuwa kweli usingeiandika hapa kirahisi hivyo, hivi unaujua uchungu wa mama yako kufariki huku anakulaumu? NI kama laana, its not that simple
 
kwaiyo sasa kilichomuua mama ni kwa sababu wewe haujamwambia au ni kwavile baba yako alivyomsaliti?
 
Nipe ruhsa nifanye muendelezo wa hii hadithi, na jinsi maisha yalivyo kubadilikia baada ya mama kufariki, pia baba alivyo kuchukulia baada ya kuona umetoa siri ilopelekea kumpoteza mkewe, bila kusahau maisha yalivyokua magumu chuoni hadi una maliza na kupata mafanikio makubwa kimaisha na leo kutupa simulizi ya mfano
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom