Nitaishije na mwanamke muongo?

CUBICBOY

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
306
223
Habarini wakuu,

Huyu mwanamke ninayeishi nae ni muongo wa kupindukia, nimejaribu kumfatilia sana nyendo zake nimegundua mambo mengi amekuwa akinidanganya sana hasa kwenye suala la pesa, amekuwa nimekuwa ni mtu wa kutunga mambo sana ili anidanganye.

Nifanyeje wakuu niweze kuishi na huyu mwanamke
 
Habarini wakuu , huyu mwanamke ninayeishi nae ni muongo Wa kupindukia, nimejaribu kumfatilia Sana nyendo zake nimegundua mambo mengi amekuwa akinidanganya Sana hasa kwenye suala la pesa, amekuwa nimekuwa ni mtu Wa kutunga mambo sana ili anidanganye nifanyeje wakuu niweze kuishi na huyu mwanamke
Weka wazi ni mke au ni mpenzi tu kama ni mpenzi tu achana nae
 
Kwa kuwa umemjua ni muongo tena "specifically" kwenye pesa na wewe hutaki kuongopewa! Nadhani umekuwa aware nae kwa hiyo ushauri wangu jitahidi kuwa unamhoji sana kuliko ulivyofanya mwanzo. Faida yako ni kwamba umemjua kwa hiyo kujua tatizo lilipo inakurahisishia utatuzi wake!
Wakati mwingine mnyime kabisa kama unaona jambo analoongea halina mashiko pia ikiwezekana mweleze kabisa kwamba umegundua sio mkweli. Ukweli humweka mtu huru.

Tahadhari; Jiandae kupokea mabadiliko ambayo huwenda hayata kufurahisha mara tu utakapoanza kuhoji na kumuwekea ngumu. Tambua ameshajenga mazoea hivyo hatua utakayochukuwa ni kumbadilisha tabia hiyo jambo ambalo lazima litakuwa na matokeo either hasi kwa 90% au matokeo chanya 10%

Kila la kheri mkuu.
 
Huyu ni mke ila mambo mengi amekuwa akinidanganya Sana

Matumizi ya fedha au kiwango anachopata au? wengi eneo hilo ni waongo sana maana wana tamaa na fedha na kuvutwa kuhudumia familia zao, usipoweza kuwapa uhuru wote - 100% - NI WAONGO...
 
Mambo mengine ujinga mtupu, kwenye ndoa kila mtu Ana mapungufu yake, huenda amegundua Unapenda kudanganywa!!

Solution, acha kufuatilia petty things, kama ni pesa ya sokoni Toa inayotosha au ambayo hataakiiiba inakua poa tu
 
Ishi nae kwa akili mbona na nyie hamtuambiagi vyanzo vyenu vyote vya Pesa....
 
Wewe mpe pesa tu ya kutosha as long as ni mkeo labda huko kwao ndio wanamtegemea nayeye anashindwa kukwambia ukweli
 
Kwa kuwa umemjua ni muongo tena "specifically" kwenye pesa na wewe hutaki kuongopewa! Nadhani umekuwa aware nae kwa hiyo ushauri wangu jitahidi kuwa unamhoji sana kuliko ulivyofanya mwanzo. Faida yako ni kwamba umemjua kwa hiyo kujua tatizo lilipo inakurahisishia utatuzi wake!
Wakati mwingine mnyime kabisa kama unaona jambo analoongea halina mashiko pia ikiwezekana mweleze kabisa kwamba umegundua sio mkweli. Ukweli humweka mtu huru.

Tahadhari; Jiandae kupokea mabadiliko ambayo huwenda hayata kufurahisha mara tu utakapoanza kuhoji na kumuwekea ngumu. Tambua ameshajenga mazoea hivyo hatua utakayochukuwa ni kumbadilisha tabia hiyo jambo ambalo lazima litakuwa na matokeo either hasi kwa 90% au matokeo chanya 10%

Kila la kheri mkuu.
asante kwa ushauri wako
 
Hili limekuwa tatizo kubwa mnoo kwenye mahusiano hasa yale yanayohusisha mmoja wapo wa nyumbani. Mama/baba wa nyumbani. Usipoangalia ndoa itakushinda
 
Habarini wakuu,

Huyu mwanamke ninayeishi nae ni muongo wa kupindukia, nimejaribu kumfatilia sana nyendo zake nimegundua mambo mengi amekuwa akinidanganya sana hasa kwenye suala la pesa, amekuwa nimekuwa ni mtu wa kutunga mambo sana ili anidanganye.

Nifanyeje wakuu niweze kuishi na huyu mwanamke
There is only solution for mtu mwongo, katika uchunguzi wako .. pata ushahidi red handed...then ukisha jua baadhi ya shahidi. Mkalishe chini muonyeshe. Akipinga badala ya kuomba msamaha... mteme dump her.

Mwanamke ambae hakubali makosa , na kuomba msamaha. Kuna vingi amekuficha.

Kama atakuomba msamaha na kukuri. Mpe muda, lakini usimuamini, endelea kumchunguza.mwekee mitego ya kifedha...
Asipo jirekebisha dump her..
 
Back
Top Bottom