Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,351
- 23,758
Ndugu zangu Watanzania ,
Muda wowote nitaijibu barua ya kujiuzulu iliyoandikwa na polepole aliyekuwa Balozi wa Tanzania Nchini Cuba. Nitazijibu hoja zote alizoziandika katika barua yake.
Nitajibu kwa kufafanua kwa undani kabisa na kuonyesha Unafiki wake wa Kiwango cha juu alichoonyesha kupitia barua yake inayoonyesha amejawa na chuki binafsi pamoja na ubaguzi kwa misingi ya ukabila ,ukanda na jinsia.
Ikumbukwe ya kuwa wakati Mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa iliyopo kisheria na kikatiba inapigwa marufuku Humphrey Polepole alikuwa ni kiongozi ndani ya chama nawala hakuongea chochote kile, wakati wagombea waliounga juhudi kutoka CHADEMA wanapitishwa bila mchujo wala ushindani wa aina yoyote ile na kupewa ubunge wa Bwelele polepole alikuwa kiongozi na hakuongea chochote kile. Je hiyo ilikuwa ndio haki anayoisema?
Wakati wagombea ndani ya CCM waliopata kura nyingi sana mwaka 2020 wanakatwa na kuchukuliwa wale waliopata kura za namba za viatu polepole alikuwa ni kiongozi na aliona sawa tu na alikaa kimya kabisa. Je hiyo ndio haki? Hiyo ndio ilikuwa demokrasia? Wakati wa awamu ya tano wakati akina Mzee Yusuphu Makamba ,Mzee Kinana ,Marehemu Bernard Membe wanadhalilishwa nani aliwatetea? Je polepole aliinua mdomo wake kuzungumza chochote?
Wakati Watu wanaokotwa kwenye viroba kama mizoga ya Mbwa au Nguruwe ni nini ilikuwa kauli ya polepole je huo ndio ulikuwa ustawi wa Wananchi ? Je amewahi kuhoji juu ya hali hiyo? Amewahi kuzungumza chochote? Wakati haki ya kuchagua na kuchaguliwa ikibakia mikononi kwa watu wachache ni nini ilikuwa kauli ya polepole? Je ndio ilikuwa haki hiyo? Je hakuona uvunjifu huo wa haki za watu?
Wakati vyombo vya habari vinafungiwa na kunyang'anywa lesseni zao ni nini ilikuwa kauli ya polepole? Je amewahi kuinua mdomo wake kuzungumza lolote lile? Wakati wafanyabiashara wanafungiwa akaunti zao ,biashara zao ,kuchotewa pesa zao ni nini ilikuwa kauli ya polepole mdomoni pake? Mmewahi kusikia akizungumza lolote?
Ni nani aliyerejesha uhuru wa habari, mikutano ya vyama vya Siasa, maridhiano ya kitaifa kama siyo Rais Samia? Ni nani aliyewarejesha watanzania uhamishoni kama vile Lissu kama siyo Rais Samia? Ni lini watanzania wamewahi kukimbia nchi yao zaidi ya kipindi ambacho polepole alikuwa kiongozi? Ni nani aliyepinga kodi za maonezi,kunyanyasa wafanyabiashara,kufunga biashara za watu bila utaratibu kama siyo Rais Samia?
Ni wakati gani kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na katiba ya Nchi yetu? Ni wakati gani ambapo Taswira ya Taifa letu ilichafuka vibaya zaidi Kimataifa kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora? Ni nani aliyerejesha Imani ya jumuiya za kimataifa kama siyo Rais Samia? Ni wakati gani katiba ya Nchi ilisiginwa kwa miguu? Je polepole ni kipofu wa akili?
Ni nani aliyepandisha mishahara ya watumishi wa umma, kuwapandisha madaraja na kuwalipa madai yao kama siyo Rais Samia? Ni nani aliyeanza kutoa ajira maelefu kwa maelfu kwa vijana kama siyo Rais Samia? Ni nani aliyevuruga bei ya korosho? Ni nani aliyepandisha mapato ya korosho kufikia Trilioni 1.6? Kama siyo Rais Samia?
Ni nani aliyejenga shule nyingi primary kwa secondary kumpita Rais Samia katika historia ya Taifa letu? Ni nani aliyevutia watalii wengi kuja Nchini kumpita Rais Samia ? Je polepole ni kipofu wa akili na macho mpaka ashindwe kuona haya? Hapana huyu siyo mjinga bali anasumbuliwa na chuki binafsi,ubaguzi kwa misingi ya ukabila na ukanda . Hivi Ndivyo vinavyomtesa yeye binafsi pamoja na wanaomtumia kujaribu kumtikisa Rais Samia na serikali yake. Hata hivyo hawataweza kamwe yeye Binafsi na wale wanaomtumia.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.