Uchaguzi 2020 Nitaichagua tena CCM tarehe 28 Oktoba

Bekiri

Member
Jun 30, 2013
14
63
Nitapiga KURA ya NDIO kuichagua CCM ifikapo tarehe 28 Oktoba 2020.

Nitaichagua kwa sababu sababu zifuatazo;

1. Ndicho Chama pekee kinacholinga na kutetea Muungano wa Tangangika na Zanzibar.

2. Ndicho chama pekee ambacho Wagombea wake wanapinga hadharani ushoga.

3. Ndicho chama pekee kimeimarisha misingi ya Uchumi wa Kitaifa.

4. Ndicho chama pekee ambaco kinaimarisha huduma za kijamii.

5. Ndicho Chama pekee ambacho kinaimarisha misingi ya maadili na uongozi bora.

6. Ndicho Chama pekee kinachodumisha TUNU za Taifa.

7. Ndicho Chama pekee kinaimarisha demokrasia nchini.

8. Ndicho chama pekee kinachoendeleza harakati za mapinduzi dhidi ya unyonge.

9. Ndicho Chama pekee kinachopinga uonevu na udhalimu duniani.

10. Ndicho chama pekee kinachowakilisha Wakulima na Wafanyakazi.

CCM NI SAUTI YA WATU, NITAICHAGUA TENA!!
#MitanoTena.
MenukaJr.
 
Ndiyo chama pekee kilichowatelekeza watumishi wa umma kwa miaka 5
 
Mabadiliko hayawezi kusubiri kila mtu ajitambue/awe tayari kwa mabadiliko.

Ni kama ambavyo ujio wa Masiha hauwezi subiri kila mtu awe tayari kumpokea ikiwa ni pamoja na kutubu dhambi zetu.
 
WATANZANIA MIMI KIJANA WENU NINAWAOMBA MSIFANYE MAKOSA 2020 YA KUIPA KURA CCM.

Tutaumizwa sana, Tutalia sana ,Tutatekwa sana, Tutauwawa sana, TutapIgwa lisasi sana.

Kwa KIFUPI Itakuwa kipindi cha MATESO SANA.
NAOMBA MSIMPE KURA MAGUFULI ANA KISASI NA MAKUNDI YOOTE AKISHINDA ANAMPANGO WA KUJIONGEZEA MIAKA KUWA RAIS ASIYE NA UKOMO.
 
unapoteza muda wako. Magufuli hawezi kushinda labda ashinde njaa
Oct 28, uje urudie hii kauli hapa.Ni ma punguani pekee wanaojua kuwa Lissu anaweza shinda. Chama cha Mbowe, baada ya kupoteza ukawa 2015 pamoja na kuzungusha mikono na miguu sahauni Urais tena. Jipangeni upya.
 
Kuchagua CCM Ni Umechagua kupingana na Mungu.
CCM ya Sasa Ni Genge Kama magenge mengine ya kihalifu.
Ha ha ha kama ccm ni genge la uhalifu, chama cha Mbowe kitakuwa nini?.Mnafanya siasa kichaka chenu, Oct 28 twakitia moto. Hakuna genge hatari kwa taifa hili kama hii saccos ya huyu mangi..
 
SABABU 31 ZA KUMKATAA MAGUFULI 28 OKTOBA 2020:

1. Hajatoa ajira miaka 5
2. Hajaongeza mishahara kwa miaka 5
3. Ameongeza makato HESLB toka 8% to 15%
4. Amefukuza wafanyakazi na hajawapa hata senti tano kisa vyeti feki
5. Kaondoa fao la kujitoa NSSF
6. Kaondoa wanunuzi binafsi wa kahawa waliokuwa wanatoa bei nzuri
7. Karudisha gharama za matibabu kwa watoto na wajawazito
8. Anatoza maiti kodi kuzitoa mochwari
9. Kavunja katiba ya nchi kuzuia wapinzani kufanya mikutano halali ya siasa
10. Katunga sheria kandamizi kukomoa watu
11. Kabambikia kesi watu kwa visasi na chuki
12. Kafilisi wafanyabiashara kwa chuki binafsi
13. Kathibiti mashirika ya kutetea haki za binadamu
14. Kadhibiti na kutisha vyombo vya habari na kuviamrisha vimtangaze yeye tu na chama chake
15. Kavuruga sana mahusiano ya kimataifa
16. Kavuruga demokrasia na anataka wananchi waishi kama mifugo yake kufuata analotaka
17. Kazima bunge live na kulitumia bunge kama muhuri kufanya mambo yake
18. Mahakama imebinywa na imekuwa siyo huru tena
19. Kawadhibiti viongozi wa dini wanaomkosoa na kumwambia ukweli
20. Kanunua ndege bila kufuata sheria ya PPRA
21. Watu wengi wameuwawa na kupotea na kutekwa
22.Amelea na kulinda kikosi kazi cha "watu wasiojulikana"
23. Amepandikiza hofu,ukatili na dhuluma kama nyenzoza siasa mpya za Tanzania na utu umetoweka
24. Kakivuruga chama chake na kukimega vipande vipande
25. Kajenga uwanja wa ndege kwao bila ya approval ya bunge wala cabinet
26. Alisema tutaishi kama MASHETANI.. Kwa madai kuwa tulikuwa tunaishi kama Malaika. Hakika amelitimiza hilo.
27. Kuwa na kundi la watu wasiojulikana awamu hii ya tano na polisi hawajawai

28. Ni mwongo kupindukia – mwaka 2015 wakati anaomba kura aliongopa mengi km kumpa kila mwalimu kompyuta, kukipa kila Kijiji milioni 50 nk. Leo hii tunaingia uchaguzi mwingine, hajatimiza hayo na anaahidi mapya bila aibu.

29. Kudhalilisha akina mama kwenye majukwaa yake ya kisiasa

30. Kula rambirambi za wahanga wa majanga. Rais anayekula rambirambi zilizotolewa na watu mbalimbali ikiwemo nchi rafiki hatufai Watanzania.

31. Kuwakana Watanzania waliopata majanga km Wanakagera wakati wa tetemeko la ardhi.



 
Iwe kwa mwanga au giza, mvua au jua Magufuli mitano mingine. Hatuwezi kurudisha uchumi wetu mikononi mwa mabepari.
 

Mkuu umepotelea wapi? michango yako muhimu kulekea kupiga kura 28/10.
 
Ccm ni chama mama wa demokrasia afrika nzima.
-Chama cha watanzania, chenye kupinga Rushwa, ufisadi, uonevu na ukoloni.
-Chama chenye kulinda na kutetea tunu za taifa.
-Chama chenye kufua viongozi kwa ajili ya sasa na baadae.
-Chama chenye kusambaza maendeleo kwa nchi nzima, sio kubagua Kutokana na kabila, kanda, dini etc.
-Chama chenye nidhamu, kwa wagombea, rasilimali za chama.
Chama cha Mbowe:
-Rushwa ndio nyumbani, hasa ile ya vitu maalum na uongozi.
-Chama wakala wa beberu, wao wanaona liwalo na liwe kisa wao kwao Ubelgiji.
-Chama chenye kuokota viongozi, wao kiongozi mkuu ni mwenyekiti yeye ndio kila kitu. Amri zake ni sheria hutaki ondoka cc Mwigamba, mkumbo na msaliti Zitto.
-Chama kinachotaka kugawa watanzania kwa kanda. Viongozi wengi wa juu, wa hilo genge wanatoka kanda flani hivi.
-Chama kisicho nidhamu ya pesa, uongozi, staha. Pesa zote ni za Mbowe, mwanachama ni marufuku kuhoji. Wengi wa viongozi wa juu wa hilo genge, ni wasagaji na mashoga. Wengi hasa wadada wanalazimika kutoa utu wao kwa Mwenyekiti ili tu wapate nafasi. Nafasi kwa wanawake chamani ni almost zero.
Mgombea kutoka chama cha Mbowe, hatufai kama taifa. Watanzania tuwaogope kama ukoma.
 
Umeandika vema. Ni taahira atakayekupinga.
 
Hapa Zito amekula za uso.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…