Mkuu sidhani kama umakini wa chadema unaweza kudondokea kwenye ku-meltdown hoja ya uraisi kwa aina hiyo! Kwa mwenye akili timamu ushauri wa mzee mtei ndio wa kufuatwa kwa sasa, haya mengine ni watu kutaka kutafuta tu press coverage ili kusafisha nyota, watu wanacho kihitaji kwa sasa sio lundo la majina ya wagombea urais au fulani ana m-support nani, mwanachadema/wana chadema wanatakiwa kuunganisha nguvu ya pamoja kueneza elimu ya uraia ili watu wa vijijini wazidi kuamka na kumrahisishia mgombea atakaye chaguliwa kwa utaratibu (sio anaye jitangaza kwenye media)urahisi wa kupata kura nyingi.
Ukiipima support ya Kisandu ina ka ukame wa maono ndani yake, yeye aligombea ubunge kupitia chadema jimbo la Lushoto, lakini pamoja na Shekifu kuwa hakuwa chaguo
mujarabu kwa wana lushoto bado aliendelea kupata na yeye kushika nafasi ya pili, alichotakiwa kukifanya ni kuangalia changamoto alizo kumbana nazo ili ziwe mbadala kwa raisi ajaye, na moja ya changamoto hata yeye anaijua kuwa ni kuto kufahamika vizuri kwa watu wa vijijini hivyo akaonekana kama mgeni wa kuja na kura zikisha pigwa atatokomea.
Tunahitaji vuguvugu la mabadiliko zaidi ya kujitangaza na ku-support watu kuwa wana faa au hawafai kuwa maraisi! Wapo walio uhemea uraisi kwa mbio za farasi hata kuitwa machaguo ya Mungu. Je wanacho kifanya ndio mapenzi ya Mungu yanayo mgusa kina mwana dongo la Tanzania?!
Uraisi sio makalio kuwa kila mtu anayo au anaweza kuyaona ya mwingine.