Omokora Nyangi
Member
- Apr 5, 2012
- 58
- 66
Ssi watu wa Mara, tuna hulka ya kuwa na majina ya "Ujana au uzee", Jina hili Omokora Nyangi ni jina langu halisi (verified) linalo nitambulisha mbele ya wana jamii forum na hasa mbele ya umma wa wapiga kura wa serengeti. Wakati ukitimu, utanisikia nikijitambulisha kwa jina hili adhimu. Kadhalika, kwa kuwa Jamvi hili lapaswa kuwa la watu makini, naamini kupitia umakini huo nitaanza kupimwa uadilifu ktk maandishi na matamshi yangu kabla ya kuiona sura yangu! Oba, naamini nimejitahidi kujibu suala lako.Ni vyema ukajipambanua humu jukwaani kwa jina lako halisi (verified name), nia haitangazwi kwa majina bandia. Wengine sisi ni wakazi wa Serengeti tuwekee humu majina yako kwani itakuwa na faida kwako, twaweza kukusapoti humu jamvini pia kwa watu wanaokufahamu wanaweza kutoa taarifa juu ya uadilifu wako na jinsi wanavyokufahamu.😛eace:
omokora nyangi, aman'gana , nahisi u mzima, hongera kwa uamuzi wako, ila inatakiwa kupata ushauri toka kwa watu kama MOSENA JOHN NYAMBABE juu ya kushindwa kwake kuchukua jimbo licha ya kampeni alizokuwa anafanya, kujitahidi kupambana na sumu ya ukanda, yaani NGOREME, ISSENYE na ROGORO, pia unahitaji kuonana na mtu anaitwa MUHOCHI huyu anajua vema siasa za SERENGETI pia unahitaji kuunga mawazo na kamand amwita maranya kwani ana ufahamu mkubwa na serengeti, vilevile uwe na mtandao mzuri wa mawakala kwani watuj wa kule kuuza ushindi hata kwa kemoro inawezekana, mwisho unatakiwa kuwa na wagombea udiwani wanaokubalika kila kata
Mmh!!isije ikawa huyu ni nyakarungu maana si ni mtu wa kule?kama umetangaza nia mapema hivi na chama kikikupitisha sawa ila msije fanya yale mambo ya masalia maana siku hizi njaa nyingi sana.....Mkuu Omokora Nyangi all the best; ni haki yako kikatiba ila mambo yakienda ndivyo sivyo sio tena unakuwa wa kwanza kuporomosha matusi kama walivyo wajinga wachache wasiojua maana ya demokrasia.
CC: Mwita Maranya
Ssi watu wa Mara, tuna hulka ya kuwa na majina ya "Ujana au uzee", Jina hili Omokora Nyangi ni jina langu halisi (verified) linalo nitambulisha mbele ya wana jamii forum na hasa mbele ya umma wa wapiga kura wa serengeti. Wakati ukitimu, utanisikia nikijitambulisha kwa jina hili adhimu. Kadhalika, kwa kuwa Jamvi hili lapaswa kuwa la watu makini, naamini kupitia umakini huo nitaanza kupimwa uadilifu ktk maandishi na matamshi yangu kabla ya kuiona sura yangu! Oba, naamini nimejitahidi kujibu suala lako.
Omokora Nyangi :nni bora kuweka jina halisi ili wanaserengeti tuendeleze mapambano binafsi ni Mwana Serengeti na nimesoma Serengeti secondari miaka 18 iliyopita ila hilo jina sijui funguka :nono:Omokora Nyangi nadhani hili litakuwa ni la uzee. Mzee Omokora Nyangi yaani unataka tukupime uadilifu wako kwa maandishi na matamshi yako humu jamvini?. Rudi ujipange, humu hatuangalii mbwembwe za uandishi au ufundi katika kuyaumba maneno. Haya wanayafanya MAGAMBA kwani ndio hodari wa kuwahadaa wananchi kwa maneno matamu matamu.
Wenzako waliotangaza nia humu wameweka majina yao halisi na tumeweza kuwafahamu na kuwauliza maswali kadha wa kadha tukiwa tayari tumeishawafahamu. Kama umeona wakati haujatimu ni kiherehere gani kilichokutuma uje kutangaza nia kwa majina fake?. Narudia kukushauri, weka majina yako halisi humu sisi watu wa SERENGETI tukujue. Mbona Mokoro Rutiginga kijana machachari kutoka kata ya NATTA ameweka jina lake humu kwanini wewe unaendelea kujificha nyuma ya pazia?.😛eace:
SAHIHISHO: Naitwa don-oba.