Nitafanya nini Maana naona giza huko mbeleni hasa mustakabali wa elimu na maisha

slow_learner

Senior Member
Nov 24, 2016
139
110
Natanguliza salamu zangu za mwaka mpya 2017 kwa wana jamii wote.

Mimi ni kijana mtanzania ambaye Nimepata misukosuko katika mchakato mzima wa elimu tangu nikiwa elimu ya msingi.
Nilibahatika kujiunga na elimu ya upili mwaka 2008 pamoja na kuwepo matatizo kadha wa kadha nilifanikiwa kuhitimu elimu yangu ya upili mnano 2011. Japokuwa Nilikuwa na uwezo mzuri darasani sikufanikiwa kujiunga na elimu ya kidato cha tano na sita kutokana na kupata alama za chini yaani daraja la nne alama 28.

Mzazi alinishawishi nirudie mtihani kwa kuwa na Mimi Nilikuwa napenda sana kusoma. Mwaka 2013 nilirudia mtihani na kupata alama nzuri.
Baadaye niliamua kujiunga na mafunzo ya GATCE lakini nilizuiliwa kujisajili kutokana na chuo husika kushindwa kunipatia taarifa mapema. Nilihisi kupoteza Kila kitu. Mbaya zaidi kilikuwa ni chuo cha binafsi. Muda si mrefu nilibahatika kujisajili kufanya mtihani wa kidato cha sita wakati nikiwa sijasoma kitu chochote. Namshukuru mungu kwa kuwa nilianza kusoma kwa juhudi zote katika kipindi cha miezi nane niliweza kuzoea na nilipofanya mtihani nilipata ufaulu wa daraja la Kwanza.

Nilifanikiwa pia kujiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam. Nikitafuta B.A.ED.
Tatizo langu ni kuwa sijapata mkopo na nime'appeal. Sijajua majibu yatakuwaje. Mtu aliyekuwa ananisaidia kulipa gharama kasema kuwa gharama ni kubwa sana na hivyo hatoweza kumudu gharama. Kiukweli ni yeye ndiye aliyeniwezesha hata kufanya malipo ya awali ndipo nikafanya usajili n's gharama zingine za maisha.

Yaani alinipatia mahitaji mwisho wake mwezi wa pili.
Baada ya likizo sijui itakuwaje nikikosa huo mkopo.
Je, nirudi nyumbani nikatafute kazi za kufanya?
Au nifanye kupostpone masomo mpaka mwaka 2019?
Au nifanye biashara? Je. Mtaji nitatoa wapi?
Au nifanye nini? Yaani hapa hata sielewi nifanye nini! Ninaishi na mama yangu ambaye ni mjane na muda mwingi husumbuliwa na matatizo ya kiafya.
Kumbuka hivi sasa nina miaka 25 sijaoa na wala sina assets yoyote ile.

Jamani naombeni mnisaidie kunifungua kifikra nifanye nini. Maana sijawahi kuishi maisha ya mitaani.
 
daaa ,ndugu yangu usipofanikiwa kupata mkopo mwaka huu na ukikosa msaada kabsa ahirisha mwaka alafu aplai tena mkopo mwakan unaweza kupata.
 
Baada ya likizo sijuwi itakuwaje nikikosa huo mkopo.
Je, nirudi nyumbani nikatafute kazi za kufanya?
Au nifanye kupostpone masomo mpaka mwaka 2019?
Au nifanye biashara? Je. Mtaji nitatoa wapi?
Au nifanye nini? Yaani hapa hata sielewi nifanye nini! Ninaishi na mama yangu ambaye ni mjane na muda mwingi husumbuliwa na matatizo ya kiafya.
Kumbuka hivi sasa nina miaka 25 sijaoa na wala sina assets yoyote ile.

Jamani naombeni mnisaidiea kunifungua kifikra nifanye nini. Maana sijawahi kuishi maisha ya mitaani.
Uyo anaekusaidia mueleze akupe mtaji,wakati tayali ushakua nawazo la biashara gani ufanye
daaa ,ndugu yangu usipofanikiwa kupata mkopo mwaka huu na ukikosa msaada kabsa ahirisha mwaka alafu aplai tena mkopo mwakan unaweza kupata.
 
Uyo anaekusaidia mueleze akupe mtaji,wakati tayali ushakua nawazo la biashara gani ufanye
Ametumia pesa nyingi sana mpaka hapa nilipo. Kumbuka ni mtu aliyejitolea tu wala siyo ndugu yangu. Kanisomesha taasisi za binafsi ila kwa sasa uchumi wake umeyumba hivyo hatoweza kutoa chochote.
Sijuwi kwa hili atakavyolipokea
 
Usikate tamaa
 
Back
Top Bottom