Mzee mmoja alipanda kwenye daladala lilikuwa limejaa, hivyo akalazimika kusima. Wakati safari ikiendelea, akagundua kuwa amechomolewa fedha zake. Hali ilikuwa hivi:
MZEE: Jamani alienichukulia hela yangu anirudishie tu mwenyewe, nisije fanya kama nilichofanya Mwaka 1961.
Baada ya kuhisi huenda angedhurika jamaa aliyechukua zile fedha akaogopa na kumrudishia, kasha akamuuliza jamaa: kwani ulifanyaje Mwaka huo?
MZEE: We acha tu mjukuu wangu nilitembea kwa miguu kuto Mbagala hadi Tegeta.