Styvo254
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 246
- 226
Vipi WanaJamii
Kwa mda mfupi nliliokua hapa nimeona wengi wakilalamika kuhusu gari hizi za Nissan. Kweli kila mtu ana haki na uhuru wa maoni/mawazo yake ni muhimu kufanya maamuzi na kua na mawazo ya ukweli na kamilifu. Kwa hili, nimeona nianzishe uzi huu ambao utakua ni wa kuhoji na kuangalia kwa kina gari hili la Nissan.
Gari hili liko kwenye toleo la tatu sasa na hii ni kudhihirisha umaarufu wake na kupendwa kwake ulimwenguni mzima. Lisingalikua zuri na bora, lisingalinunuliwa kwa wingi na kwingi hivyo. Wala sidhanii mJapan/Nissan angaliendelea kulitengeneza na kuliboresha kwa miaka karibia ishirini. Hapa hapa nchini kuna wengi wanaapa kwa hili gari na sio matani, hata uumpe gari aina nyingine na hela juu hakuskii!
Basi shida iko wapi?
Gari hili ni la kisasa na lina tumia mifumo na teknolojia ya hali ya juu. Magari haya yanauzwa soko tofauti na lazima yazingatie sheria na kanuni za nchi au maeneo husika. Mambo haya mawili ni ya muhimu sana katika kuielewa gari hili.
Kwa minajili ya usalama, kuboresha na kutofautisha chombo chao, Nissan wametumia teknolojia za kisasa kw. mf. X-Trail ya diesel yawezakua na mfumo wa DPF, huu ni wa kumaliza gesi sumu kwenye moshi wa exhaust.
Engine hii utumia oili na ratba tofauti na ya kawaida kwa matunzo yake. Gari hili laja na transmission/gearbox ya manual(sawa kabisa) na automatic aina tatu; planetary, CVT na eCVT(hapo basi baharia). Bila kusisitiza zaidi mwaona hawa ni wanyama aina tatu labda wafanane kwa kua wanafungwa kwenye engine, shaft zatoka mle na hutumia mafuta ila sio sawa.
Gari la DPF usijaribu bidhaa na mambo ya uswazi.