Nissan X-Trail

Leo pia gari limerudi limewasha MIL. Baada ya kuisoma code tumepata ni zile zile za jana.
Tukiangalia exhaust ya gari, ina kosa CAT converter na kuleta shida mbili, kwanza zile gesi zinapita kwa kazi kubwa sana na kwa hivyo Oxygen sensor zinaashindwa kusahihisha air/fuel mixture vizuri, pili, bila kuchuja au convert zile gesi, mfumo unapata taarifa zisizoeleweka kuhusu jiko/combustion.
Baada ya kubadilisha oili, gari ilitulia kiasi. Wacha tuitaftie CAT converter yake halafu twende kutoka hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usihangaike na kutaguta CAT kwanza ni garama kubwa but huo ugonjwa una solution kama 3 hivi ninazo zifaham mimi..kuzidelet hizo oxygen senaor kwenye ECM control box, kuzifanyia utundu kwa kuidanganya control box hapo pia kuna njia mbili. Na mwisho kufunga kimodulatot..

Njia rahisi na yenye garama ndogo ni hiyo ya pili.kama utahitaji tuwasiliane mkuu nitakuelekeza jinsi ya kufanya..buree kabisaaaa
 
kuna ndugu yangu mmoja aliniambia kuwa aliambiwa na fundi magari mmoja kuwa magari YOTE ni pasua kichwa! ukijumlisha na jinsi wadau wanvyo yananga humu nilishaanza kuamini pia...japo nilikuwa nakilia timing ka Nissan Note ila wana jamvi wakanikata stimu kabisa!
 
Hapa uchambuzi wa kitaharam hadi raha issue ni kuwa kwa mazingira ya vijini hamna mafundi wa uhakika wataharam nauliza vipi engine za 2AZ vvt-i ufanisi wake na service zake pia zikoje? Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa uchambuzi wa kitaharam hadi raha issue ni kuwa kwa mazingira ya vijini hamna mafundi wa uhakika wataharam nauliza vipi engine za 2AZ vvt-i ufanisi wake na service zake pia zikoje? Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
Ingawa huu ni uzi wa Nissan Xtrail, Toyota 2AZ VVTI IPO vizuri ila mafuta (oil) unayoitumia pale lazima iwe synthetic na ufaatilie vizuri change-interval/ubadilishe kw mda maalum

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo pia gari limerudi limewasha MIL. Baada ya kuisoma code tumepata ni zile zile za jana.
Tukiangalia exhaust ya gari, ina kosa CAT converter na kuleta shida mbili, kwanza zile gesi zinapita kwa kasi kubwa sana na kwa hivyo Oxygen sensor zinaashindwa kusahihisha air/fuel mixture vizuri, pili, bila kuchuja au convert zile gesi, mfumo unapata taarifa zisizoeleweka kuhusu jiko/combustion.
Baada ya kubadilisha oili, gari ilitulia kiasi. Wacha tuitaftie CAT converter yake halafu twende kutoka hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hbr za mida WanaJF
Baada ya kuangaika hapa na pale, catalyctic converter ya Xtrail QR20DE tumeipata na kuifunga kwenye gari. Mngurumo na idle speed zilibadilika pale pale. Zile sensor zake (O2) pia zilionekana zikifanya kazi yake bila tatizo. Baada ya mda kidogo hata ile harufu kali ya mafuta kwenye exhaust iliisha na gari likawa tulivu.
La msingi ninalotarajia ni matumizi yake ya petroli kupungua. Hii inatokàna na utendakazi wa mifumo na sehemu husika za engine kurudi sawa.
Matunzo na marekebisho ya gari sio kama uganga, manual na maelekezo yapo.
 
Mkuu hebu tujuze hicho kifaa kimepatikana kwa bei gani na kufa kwake kulisababishwa na nini? Nategemea kununua hii gari miezi michache ijayo ndio maana nauliza.
 
Mkuu hebu tujuze hicho kifaa kimepatikana kwa bei gani na kufa kwake kulisababishwa na nini? Nategemea kununua hii gari miezi michache ijayo ndio maana nauliza.
Asante kwa swali zuri sana Bw. Galindas. CAT converter ni kifaa kinacho nasa gesi na chembechembe haribifu kwa mazingira na kuziangamiza kw kuzichoma na kuzichanganya zikawa safi(harmless). Mle ndani kuna madini yanayosaidia katika shughuli hii, na pia muundo wake ni maalum kunasa chembechembe zile na kuzipika kwa joto la juu.
Tukilinganisha mfumo huu na kichujio, kwa hii ndio mmoja ya kazi yake, tutaona kua kuna uwezekano wa mfumo kuziba. Engine ikichoma mafuta mengi kupita kiasi, moshi hasaa carbon uzidi na kuziba mfumo. Kuliwasha gari ukiwa umekanyaga mafuta au kulipa mafuta linapowaka ni mwiko kw magari yaliyo na mifumo hii.
Magari ya Xtrail yanatumia mifumo electronic ya mafuta na kwa hivyo tatizo kidogo laweza leta majanga. Mfano, taarifa kuhusu jiko(combustion) kutoka kwa oxygen sensor zikikosa, injector umwaga mafuta mengi na kuzidisha carbon.
Kwa sababu ya i) madini nadra yanayotumika kuzitengeneza mifumo ya CAT converter na DPF, ii) sheria kali za kulinda mazingira hasaa ulaya na nchi zilizoendelea na pia iii) soko la kununua CAT/DPF mbovu mbovu ili kuvuna yale madini, mifumo hii ina bei sana mpya au used. Ile ya Xtrail niliinunua laki nane!
 
Nimekuelewa sana mkuu. Nikupongeze kwa kazi nzuri. Endelea kutujuza hasa pale unapotatua shida mbalimbali za haya magari.
 
Hbr za masiku WanaJF
Siku mingi sija changia uzi, mtanisamehe ila shughuli na kazi zinabana.
Leo nimeipata Xtrail ya petrol imesumbua kwa mda. 'Wasanii wameipigia show'; cat converter wameitoa matumbo, oxygen sensor wamebadilisha, head wameng'oa na mambo mengine mengi.
La kwanza kufanya pale ni kukagua 'vital parameters' kwa engine kama vile oili, air filter na kadhalika. Niligundua oili imechoka kweli na nyeusi sana - kumbuka gari lilikua kwa fundi siku tatu awali. Hili lilieleza mambo/observations flani nilipo liwasha gari. Engine Idle Speed ilikua juu na haijatulia; 900-970 rpm, exhaust ilinukia rich sana na mengine.
Diagnosis report ilitoa code zifatazo: P0172- fuel trim, too rich
P0120- throttle position sensor
P1123- ETC motor control circuit; mambo haya matatu yanahusu mfumo wa mafuta - fuel system. Observations zetu pale tulipoliwasha gari ziliashiria haya lakini bila kuyapata 'from the horses mouth' hakuna uhakika ila ni kukisia tu.
Bila kuongea mengi kuhusu ufundi au ujuzi wa mafundi, taratibu na itikadi za kiufundi ni muhimu kuzingatiwa. Mambo ya msingi kama kubadilisha oili na filter yana adhiri utendakazi wa engine na mifumo mingine. Ni wazi kwa kila mtu kua oili ulainisha vyuma na sehemu kwenye mfumo. Utelezi huu unahitajika kurahisisha mizunguko na kadhalika
Ubora/property hizi upotea oili inavyozeeka au inavyotumika kwenye mfumo - iwe engine, gearbox(manual au auto), diff, pump za hydraulic na pia compressors. Utapata unavyokaa na oili chafu kwenye mfumo, mfumo unapata uzito mkubwa na hapo kuhitaji nguvu zaidi kuendeleza mzunguko.
Zoezi la marekebisho kwa hili gari litaanzia na kuifanya engine service ndio tufanye tune-up ya mfumo wa mafuta. Ni muhimu kuelewa kua mifumo ya computer imewezeshwa kusoma, kusahihisha na pia kutarajia mabadiliko/mapungufu flani kwa ajili ya kuzeeka au mazingira.
Bila kujua hili, 'adaptation' za kawaida za mfumo zaweza chukuliwa kama matatizo na pale 'fundi' akaliharibu gari. Itaeleweka pia mambo haya yanafanyika kwa/na mitambo ya umeme. Mawasiliano yanategemea na kulingana na misingi flani ya kiufundi, kilele chake hua ni pale mtu anapotumia mfumo wa muunda gari - OEM, unaposhuka ngazi ndio mawasiliano yanavyokua ya kubahatisha.
Unapohisi gari/engine ina behave tofauti, ebu jiulize service iko due au kama ni baada yake, ni kipi kilichobadili kwa zoezi.
Pamoja!



Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu uwe unaweka na mawasiliano kabisa ili watu wakupe kazi.
 
Mkuu wacha niku add kwenye phone book yangu hembu fanya nipate namba yako nipo dar mm ni fundi umeme wa magari huwa nakuja sana moro..

Ishu ya nissan kwa upande wangu nilikuwa na mpango wa kuanzisha club au group la nissan.

Tena nawafanyia golo kwa watakao taka wawe wanaweza kuifanyia diagnosis popote pale watakapo kuwa dunian iki mkadi wawe na smartphone yao tuu tatizo likiwa kubwa nawapimia mm hata wakiwa nje ya nch na gari.

Juu ya dpf isikutishe sana.ukijua matumizi yake harafu wazungu sio wajinga sana dpf huwa wanaweka batan ukibonya inajisafisha yenyewe ishu ni kuwa wengi huwa hawajui na hawafanyi hivyo.

All in all solution yake ipo ikiziba inatolewa na kuidelet dpf kwenye control box mambo yana songa
LEGE unapatikana wapi dar, huwa nafuatilia post zako vizuri sana, una ujuzi mkubwa na ufundi wa magari is what i can conclude.
 
Back
Top Bottom