Kama nimekuelewa vizuri ndugu yangu ni kwamba ndio kwanza upo mwaka wa kwanza hapo UD na course unayo ichukua ni ya miaka mitatu na umepata scholarship ya kwenda nje miaka 4 tena ktk nchi ambayo ulishawahi kwenda na ukaishi for 6 months.
Ushauri wangu nikwamba andika barua ya kuhairisha masomo hapo UD then nenda nje kapige 4 years.
Why nimekushauri hivyo ni kwasababu hata utakapo maliza hiyo shule yako nje ya nchi ukirudi hapa nyumbani utakua umeongeza exposure.
Lapili nikwamba hata utakapo kujakuomba ajira utakua na chance kubwa kuajiriwa kuliko labda hata hao wenzako wanaomaliza mwaka huu, maana unaweza ukawakuta wapo wapo tuu. You know why unaweza kuajiriwa kuliko hao wenzako nikwasababu tayari ulishakua na hiyo experience ya kufanya kazi kwenye hiyo agricultural sector kama ulivyo eleza kwenye maelezo yako kwamba you worked for six months. Nakubwa zaidi umeenda kusomea the same related issues.
Halafu pia unawezakuta unaenda kusoma ktk university yenye higher status duniani kuliko hiyo UD ambayo daily kuna kiki za kijingajinga mara "Nondo" kajiteka mara paa "Msumari" umetoeka haupo chuoni. Then munaanza kudiscuss mambo ya kijingajinga badala ya kusoma.
Kubwa zaidi ndugu yangu kwa vile wewe Dume so huna skirt ya kuwavulia baadhi ya hao jamaa hapo UD ukute unamaliza na G.P.A yaajabu. Yaani haifai hata kwa mboga.
Kwa afya ya mafanikio yako ya baadae nenda mbele kwa mbele.