MBEBA MAONO KAJA
JF-Expert Member
- Dec 24, 2013
- 365
- 195
Ndugu wanajamii,
nimevumilia sana hatimae nimeona kuwa mficha ugonjwa mauti umuumbua na yamkini aliegundua ngazi alikuwa ni mfupi wa kimo.
nasema hayo kwa kuzingatia hali yangu ya maisha inavyozidi kudidimia kadri siku zinavyoenda kutokana na ukosefu wa ajira rasmi na hata mtaji wa kujiajiri.
Mimi ni msichana mwenye shahada ya fedha na uhasibu niliyoipata mwaka 2012 .
kwakweli nimejitahidi kuomba kazi sehemu mbali mbali na kufanikiwa kupata kazi ambazo kihakika hazijawa msaada kwangu ikizingatiwa kuwa nina majukumu ya kulea wadogo zangu baada ya mzazi kutoweka.
ombi langu kwenu wanajamvi, mnisaidie kupata kazi katika taasisi yoyote ya umma au binafsi ambayo no sustainable niweze kuokoa wadogo zangu kielimu.lakini pia hata kama mnaweza kunisaidia namna gani nipate mtaji nina uwezo pia wa kufanya na kusimamia mradi.
nimependelea taasisi ambayo ni sustainable kwasababu nimefanya kazi na taasisi binafsi ambayo ilikufa baada ya miezi sita kutokana na ubadhilifu hivyo kuniathiri sana .
natanguliza shukrani.
amini usiamini UTAISHIA KUAMBIWA NI PM ALAFU UTATOA NAMBA, NA KUAMBIWA UTUME CV AU MUONANE MWISHOWE UTAANZA KUOMBWA KITUMBUA...
amini usiamini UTAISHIA KUAMBIWA NI PM ALAFU UTATOA NAMBA, NA KUAMBIWA UTUME CV AU MUONANE MWISHOWE UTAANZA KUOMBWA KITUMBUA...
Pole na changamoto dadangu cha msingi ni maombi kingine unaweza kujiunga na businesss ya forever living ukaongeza kipato dadaangu kwa kuanzia mtaji wa laki 3 tu unaweza kunipm kama utakuwa interested na business uweze kuongeza kipato
Jipe moyo utashindaUsiache kumuomba mungu ipo cku atakuinuanajua wewe ndo kiungo cha familia ana namna ya kukuinua!
Ndugu wanajamii.
Nimevumilia sana hatimae nimeona kuwa mficha ugonjwa mauti umuumbua na yamkini aliegundua ngazi alikuwa ni mfupi wa kimo. Nasema hayo kwa kuzingatia hali yangu ya maisha inavyozidi kudidimia kadri siku zinavyoenda kutokana na ukosefu wa ajira rasmi na hata mtaji wa kujiajiri.e
Mimi ni msichana mwenye shahada ya fedha na uhasibu niliyoipata mwaka 2012. Kwakweli nimejitahidi kuomba kazi sehemu mbali mbali na kufanikiwa kupata kazi ambazo kihakika hazijawa msaada kwangu ikizingatiwa kuwa nina majukumu ya kulea wadogo zangu baada ya mzazi kutoweka.
Ombi langu kwenu wanajamvi, mnisaidie kupata kazi katika taasisi yoyote ya umma au binafsi ambayo no sustainable niweze kuokoa wadogo zangu kielimu, lakini pia hata kama mnaweza kunisaidia namna gani nipate mtaji nina uwezo pia wa kufanya na kusimamia mradi. Nimependelea taasisi ambayo ni sustainable kwasababu nimefanya kazi na taasisi binafsi ambayo ilikufa baada ya miezi sita kutokana na ubadhilifu hivyo kuniathiri sana.
Natanguliza shukrani.