Nishaurini ni Bora Kuoa au Kuzaa na Kuwatunza Watoto wangu

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Wadu mimi nafikiria kuwa na watoto tuu ambao nitakua nawachukua kwa mama zao na Kuwatunza huku nikiwapa matunzo yote yanayostahili pamoja na Kusoma shule nzuri.

Wengine wanasema siyo vizuri lakini nikiaangalia hata maisha ya Mjomba angu aliyeoa miaka minne minne iliyopita huku akipata misukosuko ikiwa pamoja na kuwa na mali nyingi sasa hivi amebakia kuwa mtu mwenye madeni mengi hapo ndo naona ni bora nizae watoto ambao nitawatunza mimi mwenyewe kwani wanawake wa sasa ni kama kucheza kamali.

Lakini Pia watu wanasema Umri ukifika mwenyewe utatamani uoe tuu lakini kwangu nimekua tofauti kidogo kwa sababu nina Case study za watu ambao wanapata shida kwa sababu ya kuoa watu wasio sahihi.

Ushauri wenu Pia nitausikiliza wadau wa Jamii forums.
 
mwanamke utakayezaa nae atawarithisha tabia watoto wako, sasa sijui huyo mzuri wa kuzaa nae utampataje?
 
Kama kwa dhati kabisa ya moyo wako, huoni haja ya kuoa na kupata watoto ndani ya ndoa,ni vema uka tii moyo wako.Lakini kuwa tayari na mawe utakayo rushiwa kutoka kwa ukoo wako na jamii kwa ujumla.
 
Daah! Post yako imejaq vitisho!
 
Ni gharama sana kuhudumia watoto ukiwa haushi nao. Tafuta mtu ambaye mtaelewana kitabia anzeni maisha jengeni familia. Watoto watakosa malezi bora kwa style hiyo unayoitaka wewe.
 
nakua nakaa nao mara baada ya kufikia Umri wa Kuanza Nursery school!
 
Sheria ya jamuhuri ya muungano wa tanzania haikuruhusu kukaa na mtoto kabla hajafikisha umri wa miaka 7 na kuendelea. Pia swala hilo linategemea na mama wa mtoto atakubaliana nalo vipi. Akikataa kukupa mtoto itakubidi uendelee kuhudumia.
 
Unadhani malezi mazuri ni elimu pekee?? hivi unajua athari za mtoto kulelewa na mzazi mmoja?? unahisi utakuwa umewatendea haki hao watoto kuwatenganisha na mama zao?, Na kama unahisi wanawake wote hawako sahihi kuoa, huoni kkuzaa ndo jambo kubwa na linalotakiwa uwe makini ujue unazaa na mwanamke wa aina gani?? ushawahi kuwaza kuumwa au kuugua kwa muda japo wiki au mwezi au kuperlize kabsaa??? (godforbid)..unadhani mama atakuwa hapo kukulea mpaka umri muda gani hata ukiumwa??...ni nani ataacha shughuli zake ati akuuguze kwa moyo wote n.k.?? Je? hayo unayofanya ndo Mungu ameamrisha? utakubali watoto wako watiwe mimba tu bila kuolewa?? halafu hao mabwana wabebe waototo wao?? tuliza akili yako tafuta mwanamke unaemjua vizuri tabia yake muanze maisha katika ndoa matatizo yapo hata wewe na wanao mnaweza kosana, unaogopa mali?? ushafikiria hao watoto ndo wanaweza kuwa chanzo ya kuja kuisambaratisha mali yako kwa kuwaamini na wakaenda tumbua na wanawake huko, ambapo wewe ulinyima hiyo haki ya kuwa na mwanamke, inakuja kutumiwa na wanawke wengine kwa njia nyengine...
 
Usioe mpaka uwe na uhakika! leo watoto wako bora uchelewe hata 40 years
 
Heshima yako mpendwa. Wewe waache tu wadanganyane na ubinafsi wao wa kutowafikiria watoto.
 
Ukithubutu kufanya hivyo, ipo siku utajutia maamuzi hayo. Mimi ni mmoja wa watu ambao hawakupata malezi ya mama kwa muda wa kutosha kwani baba yetu alituchukuwa tukiwa wadogo na kuishi naye maeneo tofauti aliyokuwa anahamishiwa kikazi. Changamoto zilizotupata zimekuwa funzo kwangu hata sitamani wala kufikiri kuishi peke Yangu kwani nawapenda watoto wangu na sipendi wakose malezi ya baba na mama. Nakushauri, muombe Mungu akuongoze kupata mke sahihi mtakaye saidiana kulea watoto wenu.
 
Back
Top Bottom