mimi si kuwa natetea ila kuna haja ya kuangalia hali ya mwenzio, vipi na binti hadija akisimamishwa kazi, naye achukiwe na mwenza?hapana, wasaidieni waume zenu, wanaume tupo makini sana jamani.
Maisha ni kama barabara, kuna mahali yananyooka sana tu, na kuna mahali yanapinda ile mbaya! Naamini ulimpenda sana wakati ana nafasi ya kukusaidia kwa hali na mali, endelea kumpenda hivyo hivyo kwa shida na raha! Usijidangaye eti labda ukimuacha utakujapata Malaika! Unanitia mashaka ya kuwa ulikuwa haujampenda yeye, bali vijisenti alivyokuwa anakutoa kule chuoni!Mwanaume ninae ishi nae nilikutana nae chuoni na alinisaidia sana kuanzia kimasomo mpaka matumizi yote.Hatujafunga ndoa. Baada ya chuo tuliajiriwa kwenye mashirika tofauti kazi ambayo naifanya mpaka sasa. Mwaka mmoja baada ya yeye kuajiriwa aliachishwa kazi kwa tuhuma ambazo hajaziweka wazi kwangu.
Mimi ndiye mfanya maarifa sasa. Kuanzia tule nini mpaka tuvae nini na ela ya bia nampa.Ameitiwa kazi nyingi ila hataki anasema ana mpango wa kuwa mjasiriamali dalili sizioni.
Nikifikiria hajanioa na nikimwangalia hana dalili hata ya kunikutanisha na watu wa kwao naona napoteza wakati.pia ukimwambia suala la ndoa anakuwa mkali hataki kusikia. Naletewa habari zake nyingi mbaya naogopa kumwambia tuachane kutokana na hali aliyonayo sasa. Amenilemea jamani. Nashindwa nifanyeje. Nakumbuka alivyokuwa msaada wangu nashindwa kumuacha.
Nakosa hata hamu ya mapenzi kwake. Namuona wa kawaida sana hana jipya.
Natamani apate kazi atakayoipenda(maana anachagua kazi na mahali kwa kisingizio cha ujasiriamali) ili hata nikimuacha asiwe na lawama. Kwa ukweli nilishamtoa rohoni siku nyingi nipo nae apate tu riziki yake anitoke.
Mwanaume wa kulala mpaka saa nne asubuhi!! Amenichosha jamani.!! Ananipotezea muda naona.
Naombeni ushauri ndugu zangu.
mzabzab sio kweli the guy is poor huyo ni mzembe na ndicho kilichomchosha huyu dada...mwanaume unalala mpaka saa 10am while mwanamke anagombania daladala 5am!!!LOVE will not only escape through the window aisee even through the ufa
Kwa ulalaji huo huyo hata ujasiriamali hatauweza
ha..ha..haaa! Girls jamani kuweni makini kwa style hii mta gegedwa mpaka basi!
Wewe unaenda nje ya mada..Hapa hakuna Poverty ila ni kujitakia..Kwa nini akatae kazi???Wewe unaweza kuishi kwa kulelewa huku unakataa kazi?? Na isitoshe huyu dada kamwambia wafunge ndoa ya kimya nayo bado anakataa...Lawama zote ziende kwa huyu kaka unless mdada kuna vitu anavificha
sasa wewe kwa akili yako unadhani huyu dada atakwambia kila kitu hapa....be smart!!!
Kaa nae chini na uzungumze nae huku ukionesha nia ya dhati katika mazungumzo yenu,mpe uwezo wa kuona mwanga zaidi wa kile unachokitaka na natumai atakuelewa na kila kitu kitakwenda sawa,maombi pia muhimu maana bila kumshirikisha Mungu katika mahitaji yako ni sawa na bure.Angeonyesha nia ya kunioa wala nisingetia shaka. Na angenioa ningejua hapa ni kwenye shida raha zitakuja. Tatizo hataki kusikia ndoa. Kwa hiyo hapa naona kama nimeshaachwa kuna mtu labda. Nimeshamwambia hata kama hatuna uwezo ndoa ifungwe hayo mengine ni majaaliwa. Hataki sasa hata kusikia.Umri unaenda familia haipo. Mwanaume hazeeki akija kuniacha nimeshachoka itakuaje?
Sijaamia kwake. Amehamia kwangu. Tena hata hajawahi kuuliza kodi nalipa kiasi gani.