Habari zenu jamani?
Mara nyingi nimekuwa nikija hapa pengine kujifurahisha au kumuombea mtu ushauri au kuisaidia jamii hii kwa ushauri. Lakini sikujua itafika siku nami seriously nakuja hapa kuomba ushauri.
Leo imenipasa kwakuwa nimetafuta jibu nikakosa sasa naona niombe ushauri! Kifupi nina shemeji/wifi yenu ambaye ni mchumba wangu yapata miaka miwili hivi nampenda sana tena sana.
Lakini kadri siku zinavyokwenda nakuwa simuelewi maana makubaliano yetu yalikuwa atafute kazi ambayo hawezi kwenda zamu ya usiku wala kusafiri na kuwa mbali na familia kwa muda mrefu kama mwezi na kuendelea kwa kua mama ni mlezi wa familia (baba, watoto, bibi, babu, mjomba, shangazi n.k) hivyo ni vyema usiku kuwepo nyumbani nakujua maendeleo ya familia.
Sasa kaamua kuingia jeshini kwa kujaza nafasi hiyo na ni kazi ambayo tulikubaliana asiende kutokana na sababu hizo hapo juu, kajaza akijua siko tiari kwa hilo.
Lakini pia amekuwa akijidai kakosea namba ya simu nakutuma sms ya majibu ya kutongozwa kwangu, namaanisha katongozwa zake huko ila anajidai kakosea namba ila karusha kwangu na kwa kuwa sihitaji league naamua kuchuna kama sikuona.
Hii anafanya mara kwa mara akijidai pengine kuonekana anakataa au anatoa jibu linalohitaji mwendelezo, leo kaja na mpya katuma sms kamkubali jamaa, najiuliza nimpigie nimuulize au niendelee kuchuna ama nitemane naye.
Jamii nayoishi nayo wakiwemo ndugu zangu wanamfahamu na wanawasiliana naye naona hata aibu kuachana naye naonekanaje sasa katika jamii yangu.
Pale geto amepamodify sana tu na katumia gharama zake na hata nguo zake na vitu vya thamani vya kwake viko geto kwangu kitu kinachonishangaza kwa nini asiniambie kama hataki uhusiano wetu uendelee kuliko njia anayotumia.
Nikimpigia simu anarespondi vizuri na kujidai anaupendo juu yangu.
Wakuu hapa nitoke vipi?