Nishaurini dhidi ya huyu mchumba wangu

Nishaurini dhidi ya huyu mchumba wangu

julius mahinya

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
1,152
Reaction score
384
Habari zenu jamani?

Mara nyingi nimekuwa nikija hapa pengine kujifurahisha au kumuombea mtu ushauri au kuisaidia jamii hii kwa ushauri. Lakini sikujua itafika siku nami seriously nakuja hapa kuomba ushauri.

Leo imenipasa kwakuwa nimetafuta jibu nikakosa sasa naona niombe ushauri! Kifupi nina shemeji/wifi yenu ambaye ni mchumba wangu yapata miaka miwili hivi nampenda sana tena sana.

Lakini kadri siku zinavyokwenda nakuwa simuelewi maana makubaliano yetu yalikuwa atafute kazi ambayo hawezi kwenda zamu ya usiku wala kusafiri na kuwa mbali na familia kwa muda mrefu kama mwezi na kuendelea kwa kua mama ni mlezi wa familia (baba, watoto, bibi, babu, mjomba, shangazi n.k) hivyo ni vyema usiku kuwepo nyumbani nakujua maendeleo ya familia.

Sasa kaamua kuingia jeshini kwa kujaza nafasi hiyo na ni kazi ambayo tulikubaliana asiende kutokana na sababu hizo hapo juu, kajaza akijua siko tiari kwa hilo.

Lakini pia amekuwa akijidai kakosea namba ya simu nakutuma sms ya majibu ya kutongozwa kwangu, namaanisha katongozwa zake huko ila anajidai kakosea namba ila karusha kwangu na kwa kuwa sihitaji league naamua kuchuna kama sikuona.

Hii anafanya mara kwa mara akijidai pengine kuonekana anakataa au anatoa jibu linalohitaji mwendelezo, leo kaja na mpya katuma sms kamkubali jamaa, najiuliza nimpigie nimuulize au niendelee kuchuna ama nitemane naye.

Jamii nayoishi nayo wakiwemo ndugu zangu wanamfahamu na wanawasiliana naye naona hata aibu kuachana naye naonekanaje sasa katika jamii yangu.

Pale geto amepamodify sana tu na katumia gharama zake na hata nguo zake na vitu vya thamani vya kwake viko geto kwangu kitu kinachonishangaza kwa nini asiniambie kama hataki uhusiano wetu uendelee kuliko njia anayotumia.

Nikimpigia simu anarespondi vizuri na kujidai anaupendo juu yangu.

Wakuu hapa nitoke vipi?
 
ndugu yangu ushauri tafuta kichaka chako mwenzio kashapata ... usilazimishe penzi mkuu... pili kufanyiwa kutengenezewa geto lako haina maana ndo mapenzi hayataisha.... kujulikana na nduguzo isiiwe sababu ya wewe kuendelea na huyo bibie...... mwite muuongee aaeleweki chapa lapa do other thing... maisha yana mengi ya kufanya usilazimishe penzi mkuu hata kidogo...

anaweza kusema kuwa anakutania mmmh hoping unaweza mwonya vikali asirudie hilo kosa....... afu na wasi wawsi unadate mpenzi mwenye miaka 23 yahh
 
Anataka muachane kitu uzima na sababu anakupa tena ya maandishi kabisa. wewe tu ndio unatakiwa uelewe. Hicho cha jamii kukuonaje, waache waone watakavyo wao.. hayo ni maamuzi yako na wewe ndio utayaishi hayo maisha, jamii wakati huo ndio itakuwa inakucheka, au hata sasa hio jamii huenda kuna mambo inafahamu kuhusu huyo binti ila hawakuambia, kwa nini? kwa sababu ndivyo jamii ilivyo. Fanya yale yanayokuridhisha moyo wako Mkuu. na unasonga mbele.
 
mkuu The Boss that is possible only kama jamaa huyo sio demu wake wa kwanza, I mean jamaa kama ana experience otherwise he cant....!
 
Last edited by a moderator:
Usipomjibu hiyo msg utazidi kumchanganya zaidi...nadhani anapenda attention ndo maana anakutumia hizo msgs....lakini pia anza kufikiria "exit strategy".
 
Nafatilia kwa makini sana ushauri wenu maana naamini ntapata jibu sahihi hapa. mimi si wa kwanza kwake naye si wakwanza kwangu ila kuna stage inafika huwezi kuendelea kuwa wa hivyo lazima uwe na msimamo katika uhusiano. MISS CHAGA bwana kwa nini unahisi ni 23 yrs! kama uko sahihi hivi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Na vimbwanga hivyo anavyokufanyia humuelewi tuu !!!

Atakuwa anakushangaa kwa nini humuachi akaendelea na maisha yake na mpenzi wake mpya..!!
 
Na vimbwanga hivyo anavyokufanyia humuelewi tuu !!!

Atakuwa anakushangaa kwa nini humuachi akaendelea na maisha yake na mpenzi wake mpya..!!

Si anajidai kakosea sms sasa mimi ntajibuje sms siyo yangu kwa nini asiseme mimi nina mtu mpya?
 
Anacheza na akili yako huyo na ameshajua unampenda sana.. Sizi mkuu kwa muda, kata all means of communication kwa muda wa wiki or mbili, kama anakupenda for real atahangaika ila ukiona kimya hapo nafikiri kila mtu huwa na Plan B,C,D,E hadi Z.
 
Give her a break ili ajue kama una umuhimu kwae au lah! utapata majibu mkuu usiangalie watu watasemaje?be yourself
 
Habari zenu jamani?

Mara nyingi nimekuwa nikija hapa pengine kujifurahisha au kumuombea mtu ushauri au kuisaidia jamii hii kwa ushauri. Lakini sikujua itafika siku nami seriously nakuja hapa kuomba ushauri.

Leo imenipasa kwakuwa nimetafuta jibu nikakosa sasa naona niombe ushauri! Kifupi nina shemeji/wifi yenu ambaye ni mchumba wangu yapata miaka miwili hivi nampenda sana tena sana.

Lakini kadri siku zinavyokwenda nakuwa simuelewi maana makubaliano yetu yalikuwa atafute kazi ambayo hawezi kwenda zamu ya usiku wala kusafiri na kuwa mbali na familia kwa muda mrefu kama mwezi na kuendelea kwa kua mama ni mlezi wa familia (baba, watoto, bibi, babu, mjomba, shangazi n.k) hivyo ni vyema usiku kuwepo nyumbani nakujua maendeleo ya familia.

Sasa kaamua kuingia jeshini kwa kujaza nafasi hiyo na ni kazi ambayo tulikubaliana asiende kutokana na sababu hizo hapo juu, kajaza akijua siko tiari kwa hilo.

Lakini pia amekuwa akijidai kakosea namba ya simu nakutuma sms ya majibu ya kutongozwa kwangu, namaanisha katongozwa zake huko ila anajidai kakosea namba ila karusha kwangu na kwa kuwa sihitaji league naamua kuchuna kama sikuona.

Hii anafanya mara kwa mara akijidai pengine kuonekana anakataa au anatoa jibu linalohitaji mwendelezo, leo kaja na mpya katuma sms kamkubali jamaa, najiuliza nimpigie nimuulize au niendelee kuchuna ama nitemane naye.

Jamii nayoishi nayo wakiwemo ndugu zangu wanamfahamu na wanawasiliana naye naona hata aibu kuachana naye naonekanaje sasa katika jamii yangu.

Pale geto amepamodify sana tu na katumia gharama zake na hata nguo zake na vitu vya thamani vya kwake viko geto kwangu kitu kinachonishangaza kwa nini asiniambie kama hataki uhusiano wetu uendelee kuliko njia anayotumia.

Nikimpigia simu anarespondi vizuri na kujidai anaupendo juu yangu.

Wakuu hapa nitoke vipi?
Usifanye mahusiano kwa kuangalia jamii, utaishi na BOMU na litakulipukia mwenyewe. Jamii haitalala naye kitanda, shuka na pillow moja mpaka kifo kitakapowatenganisha. Ni wewe na yeye. Chukua tahadhari. Acha
 
Si anajidai kakosea sms sasa mimi ntajibuje sms siyo yangu kwa nini asiseme mimi nina mtu mpya?

Hana ujasiri wa kukutamkia kwamba ana mtu mpya..
Ni ngumu kumwambia mpenz wako muachane kama hakuna baya alilokufanyia. !! Kaona akujuze kwa hizo texts..!!

Mwanamke akiwa na mapenzi na wewe utamjuaa tuu.. Lazima akuheshimu!!!
 
Back
Top Bottom