Nisamehe mpenzi wangu

Nisamehe mpenzi wangu

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,852
RUDISHA FURAHA YANGU.

1) Najua nilikosea,kukudhi mpenzi wangu.
Kweli sikukudia,kukutesa ndoto yangu.
Hakika ninajutia,ninatubia kwa mungu.
Nisame mpenzi wangu,rudisha furaha yangu..

2) Soni pakuelekea,yamefumba macho yangu.
Nahisi ninapotea,mbelyangu kuna kiwingu.
Hakuna wakunyokoa,ila ni wewe mwenzangu.
Nisame mpenzi wangu,rudisha furaha yangu.

3) Huoni ninapotea,usiniache mwenzangu.
Nikae nikijilia,nikiyapata machungu.
Sisi wenye kukosea,ndivyo aliumba mungu.
Nisame mpenzi wangu,rudisha furaha yangu.

4) Tena ninakuapia,sitokwacha haki ya mungu.
Kama nikikukimbia,hilo kwangu liwe rangu.
Lakini niliumia,uliponyacha pekyangu.
Nisamehe mpenzi wangu,rudisha furaha yangu.

5) Penzi letu laelea,likipigwa na ukungu.
Ndo hivyo laangamia,laozea kwa uvungu
Moyo wakulipukia,huku ukifungwa pingu.
Nisamehe mpenzi wangu,rudisha furaha yangu.

Shairi=RUDISHA FURAHA YANGU.

Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
 
Back
Top Bottom