"Nisamee Mke wangu" SIMULIZI

"Nisamee Mke wangu" SIMULIZI

Mr Acky

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2019
Posts
234
Reaction score
313
Author: Akida S. Rambao
Contact: 0658328596
Email: akidasiri@gmail.com

Naweza sema nilijiona mtu sahihi nisiyekuwa na makosa, lawama nyingi niliziweka kwake. Nilimtuhumu kwa kila tukio lisilofurahisha na wala sikujali alipo kimbilia ndani au kutoka nje. Kumbe alikuwa akienda kulia na kupunguza machungu ya matendo yangu niliyo yahalalisha wakati yalikuwa ni haramu. Nikabaki nimetulia na kuendelea na mambo yangu sura nikiikunja hasira ikitawala machoni kwa kudhani sasa na dharaulika kwanini kaondoka? itakuwa hivi mpaka lini? Nikaishia kula chakula chake alichopika na kuoga maji ya malashi aliyoniwekea na kujitupa kitandani nikimuachia mgongo, wakati yeye akijisogeza na kunikumbatia kama mtu aliye sahau niliyotoka mfanyia muda mfupi ulio pita.

Asubuhi sikujisikia kumsalimia mpaka alipo anza kisha kuondoka zangu nikishinda bila hata kumpigia simu ya bahati mbaya niliona sawa lakini yeye alithubutu kusema “Samahani mume wangu unaendeleaje na kazi? Ni samee jana nilikupazia sauti” au akisema “Mume wangu samahani usiku nikupikie chakula gan?” Niliishia kubinjua domo na kujishauri kujibu au kuacha kabisa lakini bado nilikaa na kumuita ‘Mke wangu’ sijui nilitaka nini zaidi kilichojificha zaidi ya furaha iliyopotea bila kujua sababu, ninachokijua tulikuwa kama kumbikumbi kwa mahaba enzi za uchumba na hata siku za mwanzo kabla ya kujifungua mtoto wetu wa kike! Sasa imekuwaje?!

Baada ya watoto hawa wawili tu sikuona urembo wake upendo wangu ulichuja. Au ni kazi iliyonitawala usiku na mchana na kunifanya niwe mpofu nisiye ona mazuri yake nisipate muda wakutosha nikajua hali yake na yale ayapendayo kutimiziwa?! Au yule kiongozi Mzee Maneno? asiye isha maneno ya lawama hata kwa kosa dogo ahh! na asiye na shukrani, asiyependa kusikia utetezi mbele yake mwenye kuagiza kazi na akizitaka ziishe kwa wakati bila kujali utamaliza saa Je! Ndiye aliyenifanya nisione furaha mbele ya mke wangu niliyemuacha macho mpaka usiku akisubiri nirudi ndipo ale na kulala, nilimtesa lakini mbona sikuona? Licha ya kunilaumu kuwa sina muda nae wala wa watoto mimi sikuona cha maana zaidi niliyawaza niyapendayo kuyakosa.

Nilibaki kuendelea kujiwazia bila majibu nikiwa kwenye kiambaza cha mlango moyo ukinidunda nisijue la kufanya wakati huo sauti yake ya kilio cha chini chini cha uchungu ikishambulia masikio yangu ikimaanisha Uonevu na Usaliti. Kwa mara ya kwanza nilihisi kitu tofauti kikiingia moyoni mwangu na kuona hatia huruma ikaniingia na kumfata alipo na kumuita kwa jina lake nikamwambia “…mke wangu naamini wewe sio mjinga bali mjinga ni mimi niliyejitia upofu nisione juhudi zako katika familia hii na kutia pamba masikio nisisikie maneno yako na kuyapa maana na kuutia ganzi mwili wangu nisisikie msisimko wako unapo nigusa tafadhari naomba uniambie wazi leo na mimi nikwambie yangu ili tuwe kitu kimoja tena”

“Mume wangu wewe huyo leo unataka suruhu na mimi, hapana nimechoka nafikiri unataka kucheza na akili yangu, samahani sina muda wa kupoteza nimekuvumilia nikakupa utu wangu na nafasi lakini hukujali inatosha yupo mwanamke atakaye kufaa naomba niende” aliongea mke wangu akimaanisha kwa kuchukua begi mwanangu mdogo akiwa mgongoni na mkubwa akiwa kashikwa mkono, chozi lilianza kunitelemka sikuwahi fikilia kuna siku familia yangu itagawanyika , nikaongea “Mke wangu jalibu kuniamini nahitaji msaada wako wa kuniweka sawa kama baba anaejali familia yake mimi nimeipoteza sifa hiyo na sikulitambua hilo kwa miaka nilichokuja gundua ni kuwa wewe ni mwanamke wa thamani kubwa sana uzuri wako uliochujuka umesababishwa na mimi kutokukupa thamani yako kutokukupa matunzo na mapenzi ya dhati lakini pia natakiwa kujifunza kusamee na kutoa vitu moyoni kwa sababu yanapukutisha na kula nguzo ya upendo”

Sasa nikiwa nimemsogelea na kumshika bega nikimtazama kwa jicho la ombi “Tafadhari nipe nafasi nyingine yakujirekebisha nakuhakikishia nitakuwa mume wa pekee kuwahi kutokea duniani” niliongea tayali magoti yakiwa sakafuni nimelishika dela lake nikimzuia “Mume wangu hapana hukuwahi nipenda huo ni ukweli mweupe, nilikupa moyo wangu ukausigina na kuuchana chana hukuwahi nionea huruma wala kunijali wala kunifanya kuwa mke wako” aliongea macho yakiwa na hasira machozi yakimtiririka mashavuni.

"Mume wangu ngoja niende kwetu mana sikufukuzwa na wewe utakuwa huru hapa kufanya utakalo kama kuna mwanamke mzuri mwenye sifa unazozitaka muite wala usikutane nae vichochoroni atakupikia na kukufanyia kilaunalovutiwa nalo kwakheri” alimaliza mke wangu na kuniputa mkono nilioshikilia dela huyo bila kugeuka akaukabili mlango wa geti nilichokisikia ni “Mbaaa!” sauti ya mlango huo uliopigizwa alfajiri hiyo. Nilikuwa tweeee mdomo wazi nimeduwaa ilinichukua hata dakika nyingi mana sikutazama muda halisi kuamini kuwa mke wangu Mama Shukuru ameondoka kweli, nilikurupuka kuwahi shuhudia nje lakini palikuwa peupe peee kama mtu aliye yeyukaa.

Kwa mara ya kwanza niliona moyo wangu namna nilivyouumiza nilibaki kuuliza wee moyo ulikuwa wapi siku zote? Siku hiyo ya juma mosi sikuweza kwenda kazini mwili ulikuwa mzito mchungu kila sehemu nilibaki kupiga simu lakini bila kupokelewa meseji zisizojibiwa Loo! siku ile, ilinibidi nipige simu kwa wazazi wa mwanamke na kuongea kila nilichokifanya bila kificho nikilia kama mwehu kuomba msaada wao, sikuacha nilipiga simu kwa dada zake, kaka, marafiki na majirani nikiomba msaada wa kumshawishi mke wangu arudi nyumbani.

Masaa kumi na mbili yalipo kata nikiwa sebureni nikisubiria tumaini nisilolijua nikijilaani kwa kujifanya kipofu niliona mlango ukifunguliwa na mke wangu akiingia akitabasamu, sikuamini alikuwa mke wangu mama Shukuru akitabasamu nilinyanyuka nikiona kama ndoto nikamfata na kumkumbatia. “Nimekusamee mume wangu na tumaini sasa utakuwa unajua mwanamke anataka nini toka kwa mumewe” aliongea mke wangu nami nilibaki kutingisha kichwa kuyakubali maneno yake.

Mwisho
 
Nani kavutiwa na Simulizi ya kubuni, na anaushauri upi kwa Mwandishi wetu aliyejitoa kimasomaso kutimiza ndoto zake za Uandishi?

Tafadhari usisome tu Bali acha Maneno yako ya kumjenga na kumtia moyo
 
Umeibuni ukiwa wapi? Nzuri sana hii

The Hidden Truth (Ukweli Uliofichika)


Ifuate hi Ni riwaya yake ya kijasusi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom