- Thread starter
- #21
Sasa hapo we ndo una matatizo ya kutokupenda maana wote wanaokuja wanakupenda ila wewe huwapenda upo nao tu. Sijui unayemsubiri atakuja na tofauti gani maana hutampenda tena hadi utazeeka. Jitambue na ujifunze kupenda. Hakuna utakayempenda akawa amekidhi vigezo vyako vyote. Wa namna hiyo wameshaoa au wana watu. Angalia kama una vigezo vitano halafu akawa ana sifa 3 zinazofaa basi huyo ndo anakufaa then zile 2 zifanyie kazi umsaidie abadilike akufae. Kumbuka kuwa wanaume nasi tuna vigezo kwako kama haufai tutakuacha tu hata ujitahidi vipi.
ni kitu halisia lkn,na wengi chawakumba sana ndugu yangu