Nisaidieni majibu ya maswali magumu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni majibu ya maswali magumu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MADORO, Dec 30, 2011.

 1. M

  MADORO Senior Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Watanzania nisaidieni naomba msaada wa majibu wa maswali haya magumu.
  Nilipokuwa nakua na kupata ufahamu wa akili timamu na kuitwa mtu mzima ingawa utu uzima sio kuhesbu idadi ya miaka aliyozaliwa mtu tu, nimekuwa nikisumbuliwa na vitu vingi vilivozidi kuisonga akili yangu na wakati mwingine kusababisha kichwa kuuma.vitu ambavyo nimekuwa nikikwamama mara kwa mara, na ndio maana leo nimeamua kuandika waraka huu kwenu watanzania mnisaidie kupata majibu yake,maswali haya ni pamoja na, iko wapi nchi ya Tanganyika tuliyoirithi kutoka kwa wakoloni, iko wapi nchi inayoitwa Tanzania bara? Nifungulieni vifungu vya kisheria nipate kufahamu niko hoi hapa, uko wapi uhuru wa kikatiba wa kusema kwa watanzania? Iko wapi nchi huru ya amani inayozungumzwa na baadhi ya viongozi hapa nchini? Yapo wapi maisha bora kwa kila mtanzania? Uko wapi uzalendo aliouacha baba wa taifa. Iko wapi nchi aliyoiacha baba wa taifa yenye mito,milima, mabonde, mistu na raslimali iliyotukuka? Ziko wapi mbuga za wanyama zinazomilikiwa na watanzania? Iko wapi thamani ya pesa ya watanzania? Iko wapi siasa bora nchini Tanzania? Uko wapi utawala bora? Wako wapi waandishi wanazingatia taaluma yao kama walivyofundishwa darasani? Wako wapi viongozi bora katika nchi hii? Wako wapi viongozi wanaojali mali ya umma katika nchi hii?wako wapi walimu bora katika nchi hii? Wako wapi wezi katika nchi hii , ni nani wa kuwashughulikia wezi hao kama wapo? Kwanini Tanzania ni nchi ombaomba? Kwanini Tanzania ni nchi maskini? Kwanini watu wake ni maskini? Kwanini tunaishi bila uhuru wa kusema?iko wapi ridhaa ya watanzania kuwachagua viongozi wanaowataka? Tutawapata wapi viongozi wazalendo? Nini hatima ya nchii siku ccm watakapoamua kuachia madaraka itaachwa ikiwa salama?
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona umefanya summary ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa humu JF na majibu kutolewa! Ungekuja on incremental basis ingekuwa afadhali ila umekuja na maswali meeengi hata wa ktoa majibu atachoka ila majibu yapo humuhumu labda tu huyaoni!
   
Loading...