Nisaidieni kuhusu Toyota Voltz; Uimara, mafuta, matunzo, bei

Financial Analyst

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
1,605
2,748
1686036489635.png

Toyota Voltz​

Habarini wakubwa,

Nisaidieni kujua kuhusu voltz. Ukulaji wake wa mafuta, matunzo yanayofaa, disadvantages zake na advantages

Bei ya voltz 2008, 2006 na 2002.

Karibuni wakubwa.
 
Ni gari nzuri sana kwanza ina uzani mzuri wa kuhimili barabarani ukilinganisha na gari za saizi yake, ipo juu kiasi, bodi ni imar/ ngumu kama ya rav4 old, comfot iko vizuri pia, dashboard yake iko poa kama za magari ya ulaya, spea zipo za kumwaga, engine yake ni 1ZZ-FE ambayo ipo ktk Premio, Wish, Allion, Rav4, Fielder, nk. Ambazo mafundi hadi chini ya muembe wapo.

NB: Uzima wa gari ni matunzo.
 
Ni gari nzuri sana kwanza ina uzani mzuri wa kuhimili barabarani ukilinganisha na gari za saizi yake, ipo juu kiasi, bodi ni imar/ngumu kama ya rav4 old, comfot iko vizuri pia, dashboard yake iko poa kama za magari ya ulaya, spea zipo za kumwaga, engine yake ni 1ZZ-FE ambayo ipo ktk Premio, Wish, Allion, Rav4, Fielder, nk. Ambazo mafundi hadi chini ya muembe wapo.
NB: Uzima wa gari ni matunzo.
Zina muundo mzuri sana.

Vp lakini, nilisikia mtu anasema zilitolewa katika uzalishaji, kwa hio eti spea zake ni za shida dukani,

Hii ni kweli mkuu?
 
Zina muundo mzuri sana.

Vp lakini, nilisikia mtu anasema zilitolewa katika uzalishaji, kwa hio eti spea zake ni za shida dukani,

Hii ni kweli mkuu?
Muonekano ni mzuri sana tu, tena ni nje na ndani.

Uzalishwaji inawezekana maana za mwisho kuziona sokoni ni za 2004.

Kuhusu spea part, zipo nyingi kila kona maana haina spea za kwake pekeyake, Toyota zinaingiliana spea, hivyo zipo za kutosha na ndio maana zipo nyingi barabarani.

Usiwe na khofu kuhusu gari hiyo kwa Tanzania mkoa wowote ule.
 
Habarini wakubwa,

Nisaidieni kujua kuhusu voltz. Ukulaji wake wa mafuta, matunzo yanayofaa, disadvantages zake na advantages

Bei ya voltz 2008, 2006 na 2002.

Karibuni wakubwa.

Achana nayo mkuu gari ya zamani hii hata uzalishaji wake umesitishwa..so utahangaika spea
Pia re-sale value yake ni ndogo mno

Alternative chukua wish kuanzia 2010
 
Hahahhah nashangaa, mkuu naipenda voltz, mimi sio mtalaam wa magari, kwa hio nisihofu kuhuusu spea right?, mimi i dont care about resale price
Unaipendea nini hiyo gari mkuu? Isije kuwa kukosa exposure ya kujua magari mengine kunakuponza ndio maana unataka kununua hilo shipa. Hebu tuanzie kwanza kipengele kimoja baada ya kingine mfano driving experience, je umeshawahi kuiendesha?

Pili, muonekano ( it’s one of the worst looking)! Tatu, fuel economy sio one of the fuel economical. Nne, performance yake sio nzuri ukilinganisha gari za same class.

Tano, spares zake pia sio cheap. Na mwisho kabisa umejiuliza Kwann hiyo gari ilizalishwa ndani ya muda mfupi(2002-2004) kuwa discontinued baada ya kupata mauzo kiduchu sana ya gari 10k tu ?
 
Pia gari walizouza ni elfu kumi, na zile walizotengeneza baada ya miaka miwili bado zipo sokoni hazijanunuliwa, waliziyeyusha au ziliendelea kuuzwa?
 
Back
Top Bottom