Nisaidieni jamani

Nisaidieni jamani

pachambili

Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
48
Reaction score
16
Habari zenu hii ni mara yangu ya kwanza kuingia katika mtandao huu naomba mnipokee. licha ya ugeni wangu ila nimekuja nina shida nahitaji mawazo yenu.

Mimi ni msichana wa miaka kati ya 25-30, nimekuwa na mwanaume ambaye tumekuwa na urafiki wa kimapenzi sasa ni muda wa mwaka mmoja na miezi nane, huyo jamaa yeye ni raia wa Kenya.

kwa mara ya kwanza nilivyokutana nae aliniaweka wazi kuwa anawatoto wawili wa kiume na wakike ila akaniambia kuwa mke wake alimkimbia na aliolewa na mwanume mwengine.

Nilimpokea yeye na watoto wake ingawa watoto walikuwa Kenya ila nilichukua nafasi ya mama kwa kuwafanyia hata shopping na kutuma vitu kuwafikia huko walipo.

katika familia yao wanaonifahamu ni wadogo zake na kaka zake na wajomba zake ila plan zetu ilikuwa mwezi wa sita mwaka huu niende nae kwao, lakini ilivyofika aliondoka akaniambia alipata msiba hivyo anakwenda kuzika itakuwa siyo vizuri kuna msiba na yeye ndiyo anipeleke kwa mama yake kama kunitambulisha.

Nilikubaliana naye ila cha ajabu alikaa huko miezi miwili lakini hakukuwa na mawasiliano kama ilivyokawaida katika hiyo miezi miwili alinipigia simu mara tano tuu.

Baadae alirudi na alivyokuja aliniomba msamaha kuwa simu yake ilipata matatizo, sikujibu kitu nikaamua kufanya uchunguzi. mwezi huu wa nane nimegundua kuwa huyu jamaa anamke na watoto wanne, nilijua kwa kuchukua passport yake na kuangalia kule nyuma kuna vitu amejaza.

Nikazipiga zile namba nikaongea na huyo mwanamke aliumia sana mama wa watu alilia sana kwenye simu kiukweli nilijisikia vibaya sana akanimbia huku nilipo inafikia kipindi mimi na watoto tunalala njaa, kumbe yeye anafanya starehe huko, nikamjibu kwa kweli mimi nimekuwa msaada sana kwa watoto wako kwani hata ada za mwaka huu mimi nimetoa kwa kuwa jamaa mambo yake hayakwenda vizuri.

Yule dada akaniambia nimpe muda then atanijibu, ila baadae akanipigia akaniambia yeye ni mama wa nyumbani hana kipato chochote basi niendelee tuu kumsaidia ila hakugusia swala la mume wake.

Baadae nilikaa na huyu mwanaume nikamuuliza kwanini alinificha muda wote huo kama anamke akadai kuwa kuna matatizo ya kifamilia hivyo nimwachie yeye anajua jinsi ya kuyatatua, nilimkomalia sana inabidi aniweke wai kuwa yeye aliplan toka mwanzo kuwa awe na wake wawili mmoja kwa kuwa hana kazi basi wapili akiwa na kazi watasaidiana kwenye maisha.

Wapendwa mimi naombeni ushauri licha ya nyumbani kwetu nikimanisha wazazi wanajua ni rafiki yangu na plan zetu ilikuwa mwezi wa tisa aje kujitambulisha rasmi, sasa wapendwa kwa uongo wote huo huyu ni mwanaume sahihi?

Kitabia ni mpole ila sasa amekuwa na tabia ya kuwa na wasichana wasichana wengine napo nilipo mbona akaniambia ni wasichana anawapata kwenye mtandao wa Twoo na nisipokuwepo kwake anawapeleka hao wasichana hadi kwake.

Naombeni ushauri wenu nifanyeje anadai sheria ya kwao inaruhusu wake wawili ila dini yetu hairuhusu hivyo, na mimi mwenyewe siko tayari kuwa mke wapili, ila muda mwingine naona kwakuwa ameshanipotezea muda simwezi kupata tena mtu mwingine na miaka inakimbia.

Na umri wa huyu mwanaume ni kati ya 40-45
 
Mdogo wangu, dada yangu..aaah! Kweli mapenzi ni upofu..!
 
pole sana...........bora utulie tu.....usipende kupenda watu usiowafahamu eti umemkuta kwenye one sjui twoo, tabu nyingineni za kujitakia ati
 
Haya hao mnaowasifia kila kikicha eti wameendelea ndio hao wanaohemea kwa dada zetu. Pole dadangu kaza buti achana na mkenya huyu utakuja kujuta maishani kwa maamuzi yako yenye upofu.
 
pole sana...........bora utulie tu.....usipende kupenda watu usiowafahamu eti umemkuta kwenye one sjui twoo, tabu nyingineni za kujitakia ati


asante sana kwa ushauri lakini mimi na yeye hatujakutana kwenye mtandao wowote tulikutana wenyewe tuu tukazoeana na ikafikia mpaka hapo. asante
 
Haya hao mnaowasifia kila kikicha eti wameendelea ndio hao wanaohemea kwa dada zetu. Pole dadangu kaza buti achana na mkenya huyu utakuja kujuta maishani kwa maamuzi yako yenye upofu.

asante kaka sasa hivi upofu sina naona naanza kuona mwanga mapema ila unajua uraiani pagumu kuanza tena ila namuomba Mungu anisaidie sana
 
Mimi ni msichana wa miaka kati ya 25-30, ......
Nombeni ushauri wenu nifanyeje anadai sheria ya kwao inaruhusu wake wawili ila dini yetu hairuhusu hivyo, na mimi mwenyewe siko tayari kuwa mke wapili, ila muda mwingine naona kwakuwa ameshanipotezea muda simwezi kupata tena mtu mwingine na miaka inakimbia.

cc:lara 1
 
dada pole saaana. ila mungu ndo mwenye majibu kukuoesha hayo kuna maana saaana katika maisha yako. pata muda wa kuongea na mungu kwa kumaanisha utajibiwa tu kama anafaa ama la. ila muondoe kabisa unapoomba ilg mungu akuoneshe mwenyewe apendavyo.
 
Hakuna mapenzi hapo huyo ni mnafiki anataka atumie pesa! Zako.ni kicheche kama vicheche wengine piga chini fasta.muda unao wa kukaa na kumwomba mungu atakupa mume wako..wakenya ni vichecheyuko kimaslah zaidi. Usiogope kuhusu kufahamika kwake kwa wazaz wako,fikiria maisha yako jua unataka kujiingiza kwenye matatizo ya kumlelea familia..uzuri na raha ya mwanamke utunzwe kama malkia na siyo kuumiza akili etifamilia kesho itakula nin, cjui ada nitapata lini looo. .mwanamke unatakiwauwaze mastayle ya mapenz na jinsi ya kumnyenyekea mumeo. ..asikuzeeshe bure na mawazo. .mwambie kama vipi apite vileeee akuondolee uchuro hapa. .ujana wake ale na nan na wewe uzee aje kula mturuhusu..mfyuuuuzake
 
Heheheheh

Unatumika na wewe unafumba macho

Kama unaona umri unakimbia kubali akuoe ili uhudumie mkewe na wanae

yaani na ndiyo maana niliamua kujiunga humu ili kupata mawazo, asanteni macho yangu nimeshayafunua yaani kama ni jua la asubuhi nimeshaliona. asante
 
Pole sana, ushauri gani unaotaka hapa baada ya kudanganywa kiasi hiki!? Mwambie afungashe virago vyake haraka sana toka kwako. Asikutafute kwa namna yoyote ile.
 
pachambili, huyo sio mume ila anakutumia wewe kuweka unafuu ktk familia yake, ni afadhal sana maumivu utakayopata sasa baada ya kumuacha kulikon yajayo baada ya kuolewa, na anasisitiza maana kuhusu ndoa mbili coz kwako anauhakika na hela, ila blieve me unatumika mama, relax utampata amua leo na utulie, wako anakuja huyo wa watu
 
Back
Top Bottom